Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 64

ثُمَّ تَوَلَّيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۖ فَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَكُنتُم مِّنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Kisha mkageuka baada ya hayo. Na lau kama sio fadhila za Allah na rehema zake kwenu mngekuwa miongoni mwa wenye hasara



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 105

مَّا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَلَا ٱلۡمُشۡرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ خَيۡرٖ مِّن رَّبِّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَخۡتَصُّ بِرَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Watu wa Kitabu waliokufuru na washirikishaji hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu. Na Allah humkusudia (kumpa) rehema zake amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 163

وَإِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ

Na Allah wenu ni Allah mmoja tu. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa yeye tu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 74

يَخۡتَصُّ بِرَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Anamhusisha kwa (kumpa) rehema zake amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 157

وَلَئِن قُتِلۡتُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوۡ مُتُّمۡ لَمَغۡفِرَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَحۡمَةٌ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Na ikiwa mtauliwa katika njia ya Allah au mkifa, hakika msamaha na rehema zitokazo kwa Allah ni bora kuliko yote wanayoyakusanya



Sourate: ANNISAI 

Verset : 29

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَٰرَةً عَن تَرَاضٖ مِّنكُمۡۚ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمٗا

Enyi mlioamini, msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa tu kama mali hizo ni biashara (inayofanyika) kwa maridhiano yenu. Na msijiue. Hakika, Allah ni mwenye rehema kwenu



Sourate: ANNISAI 

Verset : 83

وَإِذَا جَآءَهُمۡ أَمۡرٞ مِّنَ ٱلۡأَمۡنِ أَوِ ٱلۡخَوۡفِ أَذَاعُواْ بِهِۦۖ وَلَوۡ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنۡهُمۡ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسۡتَنۢبِطُونَهُۥ مِنۡهُمۡۗ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَٱتَّبَعۡتُمُ ٱلشَّيۡطَٰنَ إِلَّا قَلِيلٗا

Na linapowafikia jambo lolote la amani au hofu wanalitangaza. Na lau kama wangelirejesha kwa Mtume na kwa wenye mamlaka miongoni mwao, wangelijua wale walio na uwezo wa kulichambua.[1] Na lau kama sio fadhila za Allah kwenu na rehema zake, mngemfuata shetani ispokuwa wachache sana


1- - Kurani hapa inawakemea wale wenye tabia ya kusambaza habari nyeti zinazoweza kuteteresha amani au `kuleta hofu na taharuki katika jamii. Habari inapohusu amani na utulivu inapaswa kuachiwa wenye mamlaka. Katika Aya hapa ametajwa Mtume kwa sababu yeye alikuwa Mkuu wa Dola. Wenye mamlaka ni wale ambao wamekasimiwa mamlaka na Dola. Aya imeeleza kuwa hawa ndio wenye uwezo na nyenzo za kuchunguza, kutafiti na kupata undani wa habari na usahihi wake au kinyume chake. Pia hawa ndio wenye mamlaka na dhamana ya kulinda amani, utulivu na ustawi wa jamii.


Sourate: ANNISAI 

Verset : 96

دَرَجَٰتٖ مِّنۡهُ وَمَغۡفِرَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا

Ni daraja nyingi kutoka kwake na msamaha na rehema. Na Allah amekuwa Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Sourate: ANNISAI 

Verset : 113

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا

Na lau kama si hisani ya Allah na rehema zake kwako basi kwa yakini kabisa kundi miongoni mwao lilikusudia kukupotosha. Na hawapotoshi ispokuwa nafsi zao tu na hawatakudhuru chochote. Na Allah amekuteremshia kitabu (Qur’an) na hekima, na amekufundisha uliyokuwa huyajui. Na hisani ya Allah kwako ni kubwa sana



Sourate: ANNISAI 

Verset : 175

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱعۡتَصَمُواْ بِهِۦ فَسَيُدۡخِلُهُمۡ فِي رَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَفَضۡلٖ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَيۡهِ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Basi ambao wamemuamini Allah na wakashikamana naye basi atawaingiza katika rehema na fadhila zake na atawaongoza njia iliyonyooka kuelekea kwake (njia ambayo ni Uislamu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 12

قُل لِّمَن مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُل لِّلَّهِۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allah. Amejithibitishia rehema. Kwa yakini kabisa, atakukusanyeni Siku ya Kiama isiyokuwa na shaka. Waliozitia hasara nafsi zao, hawaamini



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 54

وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِنَا فَقُلۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۖ كَتَبَ رَبُّكُمۡ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَ أَنَّهُۥ مَنۡ عَمِلَ مِنكُمۡ سُوٓءَۢا بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na watakapokujia wale wanao-ziamini Aya zetu sema (uwaambie): Amani iwe kwenu. Mola wenu mwenyewe rehema amejithibitishia kwamba, yeyote miongoni mwenu atakayefanya jambo ovu kwa kutojua, kisha baada yake akatubu na kurekebisha (tabia yake) basi hakika yeye (Allah) ni Msamehevu sana, Mwenye kurehemu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 133

وَرَبُّكَ ٱلۡغَنِيُّ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفۡ مِنۢ بَعۡدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوۡمٍ ءَاخَرِينَ

Na Mola wako Mlezi ni Mkwasi, Mwenye rehema. Akitaka atakuondoeni na kuwaweka wengine awatakao kuwa badala yenu baada yenu kama vile alivyokuumbeni nyinyi kutoka katika kizazi cha watu wengine



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 147

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمۡ ذُو رَحۡمَةٖ وَٰسِعَةٖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُهُۥ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Basi wakikupinga waambie: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema yenye kuenea, na adhabu yake kwa watu waovu haizuiliki



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 56

وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَا وَٱدۡعُوهُ خَوۡفٗا وَطَمَعًاۚ إِنَّ رَحۡمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ مِّنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na msifanye uharibifu katika ardhi baada ya (ya Allah) kutengeneza na muombeni yeye (tu) kwa kuogopa (adhabu yake) na kutumai (rehema zake). Hakika, rehema za Allah zipo karibu na wenye kufanya mazuri



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 156

۞وَٱكۡتُبۡ لَنَا فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِنَّا هُدۡنَآ إِلَيۡكَۚ قَالَ عَذَابِيٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنۡ أَشَآءُۖ وَرَحۡمَتِي وَسِعَتۡ كُلَّ شَيۡءٖۚ فَسَأَكۡتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ

Na tuandikie mazuri katika hii dunia na akhera (pia tuandikie mazuri). Hakika, sisi tumerejea kwako. (Allah) Akasema: Adhabu yangu ninamlenga nimtakaye, na rehema yangu imekienea kila kitu. Basi nitaiandika (hiyo rehema yangu) kwa ambao wanamcha Allah na wanaotoa Zaka na (kwa) wale ambao Aya zetu wanaziamini



Sourate: ATTAUBA 

Verset : 61

وَمِنۡهُمُ ٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱلنَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٞۚ قُلۡ أُذُنُ خَيۡرٖ لَّكُمۡ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَيُؤۡمِنُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ رَسُولَ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na miongoni mwao (hao wanafiki) wapo wanaomuudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu (anamsikiliza kila mtu na kumsadiki). Sema: Yeye ni sikio la heri kwenu (anasikiliza heri tu si shari); anamuamini Allah, na ana imani na Waumini (wanaompa habari), na (yeye) ni rehema kwa wale wanaoamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Mtume wa Allah (kwa maneno na vitendo) watapata adhabu iumizayo mno



Sourate: ATTAUBA 

Verset : 99

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na katika Mabedui wapo wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wanachukulia (wanaamini) kuwa wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni ibada zinazowasogeza kwa Allah na maombi ya Mtume. Zindukeni na mjue kwamba, hizo ni (ibada) zinazowasogeza (kwa Allah) kwa faida yao. Allah atawaingiza katika rehema zake. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu



Sourate: YUNUS 

Verset : 58

قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Sema: Fadhila za Allah na rehema zake, basi wafurahie hayo. Hilo ni bora zaidi kwao kuliko wanavyovikusanya



Sourate: HUUD 

Verset : 9

وَلَئِنۡ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ ثُمَّ نَزَعۡنَٰهَا مِنۡهُ إِنَّهُۥ لَيَـُٔوسٞ كَفُورٞ

Na kama mwanadamu tutam-uonjesha kutoka kwetu rehema yoyote kisha tukaiondoa kwake rehema hiyo, kwa hakika yeye hukata tamaa akakufuru



Sourate: YUSUF 

Verset : 56

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kama hivyo tulimmakinisha Yusuf (na kumpa cheo katika nchi); akawa anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, na hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 56

قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ

(Ibrahimu) Alisema: Na hakuna anayekata tamaa na rehema za Mola wake Mlezi isipokuwa wale (watu) waliopotea?



Sourate: AL-KAHF 

Verset : 16

وَإِذِ ٱعۡتَزَلۡتُمُوهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأۡوُۥٓاْ إِلَى ٱلۡكَهۡفِ يَنشُرۡ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّن رَّحۡمَتِهِۦ وَيُهَيِّئۡ لَكُم مِّنۡ أَمۡرِكُم مِّرۡفَقٗا

Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Allah, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu



Sourate: AL-KAHF 

Verset : 58

وَرَبُّكَ ٱلۡغَفُورُ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۖ لَوۡ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُواْ لَعَجَّلَ لَهُمُ ٱلۡعَذَابَۚ بَل لَّهُم مَّوۡعِدٞ لَّن يَجِدُواْ مِن دُونِهِۦ مَوۡئِلٗا

Na Mola wako Mlezi ni Msa-mehevu Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu waliyo yachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo



Sourate: MARYAM 

Verset : 50

وَوَهَبۡنَا لَهُم مِّن رَّحۡمَتِنَا وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ لِسَانَ صِدۡقٍ عَلِيّٗا

Na tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu



Sourate: MARYAM 

Verset : 53

وَوَهَبۡنَا لَهُۥ مِن رَّحۡمَتِنَآ أَخَاهُ هَٰرُونَ نَبِيّٗا

Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii



Sourate: ANNUUR 

Verset : 10

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ حَكِيمٌ

Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake, na ya kuwa Allah ni Mpokeaji toba



Sourate: ANNUUR 

Verset : 14

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ لَمَسَّكُمۡ فِي مَآ أَفَضۡتُمۡ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeli kupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyo jiingiza



Sourate: ANNUUR 

Verset : 20

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake, na kwa hakika Allah ni Mpole, Mwenye kurehemu



Sourate: ANNUUR 

Verset : 21

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ وَمَن يَتَّبِعۡ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَإِنَّهُۥ يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۚ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ أَبَدٗا وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يُزَكِّي مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shetani. Na atakaye fuata nyayo za Shetani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila za Allah na rehema zake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Allah humtakasa amtakaye, na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua