وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلٗا
Na litaje jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni
Partager :
وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَٱسۡجُدۡ لَهُۥ وَسَبِّحۡهُ لَيۡلٗا طَوِيلًا
Na usiku msujudie Yeye, na umtakase, (usali kwaajili yake) usiku, wakati mrefu
وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلۡقَيِّمَةِ
Nao hawakuamrishwa kitu isipokuwa wamuabudu Allah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti
فَلۡيَعۡبُدُواْ رَبَّ هَٰذَا ٱلۡبَيۡتِ
Kwasababu ya hayo, wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii (Tukufu ya Makka)
ٱلَّذِيٓ أَطۡعَمَهُم مِّن جُوعٖ وَءَامَنَهُم مِّنۡ خَوۡفِۭ
Ambaye amewalisha wasipate njaa, na amewasalimisha wasipate hofu
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ
Sema: Enyi makafiri
لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ
Siabudu mnacho kiabudu
وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
Na nyinyi hamuabudu ninaye muabudu
وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ
Na mimi si mwenye kuviabudu mlivyo viabudu
Na nyinyi si wenye kuabudu ninayemuabudu
لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ
Nyinyi mna dini yenu, nami nina dini yangu