Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 122

إِذۡ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمۡ أَن تَفۡشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَاۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Wakati Makundi mawili kati yenu yalipoingiwa na hofu ya kushindwa, na ilhali Allah ndiye Mlinzi wao. Na Waumini (wanatakiwa) wamtegemee Allah tu



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 159

فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 160

إِن يَنصُرۡكُمُ ٱللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمۡۖ وَإِن يَخۡذُلۡكُمۡ فَمَن ذَا ٱلَّذِي يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Iwapo Allah atawanusuru, basi hakuna wa kuwashinda na endapo atakuacheni basi ni nani mwingine baada ya Yeye atakunusuruni? Na Waumini wategemee kwa Allah tu



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 173

ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدۡ جَمَعُواْ لَكُمۡ فَٱخۡشَوۡهُمۡ فَزَادَهُمۡ إِيمَٰنٗا وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ وَنِعۡمَ ٱلۡوَكِيلُ

Ambao watu waliwaambia wao: hakika kundi la watu limekukusanyikieni basi waogopeni, hilo likawazidishia imani na wakasema: Allah anatutosha na ndiye mbora wa wenye kutegemewa



Sourate: ANNISAI 

Verset : 81

وَيَقُولُونَ طَاعَةٞ فَإِذَا بَرَزُواْ مِنۡ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ غَيۡرَ ٱلَّذِي تَقُولُۖ وَٱللَّهُ يَكۡتُبُ مَا يُبَيِّتُونَۖ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا

Na wanasema: Tumetii. Lakini wakiondoka kwako kundi miongoni mwao linapanga njama usiku tofauti na yale unayosema, na Allah anayaandika wanayo yapanga usiku. Basi wapuuze, na mtegemee Allah, na inatosha kwamba Allah ni Mwenye kutegemewa



Sourate: AL-MAIDA 

Verset : 11

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ هَمَّ قَوۡمٌ أَن يَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ فَكَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Enyi mlioamini, kumbukeni neema ya Allah kwenu pale watu (Makureish na Wayahudi) walipodhamiria kukunyoosheeni mikono yao (na kutaka kumuua Mtume na Swahaba) (Allah) akaizuia mikono yao isikufikieni. Na mcheni Allah. Na Allah tu wamtegemee waumini



Sourate: AL-MAIDA 

Verset : 23

قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡهِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَٰلِبُونَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Watu wawili miongoni mwa wale waogopao (kuhalifu amri za Allah na Mtume wake) ambao Allah amewaneemesha walisema: Wavamieni kupitia kwenye huo mlango; maana mtakapowavamia (kupitia hapo mlangoni), kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Allah tu ikiwa nyinyi ni waumini



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 89

قَدِ ٱفۡتَرَيۡنَا عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا إِنۡ عُدۡنَا فِي مِلَّتِكُم بَعۡدَ إِذۡ نَجَّىٰنَا ٱللَّهُ مِنۡهَاۚ وَمَا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّعُودَ فِيهَآ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّنَاۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَاۚ رَبَّنَا ٱفۡتَحۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ قَوۡمِنَا بِٱلۡحَقِّ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰتِحِينَ

Hakika, tutakuwa tumemzulia Allah uwongo kama tutarudi kwenye mila (dini) yenu baada ya kuwa Allah ametuokoa. Na haiwezekani kwetu kurudi kwenye mila hiyo isipokuwa tu atake Allah Mola wetu Mlezi. Mola wetu anakijua vilivyo kila kitu. Tunamtegemea Allah tu. Ewe Mola wetu Mlezi, tupe ukombozi baina yetu na baina ya watu zetu na, kwa haki, wewe ni bora wa wakombozi



Sourate: AN-FAL 

Verset : 2

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Kwa hakika kabisa, Waumini (kamili) ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya zake huwaongezea imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi tu



Sourate: AN-FAL 

Verset : 49

إِذۡ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَـٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمۡۗ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

(Kumbuka) Wakati wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao (watu wapya katika Uislamu) wanasema (kuwa): Hawa (Waislamu) dini yao imewadanganya (kwamba watashinda pamoja na uchache wao). Na Mwenye kumtegemea Allah, basi hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Sourate: AN-FAL 

Verset : 61

۞وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلۡمِ فَٱجۡنَحۡ لَهَا وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na (makafiri) wakielekea kutaka amani (na suluhu), basi na wewe elekea kwenye amani (na suluhu) hiyo na mtegemee Allah. Hakika, yeye (Allah) ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua



Sourate: ATTAUBA 

Verset : 51

قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Sema: Katu halitusibu ila tu alilotuandikia Allah. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na waumini (wa kweli) wamtegemee Allah tu



Sourate: ATTAUBA 

Verset : 129

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ

Basi (wanafiki na washirikishaji) wakikengeuka (wakipinga), wewe sema: Allah ananitosheleza. Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Nimetegemea yeye tu, na Yeye tu ndiye Mola wa Arshi Tukufu



Sourate: YUNUS 

Verset : 71

۞وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Na wasomee habari za (Mtume) Nuhu wakati alipowaambia watu wake kuwa: “Enyi watu wangu, ikiwa mnachukizwa na kuishi kwangu (na nyinyi) na kukumbusha kwangu Aya za Allah, basi mimi nimemtegemea Allah tu. Basi amueni jambo lenu nyinyi na washirika (Miungu) wenu, kisha jambo lenu lisiwe la kificho, kisha pitisheni hukumu kwangu na msinicheleweshe



Sourate: YUNUS 

Verset : 84

وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰقَوۡمِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ فَعَلَيۡهِ تَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّسۡلِمِينَ

Na Musa alisema: Enyi watu wangu, kama kweli nyinyi mmemuamini Allah, basi mtegemeeni yeye tu, kama nyinyi mkiwa Waislamu (kweli)



Sourate: YUNUS 

Verset : 85

فَقَالُواْ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَا رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Basi wakasema: “Allah tu tunamtegemea. Ewe Mola wetu Mlezi, usitufanye mtihani kwa watu madhalimu”



Sourate: HUUD 

Verset : 56

إِنِّي تَوَكَّلۡتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّي وَرَبِّكُمۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذُۢ بِنَاصِيَتِهَآۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Hakika mimi nimemtegemea Allah, Mola wangu mlezi na Mola wenu mlezi. Hakuna mnyama (kiumbe) yeyote ispokuwa yeye (Allah) amezishika nywele zake za utosi. Bila shaka Mola wangu mlezi yupo katika njia iliyonyooka



Sourate: HUUD 

Verset : 88

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ

Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje kama nitakuwa na dalili kutoka kwa Mola wangu mlezi, na ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Na sipendi niwe kinyume na nyinyi nikafanya yale ninayowakatazeni. Sitaki ispokuwa kutengeneza kiasi niwezavyo. Na hakuna taufiki ispokuwa kwa Allah tu. Kwake tu nimetegemea na kwake tu nimerejea



Sourate: HUUD 

Verset : 123

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُ ٱلۡأَمۡرُ كُلُّهُۥ فَٱعۡبُدۡهُ وَتَوَكَّلۡ عَلَيۡهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na ni vya Allah tu vyote vilivyo fichikana mbinguni na ardhini, na mambo yote yatarudishwa kwake tu. Basi muabudu yeye na umtegemee yeye. Na Mola wako mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda



Sourate: YUSUF 

Verset : 67

وَقَالَ يَٰبَنِيَّ لَا تَدۡخُلُواْ مِنۢ بَابٖ وَٰحِدٖ وَٱدۡخُلُواْ مِنۡ أَبۡوَٰبٖ مُّتَفَرِّقَةٖۖ وَمَآ أُغۡنِي عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍۖ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَعَلَيۡهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

Na alisema: Enyi wanangu, msiingie (Misri) kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango mbali mbali. Na mimi sikufaeni kitu chochote mbele ya Allah. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allah tu, yeye tu nimemtegemea na yeye tu wamtegemee wenye kutegemea



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 30

كَذَٰلِكَ أَرۡسَلۡنَٰكَ فِيٓ أُمَّةٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهَآ أُمَمٞ لِّتَتۡلُوَاْ عَلَيۡهِمُ ٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَهُمۡ يَكۡفُرُونَ بِٱلرَّحۡمَٰنِۚ قُلۡ هُوَ رَبِّي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ مَتَابِ

(Kama tulivyowatuma Mitume waliotangulia) kama hivyo tulikutuma kwa umma ambao ulikwishapita kabla yao nyumati nyingine, ili uwasomee tunayokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani, Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Kwake tu nimetegemea, na kwake tu ndio marejeo



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 11

قَالَتۡ لَهُمۡ رُسُلُهُمۡ إِن نَّحۡنُ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَمَا كَانَ لَنَآ أَن نَّأۡتِيَكُم بِسُلۡطَٰنٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Mitume wao waliwaambia: Sisi kweli si chochote (kimaumbo) ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Allah humfanyia hisani amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuleta uthibitisho ila kwa idhini ya Allah. Na kwa Allah tu ndio wategemee Waumini



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 12

وَمَا لَنَآ أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنَا سُبُلَنَاۚ وَلَنَصۡبِرَنَّ عَلَىٰ مَآ ءَاذَيۡتُمُونَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

Na wala hatuna udhuru (wa kwa) nini tusimtegemee Allah, na hali Yeye ametuongoa kwenye Njia zetu. Na hapana shaka sisi tutavumilia hizo kero mlizotuudhi kwazo. Na kwa Allah tu wategemee wanaotegemea



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 42

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

(Hao ni) wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao mlezi



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 99

إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hakika yeye hana nguvu juu ya wale walioamini na kwa Mola wao mlezi tu wanategemea



Sourate: ALFURQAAN 

Verset : 58

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡحَيِّ ٱلَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِهِۦۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا

Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kwake kuwa yeye ni Mwenye khabari za dhambi za waja wake



Sourate: ASH-SHUARAA 

Verset : 217

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu



Sourate: ASH-SHUARAA 

Verset : 218

ٱلَّذِي يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ

Ambaye anakuona unapo simama,



Sourate: ASH-SHUARAA 

Verset : 219

وَتَقَلُّبَكَ فِي ٱلسَّـٰجِدِينَ

Na mageuko yako kati ya wanao sujudu



Sourate: ASH-SHUARAA 

Verset : 220

إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua