Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 121

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَتۡلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Wale ambao tumewapa kitabu (wakawa) wanakisoma ipasavyo, basi hao ndio wanaokiamini, na wale watakaokipinga basi hao ndio wenye kupata hasara



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 7

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu. Baadhi ya Aya zake zinafahamika kwa wepesi (na) ambazo ndio msingi wa kitabu (hiki cha Kurani). Na (Aya) nyingine zinatatiza. Ama wale ambao ndani ya nyoyo zao kuna upotevu, wanafuata (Aya) zinazotatiza, kwa kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Na hakuna anayejua tafsiri yake (halisi) isipokuwa Allah tu. Na wale waliobobea katika elimu husema: Tumeziamini (Aya) zote. Zote (hizo) zinatoka kwa Mola wetu Mlezi. Na hawawaidhiki isipokuwa wenye akili tu



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 8

رَبَّنَا لَا تُزِغۡ قُلُوبَنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَيۡتَنَا وَهَبۡ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةًۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡوَهَّابُ

Ewe Mola wetu, usiziache nyoyo zetu zipotee baada ya kuwa umetuongoza, na tunaomba rehema kwako. Hakika, wewe ni Mtoaji sana



Sourate: AL-IMRAN 

Verset : 199

وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Na kwa hakika katika Watu wa kitabu wapo wanaomuamini Allah hasa na kilichoteremshwa kwenu na kilichoteremshwa kwao, huku wakinyenyekea kwa Allah. Hawauzi Aya za Allah kwa thamani ndogo (ya dunia). Hao malipo yao yako kwa Mola wao mlezi, hakika Allah ni mwepesi mno wa kuhesabu



Sourate: AL-MAIDA 

Verset : 83

وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ

Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanabubujika machozi kwasababu ya haki waliyoitambua. Wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi, tumeamini; basi tuandike (tuwe) pamoja na wanaoshuhudia (Uungu wako, upekee wako na kuabudiwa kwako)



Sourate: AL-MAIDA 

Verset : 84

وَمَا لَنَا لَا نُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡحَقِّ وَنَطۡمَعُ أَن يُدۡخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na kwanini tusimuamini Allah na haki iliyotujia (Qur’an) Na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 30

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ قَالَ أَلَيۡسَ هَٰذَا بِٱلۡحَقِّۚ قَالُواْ بَلَىٰ وَرَبِّنَاۚ قَالَ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Na lau kama utawaona wakati watakaposimamishwa kwa Mola wao atasema Allah na kuwaambia): Hivi hili (la kufufuliwa) sio kweli? Watasema: Tunaapa kwa Mola wetu (kwamba ni kweli). (Allah) Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayapinga



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 114

أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡتَغِي حَكَمٗا وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مُفَصَّلٗاۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٞ مِّن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Hivi nitake hakimu (muamuzi) asiyekuwa Allah, na ilhali yeye ndiye aliyekuteremshieni kitabu kikiwa kimefafanuliwa? Na wale tuliowapa kitabu wanajua kwamba kimetereshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Kwa hiyo usiwe miongoni mwa wenye shaka kabisa



Sourate: AN-FAL 

Verset : 2

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Kwa hakika kabisa, Waumini (kamili) ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya zake huwaongezea imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi tu



Sourate: ATTAUBA 

Verset : 124

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wanaosema (kwa kebehi): Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Basi ama wale walioamini imewazidishia Imani, nao wanafurahia



Sourate: HUUD 

Verset : 17

أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتۡلُوهُ شَاهِدٞ مِّنۡهُ وَمِن قَبۡلِهِۦ كِتَٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامٗا وَرَحۡمَةًۚ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ مِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ فَٱلنَّارُ مَوۡعِدُهُۥۚ فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّنۡهُۚ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hivi yule aliye na hoja kutoka kwa Mola wake mlezi na akaifuata (hoja hiyo) shahidi kutoka kwake (Jibrili) na kabla yake palikuwepo kitabu (cha taurati kilichoteremshwa kwa Nabii) Musa juu yake amani, kikiwa ni kiongozi na rehema, hao wanaiamini Qur ani, na yeyote anaeikufuru miongoni mwa makundi, basi Moto ni mahali pake alipoahidiwa, basi usiwe katika shaka yoyote, hii Qur’ani ni haki kutoka kwa bwana wako, lakini watu wengi hawaamini



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 36

وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَۖ وَمِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ مَن يُنكِرُ بَعۡضَهُۥۚ قُلۡ إِنَّمَآ أُمِرۡتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشۡرِكَ بِهِۦٓۚ إِلَيۡهِ أَدۡعُواْ وَإِلَيۡهِ مَـَٔابِ

Na wale tuliowapa Kitabu wanafurahia yale uliyoteremshiwa[1]. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake[2]. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Allah, na wala nisimshirikishe. Kuelekea kwake Yeye tu ndiyo ninaita (watu), na kwake Yeye tu ndio marejeo yangu


1- - Wanaolengwa kuifurahikia Qura’n hapa ni wale wa Yahudi waliosilimu katika enzi za Mtume akiwemo
Abdallah bin Salam na wenzake.

2- - Na wapo baadhi ya Wayahudi kama vile Ka’b bin Al-ashraf na wenzake walikuwa wanayapinga wazi wazi
baadhi ya yale yaliyoteremshwa kwa Mtume.


Sourate: AL-ISRAA 

Verset : 107

قُلۡ ءَامِنُواْ بِهِۦٓ أَوۡ لَا تُؤۡمِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهِۦٓ إِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ يَخِرُّونَۤ لِلۡأَذۡقَانِۤ سُجَّدٗاۤ

Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika wale walio pewa ilimu kabla yake, wanapo somewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu



Sourate: MARYAM 

Verset : 58

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِن ذُرِّيَّةِ ءَادَمَ وَمِمَّنۡ حَمَلۡنَا مَعَ نُوحٖ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡرَـٰٓءِيلَ وَمِمَّنۡ هَدَيۡنَا وَٱجۡتَبَيۡنَآۚ إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُ ٱلرَّحۡمَٰنِ خَرُّواْۤ سُجَّدٗاۤ وَبُكِيّٗا۩

Hao ndio alio waneemesha Allah miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia



Sourate: AL-HAJJ 

Verset : 54

وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤۡمِنُواْ بِهِۦ فَتُخۡبِتَ لَهُۥ قُلُوبُهُمۡۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na ili walio pewa elimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Allah ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia Iliyo Nyooka



Sourate: ALFURQAAN 

Verset : 73

وَٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَمۡ يَخِرُّواْ عَلَيۡهَا صُمّٗا وَعُمۡيَانٗا

Na ambao wanapokumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi na vipofu



Sourate: AL-QASWAS 

Verset : 52

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِهِۦ هُم بِهِۦ يُؤۡمِنُونَ

Wale tuliowapa Kitabu kabla yake wanakiamini hiki



Sourate: AL-QASWAS 

Verset : 53

وَإِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلِهِۦ مُسۡلِمِينَ

Na wanaposomewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayotoka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulio nyenyekea



Sourate: AL-ANKABUUT 

Verset : 47

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَۚ فَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَمِنۡ هَـٰٓؤُلَآءِ مَن يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا ٱلۡكَٰفِرُونَ

Na namna hivi tumekuteremshia Kitabu (cha Qur’ani). Basi wale tulio wapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur’ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakaoiamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipo-kuwa makafiri



Sourate: ARRUUM 

Verset : 53

وَمَآ أَنتَ بِهَٰدِ ٱلۡعُمۡيِ عَن ضَلَٰلَتِهِمۡۖ إِن تُسۡمِعُ إِلَّا مَن يُؤۡمِنُ بِـَٔايَٰتِنَا فَهُم مُّسۡلِمُونَ

Wala wewe huwaongoi vipofu na upotovu wao. Huwasikilizishi ila wanao ziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walio nyenyekea



Sourate: ASSAJDAH 

Verset : 15

إِنَّمَا يُؤۡمِنُ بِـَٔايَٰتِنَا ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُواْ بِهَا خَرُّواْۤ سُجَّدٗاۤ وَسَبَّحُواْ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ۩

Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni



Sourate: SABAA 

Verset : 6

وَيَرَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ ٱلۡحَقَّ وَيَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Na waliopewa elimu wanaona yakuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni haki, nayo huongoa kuendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa