Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 142

۞سَيَقُولُ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَ ٱلنَّاسِ مَا وَلَّىٰهُمۡ عَن قِبۡلَتِهِمُ ٱلَّتِي كَانُواْ عَلَيۡهَاۚ قُل لِّلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Punde watasema baadhi ya watu wapumbavu: Ni nini kilichowageuza kutoka kwenye Kibla chao ambacho walikuwa wanakielekea? Sema: Mashariki na magharibi ni miliki ya Allah. Anamuelekeza amtakaye kwenye njia iliyonyooka



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 143

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَٰكُمۡ أُمَّةٗ وَسَطٗا لِّتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيۡكُمۡ شَهِيدٗاۗ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلۡقِبۡلَةَ ٱلَّتِي كُنتَ عَلَيۡهَآ إِلَّا لِنَعۡلَمَ مَن يَتَّبِعُ ٱلرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِۚ وَإِن كَانَتۡ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَٰنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Na kama hivyo tumekufanyeni umma bora ili muwe mashahidi kwa watu, na Mtume awe shahidi kwenu. Na hatukukiweka Kibla ulichokuwa unaelekea isipokuwa tu tumjue nani anamfuata Mtume na nani atakayerejea nyuma. Ilivyo ni kwamba hilo ni zito sana isipokuwa kwa wale ambao Allah amewaongoza. Na Allah hapotezi imani zenu. Kwa hakika kabisa Allah ni Mpole mno kwa watu, Mwenye huruma sana



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 144

قَدۡ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجۡهِكَ فِي ٱلسَّمَآءِۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبۡلَةٗ تَرۡضَىٰهَاۚ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ لَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ

Tunaona ukigeuzageuza uso wako mbinguni. Hakika tunakuelekeza Kibla unachokiridhia, Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu[1]. Na popote muwapo elekezeni nyuso zenu upande huo. Na hakika wale ambao wamepewa kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Mola wao. Na Allah hakuwa mwenye kughafilika na wanayotenda


1- - Msikiti Mtukufu wa Makka


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 145

وَلَئِنۡ أَتَيۡتَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ بِكُلِّ ءَايَةٖ مَّا تَبِعُواْ قِبۡلَتَكَۚ وَمَآ أَنتَ بِتَابِعٖ قِبۡلَتَهُمۡۚ وَمَا بَعۡضُهُم بِتَابِعٖ قِبۡلَةَ بَعۡضٖۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ إِنَّكَ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na kwa yakini kabisa kama ungewaletea kila aina ya hoja wale waliopewa kitabu, wasingefuata Kibla chako. Na wewe hutafuata Kibla chao. Na hata wao kwa wao hakuna mwenye kufuata Kibla cha mwingine. Na kama utafuata utashi wa nafsi zao baada ya kukufikia elimu, kwa yakini kabisa utakuwa miongoni mwa Madhalimu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 146

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Na wale tuliowapa kitabu wanayajua hayo[1], kama wana-vyowajua watoto wao. Lakini kundi katika wao wanaificha haki ilhali wanajua


1- - Ya kuwa Muhammad ni Mtume wa kweli na Kaaba ndio kibla sahihi cha Waislamu


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 147

ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Ni haki kutoka kwa Mola wako, basi usiwe miongoni mwa walio na shaka kabisa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 148

وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na kila umma una upande unaoelekea. Kwa hiyo, shindaneni kufanya kheri. Popote mtakapokuwa, Allah atakuleteni nyote. Hakika, Allah nimuweza wa kila kitu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 149

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na popote utokapo enda elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu. Na kwa hakika kabisa, hiyo ni haki kutoka kwa Mola wako. Na Allah hakuwa mwenye kughafilika na mnayoyatenda



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 150

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na popote utokapoenda elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu. Na popote muwapo, elekezeni nyuso zenu upande huo, ili watu wasipate hoja dhidi yenu, isipokuwa madhalimu miongoni mwao. Kwa hiyo, hao msiwaogope, na niogopeni Mimi tu, na ili nitimize neema zangu kwenu, na ili mpate kuongoka



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 29

قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ

Sema: Mola wangu Mlezi ameamrisha (kufanya) uadilifu. Na elekezeni nyuso zenu kila mnaposwali (mkusudieni Allah kila mfanyapo ibada) na muabuduni yeye tu mkimtakasia dini. Kama (Allah) ambavyo amekuumbeni mwanzo ndivyo mtakavyorudi



Sourate: YUNUS 

Verset : 87

وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّءَا لِقَوۡمِكُمَا بِمِصۡرَ بُيُوتٗا وَٱجۡعَلُواْ بُيُوتَكُمۡ قِبۡلَةٗ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na tulimpa Wahyi Musa na ndugu yake (Haruna) ya kuwa: Wawekeeni makazi (wajengeeni nyumba) watu wenu (katika mji wa) Misri na zifanyeni nyumba zenu ziwe na mahala pa ibada na simamisheni Swala na wape bishara Waumini