۞إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا
Hakika, sisi tumekufunulia (Wahyi) kama tulivyomfunulia (Wahyi) Nuhu na Manabii (wengine) baada yake. Na tumemfunulia (Wahyi) Ibrahimu na Ismail na Isihaka na Yakubu na kizazi (chake) na Issa na Ayubu na Yunus na Haruna na Sulaimani. Na tulimpa Daudi Zaburi
وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ كُلًّا هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَٰرُونَۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na tulimtunuku (Mtume Ibrahimu) Isihaka na Yakubu. Wote tuliwaongoa. Na Nuhu tulimuongoa kabla (yao). Na katika kizazi chake tulimongoa Daudi na Suleimani na Ayubu na Yusufu na Mussa na Haruna. Na kama hivyo tunawalipa wafanyao mazuri
۞وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Na tuliahidiana na Musa usiku (siku) thalathini na tukatimiza kwa (kuongeza) siku kumi. Basi ikatimia ahadi ya Mola wake siku arubaini. Na Musa alimwambia ndugu yake Haruna kwamba: Kuwa mrithi wangu kwa watu wangu na tengeneza (mambo yaliyoharibika) na usifuate njia ya waharibifu
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na Musa aliporudi kwa watu wake akiwa amekasirika na kuhuzunika alisema: Ubaya ulioje wa mliyoyafanya baada kuondoka kwangu! Hivi mmeharakia amri ya Mola wenu Mlezi? Na alizitupa mbao (za Taurati) na akakamata kichwa cha ndugu yake (Haruna) akimvutia kwake na kumwambia: Ewe mtoto wa mama yangu, hakika hawa watu wamenidharau na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui kupitia kwangu na usiniweke pamoja na watu madhalimu
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ
Kisha tukamtuma Musa na Haruna baada ya hao kwenda kwa Firauni na mamwinyi wake (wakiwa na) Aya zetu. Basi wakafanya kiburi na wakawa watu wakosefu
وَوَهَبۡنَا لَهُۥ مِن رَّحۡمَتِنَآ أَخَاهُ هَٰرُونَ نَبِيّٗا
Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii
وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي
Na nipe waziri katika watu wangu,
هَٰرُونَ أَخِي
Harun, ndugu yangu
ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي
Kwake yeye niongeze nguvu zangu
وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي
Na umshirikishe katika kazi yangu
كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا
Ili tukutakase sana
وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا
Na tukukumbuke sana
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا
Hakika Wewe unatuona
قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ
Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Mussa!
وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي
Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na tiini amri yangu!
قَالُواْ لَن نَّبۡرَحَ عَلَيۡهِ عَٰكِفِينَ حَتَّىٰ يَرۡجِعَ إِلَيۡنَا مُوسَىٰ
Wakasema: Hatutaacha kumua-budu mpaka Mussa atapo rejea kwetu
قَالَ يَٰهَٰرُونُ مَا مَنَعَكَ إِذۡ رَأَيۡتَهُمۡ ضَلُّوٓاْ
(Mussa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho kuzuia, ulipo waona wamepotea,
أَلَّا تَتَّبِعَنِۖ أَفَعَصَيۡتَ أَمۡرِي
Hata usinifuate? Je, umeasi amri yangu?
قَالَ يَبۡنَؤُمَّ لَا تَأۡخُذۡ بِلِحۡيَتِي وَلَا بِرَأۡسِيٓۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقۡتَ بَيۡنَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَلَمۡ تَرۡقُبۡ قَوۡلِي
Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ٱلۡفُرۡقَانَ وَضِيَآءٗ وَذِكۡرٗا لِّلۡمُتَّقِينَ
Na kwa yakini tuliwapa Mussa na Haarun kipambanuzi, na mwangaza, na ukumbusho kwa wacha Mungu
ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَٰرُونَ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ
Kisha tukamtuma Mussa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi
إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمًا عَالِينَ
Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri
فَقَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لِبَشَرَيۡنِ مِثۡلِنَا وَقَوۡمُهُمَا لَنَا عَٰبِدُونَ
Wakasema: Je, tuwaamini wawili hawa wanaadamu kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu?
فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡلَكِينَ
Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَٰرُونَ وَزِيرٗا
Na hakika tulimpa Mussa Kitabu na tukamweka pamoja naye nduguye, Harun, kuwa waziri
فَقُلۡنَا ٱذۡهَبَآ إِلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَدَمَّرۡنَٰهُمۡ تَدۡمِيرٗا
Tukawaambia: Nendeni kwa watu walio kanusha Ishara zetu. Basi tukawateketeza kabisa
وَأَخِي هَٰرُونُ هُوَ أَفۡصَحُ مِنِّي لِسَانٗا فَأَرۡسِلۡهُ مَعِيَ رِدۡءٗا يُصَدِّقُنِيٓۖ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ
Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume ende nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi nina khofu watanikadhibisha
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجۡعَلُ لَكُمَا سُلۡطَٰنٗا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيۡكُمَا بِـَٔايَٰتِنَآۚ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلۡغَٰلِبُونَ
(Allah) akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa nduguyo, na tutakupeni madaraka, hata wasikufikilieni. Kwa sababu ya Ishara zetu nyinyi na watakao kufuateni mtashinda
وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Mussa na Harun
سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Iwe salama kwa Mussa na Harun!