فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
Partager :
مُدۡهَآمَّتَانِ
Za rangi ya kijani iliyokoza
فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo
فِيهِمَا فَٰكِهَةٞ وَنَخۡلٞ وَرُمَّانٞ
Mna humo matunda na mitende na makomamanga
فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٞ
Mna humo wanawake wema wazuri
حُورٞ مَّقۡصُورَٰتٞ فِي ٱلۡخِيَامِ
weupe wakiwa na macho mapana waliotawishwa kwenye mahema
لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفۡرَفٍ خُضۡرٖ وَعَبۡقَرِيٍّ حِسَانٖ
Wakiegemea kwenye matakia ya kijani na mazulia ya rangi mbalimbali ya hariri mazuri mno yasiyo na kifani
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ
watakua juu ya vitanda vilivyofumwa vizuri
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
hali wakiwa wameviegemea huku wakitazamana
يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ
Watazungukiwa na vijana wenye kudumu
بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ
Kwa bilauri na mabirika na vikombe vya mvinyo kutoka kwenye chemchemu
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ
Hawatapata maumivu ya kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawa-tatokwa na akili
وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Na matunda watakayo pendelea wao
وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
Na nyama za ndege katika wata-kazozitamani
وَحُورٌ عِينٞ
Na wanawake wenye macho makubwa yaliyo meupe sana na weusi sana
كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ
Kama mfano wa lulu zilizohi-fadhiwa
جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Ikiwa ni malipo kwa ambayo walikuwa wanatenda (duniani)
لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا
Hawatasikia humo maneno ya upuuzi wala yanayopelekea kupata madhambi
إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا
Isipokuwa itasemwa: Salama, na Amani!
فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ
Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba
وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ
Na migomba iliyopangiliwa
وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ
Na kivuli kilichotandazwa