Sourate: ASSWAFF 

Verset : 10

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَٰرَةٖ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ

Enyi mlioamini! Nikujulisheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu (iumizayo)?



Sourate: ASSWAFF 

Verset : 11

تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Muaminini Allah na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Allah kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua



Sourate: ASSWAFF 

Verset : 12

يَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ وَيُدۡخِلۡكُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّـٰتِ عَدۡنٖۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa



Sourate: ASSWAFF 

Verset : 13

وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na kingine mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Allah, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!



Sourate: ASSWAFF 

Verset : 14

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُوٓاْ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوَارِيِّـۧنَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٞ مِّنۢ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٞۖ فَأَيَّدۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَىٰ عَدُوِّهِمۡ فَأَصۡبَحُواْ ظَٰهِرِينَ

Enyi walioamini! Kuweni wenye kuinusuru (Dini ya) Allah kama alivyosema ‘Isa mwana wa Maryam kwa wafuasi wake (watiifu): Na ni wanusuruji wangu kwa ajili ya Allah? Wafuasi wake wakasema: Sisi ni wenye kuinusuru (Dini ya) Allah, Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israail na likakufuru kundi jingine. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda



Sourate: ATTAHRIIM 

Verset : 9

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Ee Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni Motoni. Na ni mahali pabaya palioje pa kufikia



Sourate: AL-AADIYAAT 

Verset : 1

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا

Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,



Sourate: AL-AADIYAAT 

Verset : 2

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا

Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,



Sourate: AL-AADIYAAT 

Verset : 3

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا

Wakishambulia wakati wa asubuhi,



Sourate: AL-AADIYAAT 

Verset : 4

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا

Huku wakitimua vumbi,



Sourate: AL-AADIYAAT 

Verset : 5

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا

Na wakijitoma kati ya kundi,