Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 210

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِي ظُلَلٖ مِّنَ ٱلۡغَمَامِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Hakuna wanachongojea isipokuwa kuwajia Allah na Malaika kwenye vivuli vya mawingu na jambo lishakatiwa shauri. Na kwa Allah pekee ndipo yanaporudishwa mambo



Sourate: ALFURQAAN 

Verset : 25

وَيَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلسَّمَآءُ بِٱلۡغَمَٰمِ وَنُزِّلَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ تَنزِيلًا

Na siku zitapo funguka mbingu kwa mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi,



Sourate: AZZUMAR 

Verset : 67

وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعٗا قَبۡضَتُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُ مَطۡوِيَّـٰتُۢ بِيَمِينِهِۦۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na wala hawakumheshimu Allah kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa’la Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayo mshirikisha nayo



Sourate: ARRAHMAAN 

Verset : 37

فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ وَرۡدَةٗ كَٱلدِّهَانِ

Zitakapo pasuka mbingu zikawa nyekundu kama mafuta



Sourate: ARRAHMAAN 

Verset : 38

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?