وَإِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحۡنَ أَزۡوَٰجَهُنَّ إِذَا تَرَٰضَوۡاْ بَيۡنَهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ مِنكُمۡ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ ذَٰلِكُمۡ أَزۡكَىٰ لَكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
Na mnapowaacha wake na wakamaliza Eda zao, basi nyinyi mawalii msiwazuie kufunga ndoa na waume zao waliowaacha iwapo wataridhiana kwa wema. Anapewa onyo hilo yule anayemuamini Allah miongoni mwenu na Siku ya Mwisho. Hayo kwenu ni bora mno na nisafi kabisa. Na Allah anajua ilihali nyinyi hamjui
۞وَٱلۡوَٰلِدَٰتُ يُرۡضِعۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ حَوۡلَيۡنِ كَامِلَيۡنِۖ لِمَنۡ أَرَادَ أَن يُتِمَّ ٱلرَّضَاعَةَۚ وَعَلَى ٱلۡمَوۡلُودِ لَهُۥ رِزۡقُهُنَّ وَكِسۡوَتُهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ لَا تُكَلَّفُ نَفۡسٌ إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَا تُضَآرَّ وَٰلِدَةُۢ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوۡلُودٞ لَّهُۥ بِوَلَدِهِۦۚ وَعَلَى ٱلۡوَارِثِ مِثۡلُ ذَٰلِكَۗ فَإِنۡ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٖ مِّنۡهُمَا وَتَشَاوُرٖ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَاۗ وَإِنۡ أَرَدتُّمۡ أَن تَسۡتَرۡضِعُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا سَلَّمۡتُم مَّآ ءَاتَيۡتُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Na wazazi wanawake wan-yonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya baba chakula chao (mama na mtoto) na kivazi chao kwa wema. Nafsi haikalifishwi (kufanya jambo) isipokuwa lililo ndani ya uwezo wake tu. Mama asidhuriwe kwa sababu ya mwanawe, na baba asidhuriwe kwa sababu ya mwanawe. Na ni wajibu juu ya mrithi (wa mtoto kufanya hayo). Na si vibaya kwa wawili hao (baba na mama) wakitaka kumwachisha ziwa (mtoto chini ya miaka miwili) kwa kushauriana na kuridhiana. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha, basi hapana ubaya kwenu mkitoa kile mlichowapa kwa njia ya wema. Na mcheni Allah na jueni kwamba Allah ni mwenye kuyaona sana yote myatendayo
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرۡبَعَةَ أَشۡهُرٖ وَعَشۡرٗاۖ فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake, wangoje wao wenyewe miezi minne na siku kumi. Na watakapotimiza Eda zao, basi hapana ubaya kwenu katika waliyojifanyia kwa wema. Na Allah anayajua vilivyo myafanyayo
وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا عَرَّضۡتُم بِهِۦ مِنۡ خِطۡبَةِ ٱلنِّسَآءِ أَوۡ أَكۡنَنتُمۡ فِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ سَتَذۡكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّآ أَن تَقُولُواْ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗاۚ وَلَا تَعۡزِمُواْ عُقۡدَةَ ٱلنِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡكِتَٰبُ أَجَلَهُۥۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ
Na si vibaya kwenu posa za fumbo mlizowafumbia au mlicho-kificha kwenye nafsi zenu. Allah amejua kuwa nyinyi mtawakumbuka hao, Na lakini msiwaahidi (ndoa) kwa siri isipokuwa mseme maneno mema. Na msiazimie kufunga nao ndoa mpaka Eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Allah anajua yaliyomo katika nafsi zenu, basi jihadharini naye, najueni kwamba Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno
لَّا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ مَا لَمۡ تَمَسُّوهُنَّ أَوۡ تَفۡرِضُواْ لَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى ٱلۡمُوسِعِ قَدَرُهُۥ وَعَلَى ٱلۡمُقۡتِرِ قَدَرُهُۥ مَتَٰعَۢا بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakuna ubaya kwenu endapo mtawaacha wake kabla ya kuwaingilia na kuwakadiria mahari yao. Na wapeni cha kuwaliwaza (kitoka nyumba). Mwenye uwezo mkubwa atoe kulingana na uwezo wake, na mwenye uwezo mdogo atoe kulingana na uwezo alionao. Niliwazo litolewalo kwa wema na ni haki kwa watendao mazuri
وَإِن طَلَّقۡتُمُوهُنَّ مِن قَبۡلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدۡ فَرَضۡتُمۡ لَهُنَّ فَرِيضَةٗ فَنِصۡفُ مَا فَرَضۡتُمۡ إِلَّآ أَن يَعۡفُونَ أَوۡ يَعۡفُوَاْ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ عُقۡدَةُ ٱلنِّكَاحِۚ وَأَن تَعۡفُوٓاْ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۚ وَلَا تَنسَوُاْ ٱلۡفَضۡلَ بَيۡنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ
Na endapo mtawaacha kabla ya kuwaingilia na ilhali mmekwisha kadiria mahari, basi wapeni nusu ya mahari mliokadiria, isipokuwa kama wake wenyewe watasamehe au atasamehe yule ambaye kifungo cha ndoa kipo mikononi mwake. Na kama mtasamehe, hilo liko karibu zaidi na Ucha Mungu. Na msisahau utu kati yenu. Hakika, Allah ni Mwenye kuyaona myatendayo
حَٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوَٰتِ وَٱلصَّلَوٰةِ ٱلۡوُسۡطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَٰنِتِينَ
Zichungeni swala zote (tano) na (ichungeni) swala ya kati. Na simameni kwa ajili ya Allah mkiwa wanyenyekevu
فَإِنۡ خِفۡتُمۡ فَرِجَالًا أَوۡ رُكۡبَانٗاۖ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ
Basi mkiwa na hofu (swalini) mkiwa mnatembea kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani basi mtajeni Allah kama alivyokufundisheni mliyokuwa hamyajui
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا وَصِيَّةٗ لِّأَزۡوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٖۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِي مَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٖۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ
Na wale wanaokufa miongoni mwenu na wakaacha wake, waache Usia kwa ajili ya wake zao wapatiwe matunzo kwa mwaka mzima bila ya kuwatoa (majumbani). Na kama watatoka wenyewe, basi hakuna ubaya kwenu kwa kile walichokifanya kwenye nafsi zao. Na Allah ni Mwenye nguvu mno, Mwingi mno wa hekima
وَلِلۡمُطَلَّقَٰتِ مَتَٰعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ
Na wapeni wanawake wali-oachwa kiliwazo (kitoka nyumba) kwa wema, ikiwa ni haki kwa wam-chao Allah
كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Kama hivi Allah anabainisha Aya zake ili mpate kufahamu
۞أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَهُمۡ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُواْ ثُمَّ أَحۡيَٰهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ
Hivi huwaoni wale waliotoka kwenye miji yao wakiwa maelfu wakiogopa kifo? Na Allah akawaambia kufeni, kisha akawahuisha. Hakika Allah ni mwenye fadhila kwa watu, lakini watu wengi sana hawashukuru
وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Na piganeni katika njia ya Allah, najueni kwamba, Allah ni Mwenye kusikia mno, Mjuzi sana
مَّن ذَا ٱلَّذِي يُقۡرِضُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا فَيُضَٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضۡعَافٗا كَثِيرَةٗۚ وَٱللَّهُ يَقۡبِضُ وَيَبۡصُۜطُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Ni nani anayemkopesha Allah mkopo mzuri iwe sababu Allah amzidishie ziada nyingi? Na Allah anazuia na kutoa, na kwake tu mtarudishwa
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ مِنۢ بَعۡدِ مُوسَىٰٓ إِذۡ قَالُواْ لِنَبِيّٖ لَّهُمُ ٱبۡعَثۡ لَنَا مَلِكٗا نُّقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ قَالَ هَلۡ عَسَيۡتُمۡ إِن كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ أَلَّا تُقَٰتِلُواْۖ قَالُواْ وَمَا لَنَآ أَلَّا نُقَٰتِلَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَدۡ أُخۡرِجۡنَا مِن دِيَٰرِنَا وَأَبۡنَآئِنَاۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ تَوَلَّوۡاْ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ
Je, hukupata habari za mabwana wakubwa wa Wana wa Israili baada ya Musa? Walipomwambia Nabii wao: Tuteulie Mfalme ili tukapigane katika njia ya Allah. Akawaambia: Je, mtakuwa tayari kupigana iwapo mtafaradhishiwa kupigana? Wakasema: Na kwanini tusipigane katika njia ya Allah na ilhali tumetolewa katika makazi yetu na wanetu? Basi walipofaradhishiwa kupigana, waligeuka ila wachache tu miongoni mwao, na Allah anawajua mno madhalimu
وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ بَعَثَ لَكُمۡ طَالُوتَ مَلِكٗاۚ قَالُوٓاْ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ عَلَيۡنَا وَنَحۡنُ أَحَقُّ بِٱلۡمُلۡكِ مِنۡهُ وَلَمۡ يُؤۡتَ سَعَةٗ مِّنَ ٱلۡمَالِۚ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰهُ عَلَيۡكُمۡ وَزَادَهُۥ بَسۡطَةٗ فِي ٱلۡعِلۡمِ وَٱلۡجِسۡمِۖ وَٱللَّهُ يُؤۡتِي مُلۡكَهُۥ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ
Na Nabii wao akawaambia: Hakika Allah ameshakuteulieni Twaluti kuwa Mfalme. Wakasema: Anawezaje kuwa Mfalme wetu, na ilhali sisi tuna haki zaidi ya Ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Hakika Allah ameshakuteulieni na amemzidishia wasaa wa elimu na mwili. Na Allah humpa Ufalme wake amtakaye na Allah ni Mwenye wasaa, Mjuzi mno
وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ءَايَةَ مُلۡكِهِۦٓ أَن يَأۡتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَبَقِيَّةٞ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَٰرُونَ تَحۡمِلُهُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
Na Nabii wao akawaambia: “Hakika alama ya ufalme wake nikukuleteeni sanduku ambalo ndani yake kuna kitulizacho nyoyo zenu kitokacho kwa Mola wenu na mabaki ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Haruni linalobebwa na Malaika. Bila shaka katika hayo mna dalili kwenu ikiwa ninyi ni waumini
فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Basi Twaluti alipoondoka na majeshi alisema: Hakika Allah atakufanyieni mtihani kwa mto, basi atakayekunywa humo si pamoja nami, na asiye yanywa bila shaka yupo pamoja nami, ila atakayeteka kiasi cha kiganja cha mkono wake. Basi walikunywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi alipovuka yeye na walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatumuwezi Jaluti na majeshi yake. Wakasema: wale ambao wana yakini ya kukutana na Allah: Makundi mangapi machache yameyashinda makundi mengi kwa idhini ya Allah? Na Allah yupo pamoja na wafanyao subira
وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na walipotoka (hadharani) kupambana Na Jaluti Na majeshi yake, walisema: Mola wetu! Tumi-minie subira, na uiimarishe miguu yetu na utupe ushindi dhidi ya watu makafiri
فَهَزَمُوهُم بِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّفَسَدَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Basi waliwashinda kwa idhini ya Allah na Daudi akamuua Jaluti, na Allah akampa (Daudi) ufalme na utume na akamfundisha aliyoyataka. Na kama Allah asingewakinga watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka ardhi ingeliharibika, lakini Allah ni Mwenye hisani kubwa mno kwa walimwengu
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Hizi ni Aya za Allah tunazokusomea kwa haki na bila shaka wewe ni miongoni mwa Mitume