وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na lau kama kila nafsi iliyodhu-lumu ingekuwa inamiliki vyote vilivyomo duniani, bila shaka yoyote ingevitoa fidia (ili kujikomboa isiadhibiwe). Na watakapoiona adhabu wataficha majuto na patahu-kumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa
أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Zindukeni: Bila ya shaka, ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Zindukeni: Hakika, ahadi ya Allah ni kweli, na lakini wengi wao sana hawajui
هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Yeye (Allah) anahuisha na anafisha, na kwake tu mtarejeshwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Enyi watu, hakika yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi na ponyo (dawa) ya (maradhi) yaliyomo vifuani (mwenu) na muongozo na rehema kwa Waumini
قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ
Sema: Fadhila za Allah na rehema zake, basi wafurahie hayo. Hilo ni bora zaidi kwao kuliko wanavyovikusanya
قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ
Sema: Hivi mwaonaje, zile riziki alizokuteremshieni Allah na mkafanya baadhi yake haramu na (nyingine) halali, sema (uwaulize): Hivi Allah, amekuruhusuni (hayo) au mnamzulia Allah tu uongo?
وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَشۡكُرُونَ
Na ni ipi dhana ya wanaomzushia Allah uongo Siku ya Kiyama? (Wanadhani hali yao itakuwaje siku hiyo?). Hakika kabisa, Allah ndiye mwenye fadhila kwa watu, na lakini wengi wao sana hawashukuru
وَمَا تَكُونُ فِي شَأۡنٖ وَمَا تَتۡلُواْ مِنۡهُ مِن قُرۡءَانٖ وَلَا تَعۡمَلُونَ مِنۡ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيۡكُمۡ شُهُودًا إِذۡ تُفِيضُونَ فِيهِۚ وَمَا يَعۡزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثۡقَالِ ذَرَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصۡغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرَ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٍ
Na huwi katika jambo lolote na husomi chochote katika Qur’ani na hamtendi kitendo chochote isipokuwa kwamba tumekuwa mashahidi kwenu mnapokiendea (mnapofanya). Na haujifichi kwa Mola wako Mlezi uzito wa chembe ndogo ardhini wala mbinguni na hata kidogo zaidi ya hicho au kikubwa isipokuwa kipo katika kitabu chenye kuweka wazi (kila kitu)
أَلَآ إِنَّ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهِ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Zindukeni: Hakika, Mawalii (wapenzi) wa Allah hawana hofu (yoyote) na hawahuzuniki
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ
(Mawalii wa Allah ni) Ambao wameamini na wakawa wacha Mungu
لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Wana bishara (habari njema) katika maisha ya duniani (kwa kupata wanachokipenda) na Akhera (kwa kuingia Peponi). Hakuna kubadilishwa kwa maneno ya Allah. Hayo ndio mafanikio makubwa
وَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًاۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Na zisikuhuzunishe kauli zao[1]. Hakika, utukufu wote ni wa Allah tu. Yeye tu ndiye Mwenye kusikia, Mjuzi sana
1- - Makafiri walikuwa wakimwambia Mtume kauli nyingi za kejeli na kumkatisha tamaa. Miongoni mwa kauli hizo walizokuwa wakimwambia ni pamoja na hii: Wewe sio Mtume n.k.
أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا يَتَّبِعُ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُرَكَآءَۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ
Zindukeni kuwa, wote waliomo mbinguni na ardhini ni wa Allah tu. Na wale wanaowaomba (Miungu) wengine kinyume na Allah hawawafuati washirika. Hawafuati isipokuwa dhana tu na hawana chochote isipokuwa wanasema uongo tu
هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبۡصِرًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ
Yeye (Allah) ndiye ambaye amekuwekeeni usiku ili muweze kutulia humo na (amekuwekeeni) mchana ukiangaza (ili mpate kuona na kufanya shughuli zenu mbali mbali). Hakika, katika haya zipo ishara (za kuzingatia) kwa watu wanaosikia (na kuzingatia)
قَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ هُوَ ٱلۡغَنِيُّۖ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنۡ عِندَكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭ بِهَٰذَآۚ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
(Wayahudi na Wakristo na wanaoiga itikadi zao) Wamesema: Allah ana mtoto. Utakasifu ni wake! Yeye tu ndiye Mkwasi. Ni vyake yeye tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nyinyi hamna hoja yoyote juu ya haya! Hivi mnamsingizia Allah msiyoyajua?
قُلۡ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ
Sema: Hakika, wale wanaomzushia Allah uwongo, hawafaulu
مَتَٰعٞ فِي ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ ٱلۡعَذَابَ ٱلشَّدِيدَ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ
Ni starehe (ndogo) tu duniani, kisha marejeo yao ni kwetu tu, kisha tutawaonjesha adhabu kali, kwa sababu ya ukafiri waliokuwa wakiufanya
۞وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ
Na wasomee habari za (Mtume) Nuhu wakati alipowaambia watu wake kuwa: “Enyi watu wangu, ikiwa mnachukizwa na kuishi kwangu (na nyinyi) na kukumbusha kwangu Aya za Allah, basi mimi nimemtegemea Allah tu. Basi amueni jambo lenu nyinyi na washirika (Miungu) wenu, kisha jambo lenu lisiwe la kificho, kisha pitisheni hukumu kwangu na msinicheleweshe
فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَمَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Basi mkikengeuka, mimi sikukuombeni ujira wowote. Ujira wangu haupo (popote) isipokuwa kwa Allah tu, na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu”
فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَـٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ
Basi (watu wake) wakamka-dhibisha (wakampinga Mtume Nuhu), tukamuokoa yeye na waliokuwepo pamoja naye katika mashua, na tukawafanya warithi (wa nafasi za walioangamizwa) na tukawazamisha baharini wale waliozikadhibisha Aya zetu. Basi angalia namna ulivyokuwa mwisho wa walio onywa
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ بِهِۦ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ نَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡمُعۡتَدِينَ
Kisha baada yake tuliwatuma Mitume (mbali mbali) kwa watu wao, na (Mitume hao) waliwaendea kwa hoja za waziwazi. Hawakuweza kuyaamini yale waliyoyapinga hapo kabla. Kama hivyo, tunazipiga chapa nyoyo za watu wavukao mipaka (ya sheria za Allah)
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ
Kisha tukamtuma Musa na Haruna baada ya hao kwenda kwa Firauni na mamwinyi wake (wakiwa na) Aya zetu. Basi wakafanya kiburi na wakawa watu wakosefu
فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰذَا لَسِحۡرٞ مُّبِينٞ
Basi ilipowajia haki kutoka kwetu walisema: “Bila shaka, huu hasa ni uchawi ulio dhahiri sana”
قَالَ مُوسَىٰٓ أَتَقُولُونَ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَكُمۡۖ أَسِحۡرٌ هَٰذَا وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّـٰحِرُونَ
Akasema Musa: Hivi, mnasema kuhusu haki ilipokujieni kwamba, huu ni uchawi? Na wachawi hawafaulu
قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ
Wakasema: “Hivi, umetujia ili utuondoe katika yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ukubwa uwe wenu wawili nyie katika ardhi? Na sisi kamwe hatutakuaminini”
وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ ٱئۡتُونِي بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mahiri sana
فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلۡقُواْ مَآ أَنتُم مُّلۡقُونَ
Basi wachawi walipofika, Musa aliwaambia: Tupeni (chini) mnavyotaka kuvitupa (chini)
فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئۡتُم بِهِ ٱلسِّحۡرُۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُۥٓ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُصۡلِحُ عَمَلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Basi (wachawi) walipotupa, Musa akasema: “Hiki mlicholeta ni uchawi. Hakika, Allah ataubatilisha. Hakika, Allah hastawishi vitendo vya waharibifu”
وَيُحِقُّ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Na Allah anahakikisha haki inashinda kwa maneno yake, na hata kama waovu watachukia
فَمَآ ءَامَنَ لِمُوسَىٰٓ إِلَّا ذُرِّيَّةٞ مِّن قَوۡمِهِۦ عَلَىٰ خَوۡفٖ مِّن فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِمۡ أَن يَفۡتِنَهُمۡۚ وَإِنَّ فِرۡعَوۡنَ لَعَالٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Basi hakuna aliyemuamini Musa (pamoja na dalili na hoja zote alizowaonesha) isipokuwa vijana wachache katika kaumu yake huku wakiwa na hofu (ya kumuogopa) Firauni na mamwinyi wao wasiwatese. Na hakika kabisa, Firauni alikuwa mwenye kujikweza ardhini, na kwa yakini kabisa yeye (Firauni) alikuwa miongoni mwa waliokiuka mipaka (katika kufanya uovu)