۞وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ
Na kama mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, basi (mdai) apewe (kitu) kiwe rehani mikononi mwake. Na kama mtaaminiana, basi aliyeaminiwa atekeleze uaminifu wake, na amche Allah, Mola wake Mlezi. Na msifiche ushahidi. Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Allah ni mwenye kuyajua mno yote mnayoyatenda
لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na kama mkidhihirisha yaliyomo katika nyoyo zenu, au mkiyaficha, Allah atakuhojini kwayo; kwahiyo atamsamehe amtakaye, na atamuadhibu amtakaye. Na Allah ni Mwenye uweza mno wa kila kitu
ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ
Mtume ameamini yote yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi na Waumini (pia wameamini hivyo). Kila mmoja amemwamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake. (Waumini na Mtume wao husema), “Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake (wote tunawaamini). Na husema: “Tumesikia na tumetii tunakuomba msamaha ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako tu
لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَعَلَيۡهَا مَا ٱكۡتَسَبَتۡۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذۡنَآ إِن نَّسِينَآ أَوۡ أَخۡطَأۡنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تَحۡمِلۡ عَلَيۡنَآ إِصۡرٗا كَمَا حَمَلۡتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلۡنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦۖ وَٱعۡفُ عَنَّا وَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَآۚ أَنتَ مَوۡلَىٰنَا فَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Allah haikalifishi nafsi yoyote ila (kwa) iliwezalo. Itafaidika na mema iliyoyachuma na itadhurika na mabaya iliyoyachuma. (Waumini) wanasema: “(Ewe) Mola wetu Mlezi, usitutie hatiani kama tukisahahu (kutenda yaliyo mema) au tukikosea (kwa kutenda mabaya). (Ewe) Mola wetu Mlezi, na usitubebeshe mazito kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. (Ewe) Mola wetu Mlezi, usitubebeshe tusiyoyaweza, na tusamehe na tughufirie na turehemu. Wewe ndiye Mola wetu. Basi tusaidie dhidi ya watu makafiri
الٓمٓ
Alif Laam Miim[1]
1- - Allah ndiye ajuwaye zaidi madhumuni ya herufi hizi.
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ
Allah, hakuna Mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Yeye tu, Mwenye uhai wa milele, Mwenye kusimamia mambo yote
نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ
Amekuteremshia Kitabu kwa haki kikisadikisha yaliyokuwepo kabla yake. Na ameteremshaTaurati na Injili
مِن قَبۡلُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلۡفُرۡقَانَۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ
(Ameteremsha Taurati na Injili) Kabla (ya Kurani) ili (vitabu vyote hivyo) viwe muongozo kwa watu. Na ameteremsha Alfurqan. Hakika, wale waliokanusha Aya za Allah watapata adhabu kali, na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kutesa
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخۡفَىٰ عَلَيۡهِ شَيۡءٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ
Kwa hakika, Allah hakijifichi kwake chochote; sio ardhini wala mbinguni
هُوَ ٱلَّذِي يُصَوِّرُكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡحَامِ كَيۡفَ يَشَآءُۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Yeye ndiye anayekutieni maumbo mkiwa katika mifuko ya uzazi kwa namna apendavyo. Hakuna aliye na haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, Mwenye nguvu kubwa, Mwingi wa hekima
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu. Baadhi ya Aya zake zinafahamika kwa wepesi (na) ambazo ndio msingi wa kitabu (hiki cha Kurani). Na (Aya) nyingine zinatatiza. Ama wale ambao ndani ya nyoyo zao kuna upotevu, wanafuata (Aya) zinazotatiza, kwa kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Na hakuna anayejua tafsiri yake (halisi) isipokuwa Allah tu. Na wale waliobobea katika elimu husema: Tumeziamini (Aya) zote. Zote (hizo) zinatoka kwa Mola wetu Mlezi. Na hawawaidhiki isipokuwa wenye akili tu
رَبَّنَا لَا تُزِغۡ قُلُوبَنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَيۡتَنَا وَهَبۡ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةًۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡوَهَّابُ
Ewe Mola wetu, usiziache nyoyo zetu zipotee baada ya kuwa umetuongoza, na tunaomba rehema kwako. Hakika, wewe ni Mtoaji sana
رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ
Ewe Mola wetu, hakika wewe ni mwenye kuwakusanya watu katika siku isiyokuwa na shaka. Hakika, Allah havunji ahadi
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمۡ وَقُودُ ٱلنَّارِ
Hakika, waliokufuru, katu hazitawasaidia chochote mali zao wala watoto wao kwa Allah, na hao ndio kuniza Motoni
كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
Sawa na mwenendo wa watu wa Firauni na wale waliokuwepo kabla yao; walizipinga Aya zetu, basi Allah akawaadhibu kwa sababu ya madhambi yao na Allah ni Mkali sana wa kuadhibu
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغۡلَبُونَ وَتُحۡشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ
Waambie waliokufuru kwamba: Mtashindwa na mtakusanywa mpelekwe Jahanamu, na hayo ni makazi mabaya sana
قَدۡ كَانَ لَكُمۡ ءَايَةٞ فِي فِئَتَيۡنِ ٱلۡتَقَتَاۖ فِئَةٞ تُقَٰتِلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَأُخۡرَىٰ كَافِرَةٞ يَرَوۡنَهُم مِّثۡلَيۡهِمۡ رَأۡيَ ٱلۡعَيۡنِۚ وَٱللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصۡرِهِۦ مَن يَشَآءُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ
Hakika, ilikuwepo kwenu alama katika makundi mawili yaliyokutana (katika vita). Kundi moja likipigana katika njia ya Allah, na jingine la makafiri wanawaona (Waislamu) kwa mtazamo wa macho mara mbili yao. Na Allah anamtia nguvu amtakaye kwa (kumpa) ushindi wake. Hakika, katika hilo kuna mazingatio kwa wenye kuona mbali
زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٰلِكَ مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ
Watu wamepambiwa kupenda kutamani wanawake na watoto wanaume na marundo mengi ya dhahabu na fedha na farasi wanaofunzwa na wanyama wafugwao na mashamba. Hizo ni starehe za maisha ya duniani, na mafikio mazuri yapo kwa Allah tu