۞قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلۡأَرۡذَلُونَ
Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanaokufuata ni watu wa chini?
Compartir :
قَالَ وَمَا عِلۡمِي بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
إِنۡ حِسَابُهُمۡ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّيۖ لَوۡ تَشۡعُرُونَ
Hesabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini
إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Mimi si chochote ila ni Muonyaji wa dhahiri
قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمَرۡجُومِينَ
Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوۡمِي كَذَّبُونِ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha
فَٱفۡتَحۡ بَيۡنِي وَبَيۡنَهُمۡ فَتۡحٗا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Kwahivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni
ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا بَعۡدُ ٱلۡبَاقِينَ
Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo ishara, lakini si wengi wao waliokuwa waumini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
كَذَّبَتۡ عَادٌ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kina A’d waliwakanusha Mitume
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamumchi Allah?
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Allah, na nitiini mimi
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
أَتَبۡنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةٗ تَعۡبَثُونَ
Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمۡ تَخۡلُدُونَ
Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
وَإِذَا بَطَشۡتُم بَطَشۡتُمۡ جَبَّارِينَ
Na mnapotumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari
Basi mcheni Allah, na nitiini
وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِيٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعۡلَمُونَ
Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua
أَمَدَّكُم بِأَنۡعَٰمٖ وَبَنِينَ
Amekupeni wanyama wa kufuga na watoto
وَجَنَّـٰتٖ وَعُيُونٍ
Na mabustani na chemchem
إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku kubwa
قَالُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَوَعَظۡتَ أَمۡ لَمۡ تَكُن مِّنَ ٱلۡوَٰعِظِينَ
Wakasema: Ni sawasawa kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani
وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
Wala sisi hatutaadhibiwa
فَكَذَّبُوهُ فَأَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Wakamkanusha; nasi tukawaan-gamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu