وَمِمَّنۡ خَلَقۡنَآ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ
Na katika tuliowaumba upo umma unao ongoza kwa kutumia haki na kwa (haki) hiyo wanafanya uadilifu
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ
Na wale waliozikadhibisha Aya zetu, tutakwenda nao pole pole kwa namna ambayo (wenyewe) hawaijui
وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ
Na ninawapa muda. Hakika, mkakati wangu ni madhubuti sana
أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Hivi hawatafakari? Huyu mwen-zao (Mtume Muhammad) hana chembe ya wazimu! Hakuwa yeye isipokuwa tu ni Muonyaji dhahiri
أَوَلَمۡ يَنظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ وَأَنۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقۡتَرَبَ أَجَلُهُمۡۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Hivi hawautafakari ufalme (mkubwa) wa mbinguni na ardhini na vitu vyote (vingine) ambavyo Allah ameviumba na kwamba inawezekana kuwa muda wao utakuwa umekaribia? Basi ni mazungumzo gani tena baada ya haya watayaamini?
مَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُۥۚ وَيَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Wote ambao Allah amewaacha wapotee hakuna wa kuwaongoza, na anawaacha katika upotevu wao wakitangatanga
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Wanakuuliza kuhusu Kiyama; ni lini? Sema: Ilivyo ni kwamba ujuzi wake upo kwa Mola wangu Mlezi. Hakuna wa kuuweka wazi wakati wake isipokuwa yeye tu. Limekuwa jambo zito mno mbinguni na ardhini. Hakitakujieni isipokuwa tu kwa ghafla. Wanakuuliza kuhusu hicho (Kiyama) kama vile wewe umekitafiti (na ukakijua bara bara). Sema (uwaambie): Ujuzi wake uko kwa Allah na lakini watu wengi hawajui
قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي نَفۡعٗا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ وَلَوۡ كُنتُ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ لَٱسۡتَكۡثَرۡتُ مِنَ ٱلۡخَيۡرِ وَمَا مَسَّنِيَ ٱلسُّوٓءُۚ إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Sema: Similiki manufaa wala madhara kuiletea nafsi yangu, isipokuwa tu alitakalo Allah (ndilo linaloweza kunifika; liwe jema au baya). Na lau kama ningekuwa najua Ghaibu (yaliyojificha) ningefanya sana (mambo ya) kheri na lisingenigusa jambo baya (lolote). Mimi sio chochote isipokwa tu ni Muonyaji na Mbashiri (Mtoaji habari njema) kwa watu wanaoamini
۞هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ
Yeye (Allah) Ndiye aliyeku-umbeni kutokana na nafsi moja (Adamu), na akajaalia kutoka katika nafsi hiyo mkewe ili apate utulivu kwake. Na (Adamu) alipomuingilia (mkewe) tu alibeba mimba nyepesi (kwa sababu ndio kwanza ilitunga) na aliweza kutembea nayo. Basi alipopata uzito (wa mimba kwa sababu ilikuwa kubwa) wote wawili (Adamu na mkewe) walimuomba Allah Mola wao Mlezi (na kusema): Kwa yakini kabisa (ewe Mola wetu), kama utatupa (mtoto) mwema bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَٰلِحٗا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَاۚ فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Basi (Allah) alipowapa wawili hao (mtoto) mwema, walimfanyia yeye (Allah) washirika katika kile alichowapa.[1] Basi Allah ametakasika na vyote wanavyovishirikisha naye
1- - Wanazuoni wa Kisunna (Ahlus Sunna Wal Jamaa) wanaamini kwamba, Adamu kama Nabii wa Allah hawezi kumfanyia ushirika Allah katika kumuomba na kumuabudu. Neno ushirikishaji ulikousudiwa hapa ni msamiati wa lugha tu na hauna maana ile ya kisheria inayomtoa muumini katika Imani yake.
أَيُشۡرِكُونَ مَا لَا يَخۡلُقُ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Hivi wanafanya ushirikina (wa kuvishirikisha na Allah na kuvifanya Miungu) visivyokuwa na uwezo wa kuumba chochote, na ilhali Miungu hao (wanaoshirikishwa ndio) wanaumbwa?
وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ لَهُمۡ نَصۡرٗا وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Na hawana uwezo wa kuwanusuru wao, wala wao wenyewe hawawezi kujinusuru
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمۡۚ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡ أَدَعَوۡتُمُوهُمۡ أَمۡ أَنتُمۡ صَٰمِتُونَ
Na mkiwaita wafuate muongozo (wa Allah) hawakufuateni. Ni sawa kwenu; mmewaita au mmekaa kimya
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Hakika, wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allah ni waja mfano wenu (ni waja kama nyinyi). Basi waombeni wakuitikieni, ikiwa nyinyi ni wakweli
أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ
Hivi wana miguu wanayotembelea? au wana mikono wanayokamatia? au wana macho wanayo onea? au wana masikio wanayosikilizia? Sema (uwaambie): Waiteni hao washirika wenu kisha nifanyieni vitimbi vyenu wala msinicheleweshe
إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ
Hakika, mlinzi wangu ni Allah ambaye ameteremsha kitabu (Qur’ani), naye ndiye anawalinda waja wema
وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَكُمۡ وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Na wale mnaowaomba badala yake hawawezi kukunusuruni wala wao wenyewe hawawezi kujinusuru
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَسۡمَعُواْۖ وَتَرَىٰهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ وَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Na kama mtawaita wafuate muongozo (wa Allah) hawasikii, na utawaona wanakukodolea macho na ilhali hawaoni
خُذِ ٱلۡعَفۡوَ وَأۡمُرۡ بِٱلۡعُرۡفِ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Samehe na amrisha mema, na wapuuze wajinga
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ نَزۡغٞ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Na iwapo utahisi ushawishi wowote wa shetani basi omba kinga kwa Allah. Hakika, yeye (Allah) ni Msikivu sana, Mjuzi mno
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّهُمۡ طَـٰٓئِفٞ مِّنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ تَذَكَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ
Hakika, wale wamchao Allah ukiwagusa upepo (wasiwasi, uchochezi na ushawishi) wa shetani wanakumbuka (mafundisho na muongozo wa Allah) na hapo hapo wanaona (haki na kuifuata)
وَإِخۡوَٰنُهُمۡ يَمُدُّونَهُمۡ فِي ٱلۡغَيِّ ثُمَّ لَا يُقۡصِرُونَ
Na ndugu zao wanawavuta kwenye upotevu kisha hawaachi
وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Na usipowaletea Aya (zile wanazozitaka wao au muujiza wanaoutaka) wanasema: Kwa nini usiubuni (usilete wa kutengeneza)? Sema (uwaambie kuwa): Ukweli ni kwamba, mimi nafuata kile kinachofunuliwa kwangu (Wahyi) kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Hii (Qur’ani) ni mwangaza kutoka kwa Mola wenu Mlezi na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na wakati inasomwa Qur’ani isikilizeni na nyamazeni ili mpate kupewa rehema[1]
1- - Aya hii ina mafunzo makubwa kwa Muislamu. 1) Kuiheshimu Qur’ani kwa kuisikiliza na kukaa kimya. 2) Muislamu anapata rehema kwa kutekeleza agizo la kusikiliza na kukaa kimya. 3) Kama kusikiliza tu na kukaa kimya Muislamu anapata rehema, hii inaonesha kwamba kuifanyia kazi Qur’ani na kutekeleza mafunzo yake kuna rehema zaidi. 4) Ni muhimu kwa Muislamu kuangalia mazingira ya kusoma Qur’ani. Kwa muktadha huu, si jambo jema na ni makuruhu kusoma Qur’ani au kuweka sauti ya Qu’ani katika mazingira ambayo sio rafiki kama kwenye mikusanyiko ya sokoni, dukani, ndani ya vyombo vya usafiri n.k.
وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِي نَفۡسِكَ تَضَرُّعٗا وَخِيفَةٗ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Na mtaje Mola wako ndani ya nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa hofu na bila ya kupaza sauti. (Mtaje) Asubuhi na jioni, na usiwe miongoni mwa wenye kughafilika
إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُۥ وَلَهُۥ يَسۡجُدُونَۤ۩
Hakika, wale waliopo kwa Mola wako (Malaika) hawajivuni wakaacha kumuabudu, na wanamtakasa na wanamsujudia yeye tu