إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ
Hakika Sisi Tulipeleka Kwao Ukelele Moja tu, wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi
Compartir :
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na Hakika Tumeirahisisha Qur’an Kwa Ajili Ya Ukumbusho Je Kuna Mwenye kukumbuka
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ
Wamekadhibisha Watu wa Luutwi Mitume waonyaji
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ
Hakika Sisi Tumewapelekea Upepo Uliyo Na Mchanga Ispokua Watu Wa Luutwi Waliyomuamini Tuliwaokoa Wakati Wa Theluthi Ya Mwisho Ya Usiku
نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ
Neema kutoka Kwetu, hivyo ndivyo Tunavyomlipa ambaye ameshukuru
وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ
Na Hakika Aliwaonya Kuhusiana Na Adhabu Yetu Wakatia Shaka Na Maonyo Hayo
وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Na kwa yakini walimshawishi awape wageni wake, basi Tukawapofoa macho yao. Basi onjeni adhabu Yangu na maonyo Yangu
وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ
Hakika Iliwafika Wao Adhabu Yenye Kudumu Asubuhi Mapema
فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi Onjeni Adhabu Yangu na Maonyo
Na Hakika Tumeirahisisha Qur’ani kwaajili ya Ukumbusho Je Kuna Mwenye kukumbuka.?
وَلَقَدۡ جَآءَ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ ٱلنُّذُرُ
Hakika yaliwajia watu wafiraun maonyo
كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذۡنَٰهُمۡ أَخۡذَ عَزِيزٖ مُّقۡتَدِرٍ
Na kwa yakini watu wa Fir’awn walifikiwa na waonyaji
أَكُفَّارُكُمۡ خَيۡرٞ مِّنۡ أُوْلَـٰٓئِكُمۡ أَمۡ لَكُم بَرَآءَةٞ فِي ٱلزُّبُرِ
Je, makafiri wenu (enyi Maquraysh) ni bora kuliko hao (ummah) wa awali? Au mna msamaha katika Maandiko Tukufu?
أَمۡ يَقُولُونَ نَحۡنُ جَمِيعٞ مُّنتَصِرٞ
Au wanasema: Sisi ni wengi (kundi) tutashinda tu.?
سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ
Litashindwa kundi hilo na watakimbia
بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوۡعِدُهُمۡ وَٱلسَّاعَةُ أَدۡهَىٰ وَأَمَرُّ
Bali Kiyama Ndio Ahadi Yao Na Adhabu Ya Kiyama Kubwa Na Chungu Zaidi
إِنَّ ٱلۡمُجۡرِمِينَ فِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٖ
Hakika wahalifu wamo katika upotofu na wazimu
يَوۡمَ يُسۡحَبُونَ فِي ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ ذُوقُواْ مَسَّ سَقَرَ
Siku watakayoburutwa motoni kifudi fudi, Waambiwe: Onjeni mguso wa moto mkali mno
إِنَّا كُلَّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَٰهُ بِقَدَرٖ
Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar (makadirio)
وَمَآ أَمۡرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٞ كَلَمۡحِۭ بِٱلۡبَصَرِ
Na amri Yetu haiwi ila ni moja tu, kama upepeso wa jicho
وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَآ أَشۡيَاعَكُمۡ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na kwa yakini Tumewaangamiza wenzenu, je, basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
وَكُلُّ شَيۡءٖ فَعَلُوهُ فِي ٱلزُّبُرِ
Na yote waliyoyafanya yamehi-fadhiwa kwenye vitabu
وَكُلُّ صَغِيرٖ وَكَبِيرٖ مُّسۡتَطَرٌ
Na kila kidogo na kikubwa kime-andikwa
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّـٰتٖ وَنَهَرٖ
Hakika Waliomcha Allah watakua kwenye mabustani Na Mito
فِي مَقۡعَدِ صِدۡقٍ عِندَ مَلِيكٖ مُّقۡتَدِرِۭ
Katika kizazi kilichoridhiwa mbele ya Mfalme aliye Muweza