قَدۡ كَانَ لَكُمۡ ءَايَةٞ فِي فِئَتَيۡنِ ٱلۡتَقَتَاۖ فِئَةٞ تُقَٰتِلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَأُخۡرَىٰ كَافِرَةٞ يَرَوۡنَهُم مِّثۡلَيۡهِمۡ رَأۡيَ ٱلۡعَيۡنِۚ وَٱللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصۡرِهِۦ مَن يَشَآءُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ
Hakika, ilikuwepo kwenu alama katika makundi mawili yaliyokutana (katika vita). Kundi moja likipigana katika njia ya Allah, na jingine la makafiri wanawaona (Waislamu) kwa mtazamo wa macho mara mbili yao. Na Allah anamtia nguvu amtakaye kwa (kumpa) ushindi wake. Hakika, katika hilo kuna mazingatio kwa wenye kuona mbali
كَمَآ أَخۡرَجَكَ رَبُّكَ مِنۢ بَيۡتِكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لَكَٰرِهُونَ
Kama Mola wako Mlezi alivyokutoa nyumbani kwako (Madina) kwa haki (kwenda vitani na Swahaba wanachukia kwa kuwa wachache na hawakuwa na maandalizi ya vita), na kwa hakika kabisa kundi moja miongoni mwa Waumini lilikereka sana
يُجَٰدِلُونَكَ فِي ٱلۡحَقِّ بَعۡدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلۡمَوۡتِ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wanajadiliana nawe katika jambo la haki (vita) baada ya kuwa limeshakuwa bayana (na kwa kuogopa kwao vita ilikuwa) kama kwamba wanaswagwa kupelekwa kwenye kifo huku wanatazama
وَإِذۡ يَعِدُكُمُ ٱللَّهُ إِحۡدَى ٱلطَّآئِفَتَيۡنِ أَنَّهَا لَكُمۡ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيۡرَ ذَاتِ ٱلشَّوۡكَةِ تَكُونُ لَكُمۡ وَيُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُحِقَّ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَيَقۡطَعَ دَابِرَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na (kumbukeni) wakati Allah anakuahidini kuwa, moja ya makundi mawili ni lenu. Nanyi mkapenda kundi lisilokuwa na silaha ndio liwe lenu. Na Allah anataka aisimamishe haki kwa maneno yake, na aukate mzizi wa makafiri (awaangamize)
لِيُحِقَّ ٱلۡحَقَّ وَيُبۡطِلَ ٱلۡبَٰطِلَ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ
(Allah ameyafanya hayo) Ili aisimamishe haki na ateketeze batili (ukafiri) na hata kama waovu watachukia
إِذۡ تَسۡتَغِيثُونَ رَبَّكُمۡ فَٱسۡتَجَابَ لَكُمۡ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلۡفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ مُرۡدِفِينَ
(Kumbukeni) Wakati mna-muomba msaada Mola wenu Mlezi akuokoeni (dhidi ya maadui zenu), akakujibuni kuwa: Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa (kuleta vikosi vya) Malaika elfu moja wanaofuatana mfululizo
وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ وَلِتَطۡمَئِنَّ بِهِۦ قُلُوبُكُمۡۚ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na Allah hakulifanya (hili la kuleta vikosi vya Malaika) ila liwe bishara na ili kwalo nyoyo zenu zituwe (zitulizane). Na (ili hatimae mjue kwamba,) haupatikani ushindi ila kutoka kwa Allah tu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima
إِذۡ يُغَشِّيكُمُ ٱلنُّعَاسَ أَمَنَةٗ مِّنۡهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ لِّيُطَهِّرَكُم بِهِۦ وَيُذۡهِبَ عَنكُمۡ رِجۡزَ ٱلشَّيۡطَٰنِ وَلِيَرۡبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمۡ وَيُثَبِّتَ بِهِ ٱلۡأَقۡدَامَ
(Kumbukeni) Wakati (Allah) anakugubikeni kwa lepe la usingizi (kwenye usiku wa kuamkia vita) kwa ajili ya amani na utulivu kutoka kwake, na anakuteremshieni maji (mvua) kutoka mawinguni ili kwayo akusafisheni (Hadathi na Janaba) na kukuondoleeni wasiwasi wa Shetani (hofu), na ili azipe nguvu nyoyo zenu, na kwa (yote) hayo aiimarishe miguu yenu (isitetereke kwenye medani ya vita)
إِذۡ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ أَنِّي مَعَكُمۡ فَثَبِّتُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ سَأُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ فَٱضۡرِبُواْ فَوۡقَ ٱلۡأَعۡنَاقِ وَٱضۡرِبُواْ مِنۡهُمۡ كُلَّ بَنَانٖ
(Kumbuka) Wakati Mola wako Mlezi alipowapa Wahyi (vikosi vya) Malaika kwamba: Hakika Mimi nipo pamoja nanyi (kwa kukusaidieni na kukupeni ushindi), basi watieni nguvu walioamini (kwa kuwapa bishara njema). Nitatia woga kwenye nyoyo za waliokufuru (hadi washindwe). Basi wapigeni juu ya shingo (vichwani) na wapigeni kwenye kila ncha za vidole (vya mikono na miguu)
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ شَآقُّواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَمَن يُشَاقِقِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
Hilo (la kuwapiga Washirikina) ni kwasababu wamemuasi Allah na Mtume wake (na kuwafurusha waumini kwenye miji yao). Na mwenye kumuasi Allah na Mtume wake basi (ajue) Allah ni Mkali wa kuadhibu
ذَٰلِكُمۡ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابَ ٱلنَّارِ
Hiyo (adhabu ya awali mliyoipata enyi makafiri ya kukatwa shingo na vidole vitani) basi ionjeni. Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto (Akhera)
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ زَحۡفٗا فَلَا تُوَلُّوهُمُ ٱلۡأَدۡبَارَ
Enyi Mlioamini, mkikutana na (kundi la majeshi ya) waliokufuru uso kwa uso (vitani) msiwageuzie mgongo (msiwakimbie)
وَمَن يُوَلِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ دُبُرَهُۥٓ إِلَّا مُتَحَرِّفٗا لِّقِتَالٍ أَوۡ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٖ فَقَدۡ بَآءَ بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأۡوَىٰهُ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo (atakayewakimbia) isipokuwa kama (amefanya hivyo kama) mbinu za vita (geresha) au kuungana na kikosi (cha wapiganaji wenzake), basi atakuwa amestahiki ghadhabu kutoka kwa Allah na makazi yake ni Jahanamu, na huo ni mwisho mbaya mno
فَلَمۡ تَقۡتُلُوهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمۡۚ وَمَا رَمَيۡتَ إِذۡ رَمَيۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِيُبۡلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡهُ بَلَآءً حَسَنًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Basi (Kwenye Siku ya Badri) hamkuwaua nyinyi (hao makafiri kwa nguvu na uhodari wenu) lakini Allah ndiye aliyewaua. Na wewe (Muhammad) hukutupa (na kuufikisha mchanga kwenye nyuso za makafiri), lakini Allah ndiye aliyetupa (aliyeufikisha mchanga na ukawapata makafiri), na ili awajaribu Waumini kutokana na hayo majaribio mazuri (kwa kuwapa neema ya ngawira walio hai na waliouawa wakiwa mashahidi). Hakika Allah ni Msikivu, Mjuzi sana
ذَٰلِكُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُوهِنُ كَيۡدِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
(Tukio hilo la vita vya Badri lililenga kuwatahini waumini), na hakika Allah ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri
إِن تَسۡتَفۡتِحُواْ فَقَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡفَتۡحُۖ وَإِن تَنتَهُواْ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَعُودُواْ نَعُدۡ وَلَن تُغۡنِيَ عَنكُمۡ فِئَتُكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَوۡ كَثُرَتۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Kama mnataka ushindi (kwenye vita) basi ushindi ume-kwishakujieni[1]. Na mkiacha (kupigana na Mtume na Waislamu) itakuwa ndio heri kwenu (duniani na Akhera). Na mkirejea (kupigana na Mtume na Waislamu) sisi pia tutarejea (kuwapa kichapo na kipigo) na katu kundi (jeshi) lenu halitakufaeni kitu chochote, hata kama litakuwa kubwa, na kwa hakika Allah yupo pamoja na waumini
1- - Hapa wanaambiwa makafiri kwa lugha ya kuwakejeli kwamba mnataka kuwashinda Waislamu basi mmekwishaupata kwa kichapo mlichokipata katika vita vya Badri! Walichokipata ni kipigo na sio ushindi!
إِذۡ أَنتُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلۡقُصۡوَىٰ وَٱلرَّكۡبُ أَسۡفَلَ مِنكُمۡۚ وَلَوۡ تَوَاعَدتُّمۡ لَٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡمِيعَٰدِ وَلَٰكِن لِّيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗا لِّيَهۡلِكَ مَنۡ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٖ وَيَحۡيَىٰ مَنۡ حَيَّ عَنۢ بَيِّنَةٖۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ
(Kumbukeni) Wakati nyinyi mlipokuwa kando ya bonde la karibu (na Madina), na wao (makafiri) walikuwa upande wa bonde la mbali (na Madina), na ilhali msafara (wa Abu Sufiyan) ukiwa chini zaidi yenu. Na ingelikuwa mmeagana (nyinyi na majeshi ya Makureishi) bila shaka mngetafautiana katika miadi (ya kufika Badri). Lakini (mkakutana) ili Allah atimize jambo lililokuwa lazima litendeke, ili aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo wazi, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo wazi. Na kwa hakika kabisa, Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua
إِذۡ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلٗاۖ وَلَوۡ أَرَىٰكَهُمۡ كَثِيرٗا لَّفَشِلۡتُمۡ وَلَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
(Kumbuka) Wakati Allah ana-kuonyesha usingizini mwako (kabla ya vita) kwamba wao (makafiri ni) wachache. Na lau angekuonyesha kuwa (makafiri) ni wengi, kwa yakini kabisa mngeingiwa na woga na mngelizozana katika jambo (hilo). Lakini Allah akaleta salama. Hakika, Yeye (Allah) ni Mwenye kuyajua yaliyomo nyoyoni
وَإِذۡ يُرِيكُمُوهُمۡ إِذِ ٱلۡتَقَيۡتُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِكُمۡ قَلِيلٗا وَيُقَلِّلُكُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِهِمۡ لِيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗاۗ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ
Na (kumbukeni) wakati (Allah) anakuonyesheni machoni mwenu mlipokutana (nao) kuwa wao ni wachache mno, na anakufanyeni nyinyi wachache machoni mwao, ili Allah atimize jambo lililokuwa liwe[1]. Na kwa Allah tu hurejeshwa mambo yote
1- - Allah amelizungumzia tukio hili pia katika Sura Al-imran (3) 13: “Hakika imepetikana Aya kubwa
kwenu katika yale makundi mawili yaliyokutana (Siku ya Badri); kundi moja likipigana katika njia ya Allah
na jingine limekufuru. (Makafiri wakawaona (Waislamu) wapo zaidi kuliko wao mara mbili kwa kuona
kwa macho; na Allah humtia nguvu amtakaye kwa nusra yake. Kwa yakini katika hayo yapo mazingatio
kwa mwenye upeo.”
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمۡ فِئَةٗ فَٱثۡبُتُواْ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Enyi mlioamini, mkikutana na jeshi (la makafiri), basi kuweni thabiti (kuweni imara na msikimbie), na mtajeni sana Allah (muombeni) ili mpate kufanikiwa
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُواْ فَتَفۡشَلُواْ وَتَذۡهَبَ رِيحُكُمۡۖ وَٱصۡبِرُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Na mtiini Allah na Mtume wake, wala msizozane mtasambaratika (na woga utakutawaleni) na nguvu zenu zitatoweka. Na vumilieni. Hakika Allah yupo pamoja na wavumilivu
وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِم بَطَرٗا وَرِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ
Na msiwe kama wale (washi-rikina) waliotoka majumbani mwao (chini ya ujemedari wa Abu Jahali) kwa mbwembwe na kujionyesha kwa watu (ili wasifiwe)[1], na wanawazuia (watu) kwenye njia ya Allah (wasijiunge na Uislamu). Na Allah anayajua vyema yote wayafanyayo
1- - Kuwa nguvu za kuwapiga Waislamu wanazo, uwezo wanao na nia wanayo.
وَإِذۡ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلۡيَوۡمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّي جَارٞ لَّكُمۡۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلۡفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكُمۡ إِنِّيٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوۡنَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
Na (kumbukeni) wakati Shetani alipowapambia (alipowaaminisha makafiri kwamba) amali zao (ni nzuri) na akawaambia: Leo hii hakuna watu wa kukushindeni, na hakika mimi nipo bega kwa bega na nyinyi (nitakunusuruni). Basi yalipoona na majeshi mawili (na kukabiliana macho kwa macho), (shetani) alirudi nyuma na akasema: Mimi sipo pamoja nanyi. Mimi naona msiyoyaona. Mimi namuogopa Allah, na Allah ni mkali wa kuadhibu
سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ
Litashindwa kundi hilo na watakimbia