بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
(Walivyo tanabahi!): wakasema Bali sisi tumenyimwa (mavuno yake)!
Compartir :
قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ
Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Allah (kuiacha nia yenu mbaya)?
قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Wakasema: utukufu ni wa mola wetu, hakika tulikuwa wenye kudhulumu
فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ
Basi Wakakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana
قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ
Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka
عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ
Asaa Mola wetu akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi
كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ
Kama hivyo ndivyo inakuwa adhabu (ya hapa duniani), bila shaka adhabu ya akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!