فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَٰتٖ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Adamu akapokea maneno (ya toba) kutoka kwa Mola wake (akatubu) na (Allah) akamkubalia toba yake. Hakika yeye (Allah) ni Mwingi wa kupokea toba, Mwingi wa rehema
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَبَيَّنُواْ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَتُوبُ عَلَيۡهِمۡ وَأَنَا ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Isipokuwa waliotubu na wakare-kebisha na wakabainisha. Basi hao nitakubali tobayao, na mimi tu ndiye Mwingi wa kukubali toba, Mwingi wa kurehemu
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Isipokuwa (watakaoepuka laana ni) wale waliotubu baada ya hapo na wakafanya mema. Basi kwa hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno
أُوْلَـٰٓئِكَ جَزَآؤُهُم مَّغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَجَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَنِعۡمَ أَجۡرُ ٱلۡعَٰمِلِينَ
Hao malipo yao ni msamaha wa Mola wao Mlezi na bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, naujira bora kwawanaotenda (mema) ni huo
إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٖ فَأُوْلَـٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Hakika wanaomrudia Allah kwa toba ya kweli ni wale tu wanaofanya baya bila kujua kisha wanatubu muda mchache kabla ya kufa, basi Allah hao anawapokelea toba zao, na Allah ni Mjuzi saana mwenye Hekima
وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّي تُبۡتُ ٱلۡـَٰٔنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ كُفَّارٌۚ أُوْلَـٰٓئِكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا
Na haikubaliwi toba kwa wale ambao wanafanya mabaya hadi mmoja wao umauti umfike (ndipo) anasema: Mimi sasa nimetubu, na wala wale wanaokufa wakiwa makafiri. Hao tumewaandalia adhabu yenye maumivu makali mno
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا
Hakika, Allah hatoi msamaha (wa dhambi ya) kushirikishwa na anasamehe (dhambi) isiyokuwa hiyo kwa amtakaye. Na yeyote amshirikishaye Allah basi hakika amezua dhambi kubwa kabisa
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ إِذ ظَّلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ جَآءُوكَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡتَغۡفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُواْ ٱللَّهَ تَوَّابٗا رَّحِيمٗا
Na hatukumtuma Mtume yeyote ila tu atiiwe kwa idhini ya Allah. Na lau kama walipozidhulumu nafsi zao (kwa kutenda dhambi) wangelikujia wakamuomba msamaha Allah, na Mtume (naye) akawaombea msamaha, kwa yakini kabisa, wangemkuta Allah ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu
وَمَن يَعۡمَلۡ سُوٓءًا أَوۡ يَظۡلِمۡ نَفۡسَهُۥ ثُمَّ يَسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na yeyote mwenye kutenda baya au kudhulumu nafsi yake, kisha akamuomba msamaha Allah, atamkuta Allah ni Msamehevu sana, Mwenye kurehem
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Hakika, Allah hatoi msamaha (wa dhambi ya) kushirikishwa, na anasamehe (dhambi) zilizo chini ya hiyo kwa amtakaye. Na yeyote anayemfanyia ushirika Allah kwa hakika amepotea upotevu ulio mbali kabisa (na haki)
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Isipokuwa wale waliotubu (unafiki wao) na wakatengeneza (wakarekebisha na kusahihisha itikadi na misimamo yao mibovu) na wakashikamana na (sheri za) Allah na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Allah. Basi hao watakuwa pamoja na waumini. Na Allah atawapa waumini ujira mkubwa sana
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِن قَبۡلِ أَن تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهِمۡۖ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Isipokuwa wale waliotubu kabla hamjawatia nguvuni. Basi jueni kwamba, kwa hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu
فَمَن تَابَ مِنۢ بَعۡدِ ظُلۡمِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَتُوبُ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Basi mwenye kutubu baada ya kudhulumu kwake na akatengeneza (akarekebisha tabia zake), basi Allah hupokea toba yake. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu
وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِنَا فَقُلۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۖ كَتَبَ رَبُّكُمۡ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَ أَنَّهُۥ مَنۡ عَمِلَ مِنكُمۡ سُوٓءَۢا بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na watakapokujia wale wanao-ziamini Aya zetu sema (uwaambie): Amani iwe kwenu. Mola wenu mwenyewe rehema amejithibitishia kwamba, yeyote miongoni mwenu atakayefanya jambo ovu kwa kutojua, kisha baada yake akatubu na kurekebisha (tabia yake) basi hakika yeye (Allah) ni Msamehevu sana, Mwenye kurehemu
وَٱلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِهَا وَءَامَنُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na wale waliotenda maovu, kisha wakatubu baada yake na wakaamini, hakika Mola wako baada ya hayo ni Msamehevu sana, Rahimu sana
وَءَاخَرُونَ ٱعۡتَرَفُواْ بِذُنُوبِهِمۡ خَلَطُواْ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Na wapo wengine (miongoni mwa wakazi wa mji wa Madina waliohalifu kwenda jihadi) waliokiri dhambi zao; wamechanganya vitendo vyema na vingine viovu. Huwenda Allah akapokea Toba zao. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقۡبَلُ ٱلتَّوۡبَةَ عَنۡ عِبَادِهِۦ وَيَأۡخُذُ ٱلصَّدَقَٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Je, (waumini na wanaotubu) hawajui ya kwamba Allah (ndiye) anayekubali Toba za waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Allah tu ndiye Mwingi wa kupokea Toba, Rahimu sana?
لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِيِّ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ ٱلۡعُسۡرَةِ مِنۢ بَعۡدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٖ مِّنۡهُمۡ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّهُۥ بِهِمۡ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Kwa hakika kabisa, Allah alishamsamehe Nabii (baada ya kuwaruhusu waliotoa udhuru wa uongo wa kutokwenda kupigana Jihadi) na (aliwasamehe pia) Muhajirina na Answari waliomfuata Mtume katika kipindi kigumu, baada ya nyoyo za baadhi yao kukaribia kugeuka (kwa kutamani kuacha kwenda vitani katika kipindi cha joto kali na mazingira magumu), kisha (Allah) akapokea Toba zao. Hakika, Yeye kwao ni Mpole mno, Mwenye kurehemu
وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Na (pia Allah amekubali Toba ya wale watu) watatu walioachwa nyuma (waliokataa kwenda Jihadi kwa uvivu[1] ambao Mtume hakuikubali toba yao kwa wepesi na aliwawekea vikwazo) mpaka dunia walipoiona finyu kwao pamoja na upana wake, na nafsi zao zikadhikika na wakawa na yakini kuwa hakuna pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake Yeye tu. Kisha Allah aliwasamehe (baada ya kubainika ni waumini kweli aliwawezesha kujirudi) ili watubu. Hakika, Allah tu ndiye Mwenye kupokea sana Toba, Mwenye kurehemu
1- - Hawa ni Kaabi bin Malik, Hilal bin Umaya na Murara bin Rabii.
۞نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Wape habari waja wangu ya kwamba, Mimi ndiye Mwenye kusamehe sana, Mwenye kurehemu
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا فُتِنُواْ ثُمَّ جَٰهَدُواْ وَصَبَرُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Kisha hakika Mola wako mlezi, kwa wale waliohama baada ya kuteswa, kisha wakajitahidi na wakasubiri, bila shaka Mola wako mlezi baada ya hayo ni msamehevu sana, mwenye rehema
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ
Kisha hakika Mola wako mlezi kwa wale waliofanya ubaya (dhambi) kwa kutokujua, kisha wakatubu baada ya hayo na waka-tenda mema, hakika bila shaka Mola wako baada ya hayo ni mwingi wa kusamehe, mwenye rehema
وَإِنِّي لَغَفَّارٞ لِّمَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا ثُمَّ ٱهۡتَدَىٰ
Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Allah ni Msamehevu, Mwenye kurehemu
إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلٗا صَٰلِحٗا فَأُوْلَـٰٓئِكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمۡ حَسَنَٰتٖۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Isipokuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allah atayaba-dilisha maovu yao yawe mema. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu
وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَإِنَّهُۥ يَتُوبُ إِلَى ٱللَّهِ مَتَابٗا
Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Allah
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمۡتُ نَفۡسِي فَٱغۡفِرۡ لِي فَغَفَرَ لَهُۥٓۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu
فَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلۡمُفۡلِحِينَ
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufanikiwa
لِّيُعَذِّبَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ وَيَتُوبَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمَۢا
Kwa hivyo Allah anawaadhibu wanafiki wanaume, na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na anawapokelea toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu
وَهُوَ ٱلَّذِي يَقۡبَلُ ٱلتَّوۡبَةَ عَنۡ عِبَادِهِۦ وَيَعۡفُواْ عَنِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ وَيَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ
Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua mnayo yatenda