Uzinduzi wa Quran ya Al-Noor

2025-11-10

Tunamshukuru Allah… Kazi ya kuutafsiri “Msahafu wa Nuur” Imekamilika kwa lugha 10 za ulimwenguni, katika kutafsiri maana za Qur’an Tukufu.

Kazi hii ya “Msahafu wa Nuur” ni utekelezaji wa hali ya juu katika kuitafsiri Qur’an kwa kukusanya mambo mengi. Miongoni mwa hayo ni:

- Kutafsiri maana ya Qur’an Tukufu kwa lugha 10 ambazo ni: Kingereza, Kifaransa, Kihispania, Kilatini, Kijerumani, Kireno, Kibrazil, Kifursi, Kihausa na Kiswahili.

- Kutoa miongozo ya utumiaji wake kwa lugha 11 za ulimwengu.

- Kuhusisha usomaji wa Aya kwa sauti za lugha zote kwa ukamilifu.

- Uwezekano wa kufanya utafiti katika Aya za Qur’an na tafsiri zake.

- Mpangilio mzuri wa kuhama kati ya Msahafu wa Kiarabu na Msahafu ulio tafsiriwa.

- Kusikiliza Aya kwa usomaji mzuri wa sauti za Wasomaji wabobezi wa Qur’an.

- Kuwepo kwa Maktaba ya Qur’an iliyo kusanya Lugha 10 za ulimwenguni.

- Kuwepo wepesi wa mpangilio kati ya sura na kurasa.

- Ushirikiano wa Aya, tafsiri na ufafanuzi kupitia mitandao ya kijamii iliyopo ulimwenguni.

- Tafsiri yake kukusanywa na Wanazuoni wakubwa wa Tafsiri za Qur’an.

 Upatikanaji wake kupitia tovuti ifuatayo:
https://noor.gallery/download/