هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ
Je, imekufikia habari ya msiba wa kufudikiza (ugongao moyo)?
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ
Siku hiyo nyuso zitainama,
عَامِلَةٞ نَّاصِبَةٞ
Zikifanya kazi, nazo taabani
تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةٗ
Ziingie katika Moto unao waka
تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٖ
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka
لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٖ
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba
لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٖ
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاعِمَةٞ
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu
لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٞ
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Katika Bustani ya juu
لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةٗ
Hawatasikia humo upuuzi. Humo imo chemchem inayo miminika
فِيهَا عَيۡنٞ جَارِيَةٞ
Humo imo chemchem inayo miminika
فِيهَا سُرُرٞ مَّرۡفُوعَةٞ
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
وَأَكۡوَابٞ مَّوۡضُوعَةٞ
Na bilauri zilizo pangwa,
وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةٞ
Na matakia (yakiwa) safu safu,
وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ
Na mazulia yaliyo tandikwa
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa (simamishwa)?
وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٞ
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji
لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ
Wewe si mwenye kuwatawalia
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ
Lakini anaye rudi nyuma na kukufuru,
فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ
Basi Allah Atamuadhibu adhabu kubwa kabisa
إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao
ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hesabu yao!