Sure: ALJINN 

Vers : 1

قُلۡ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ ٱسۡتَمَعَ نَفَرٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَقَالُوٓاْ إِنَّا سَمِعۡنَا قُرۡءَانًا عَجَبٗا

Sema: Nimefunuliwa Wahyi kwamba, kundi miongoni mwa majini lilisikiliza (Qur’ani) likasema: Hakika sisi tumeisikia Qurani ya ajabu sana



Sure: ALJINN 

Vers : 2

يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلرُّشۡدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦۖ وَلَن نُّشۡرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدٗا

Inaongoza kwenye uongofu, kwa hivyo tumeiamini, na wala hatutamshirikisha yeyote kwa Mola wetu Mlezi



Sure: ALJINN 

Vers : 3

وَأَنَّهُۥ تَعَٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَٰحِبَةٗ وَلَا وَلَدٗا

Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa; Hakujifanyia Mke wala Mtoto (hana mke wala mwana)



Sure: ALJINN 

Vers : 4

وَأَنَّهُۥ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطٗا

Na kwa hakika hali ilivyo, wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema juu ya Allah uongo uliopindukia mipaka



Sure: ALJINN 

Vers : 5

وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن تَقُولَ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا

Na kwamba sisi tulidhania wanadamu na majini hawatosema uongo juu ya Allaah, (hawatomzulia uongo Allah)



Sure: ALJINN 

Vers : 6

وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٞ مِّنَ ٱلۡإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٖ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقٗا

Na kwamba wanaume miongoni mwa wanadamu walikuwa wanajikinga kwa wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia wao madhambi, (uvukaji mipaka ya kuasi na khofu)



Sure: ALJINN 

Vers : 7

وَأَنَّهُمۡ ظَنُّواْ كَمَا ظَنَنتُمۡ أَن لَّن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ أَحَدٗا

Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Allah hatamleta Mtume yeyote. (au Hatomfufua yeyote yule)



Sure: ALJINN 

Vers : 8

وَأَنَّا لَمَسۡنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدۡنَٰهَا مُلِئَتۡ حَرَسٗا شَدِيدٗا وَشُهُبٗا

Nasi tulizigusa mbingu, (au tulitafuta kuzifikia mbingu) na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo



Sure: ALJINN 

Vers : 9

وَأَنَّا كُنَّا نَقۡعُدُ مِنۡهَا مَقَٰعِدَ لِلسَّمۡعِۖ فَمَن يَسۡتَمِعِ ٱلۡأٓنَ يَجِدۡ لَهُۥ شِهَابٗا رَّصَدٗا

Na hakika sisi tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini anaetaka kusikiliza hivi sasa atakuta kimondo kinamvizia!



Sure: ALJINN 

Vers : 10

وَأَنَّا لَا نَدۡرِيٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ أَرَادَ بِهِمۡ رَبُّهُمۡ رَشَدٗا

Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uongofu



Sure: ALJINN 

Vers : 11

وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا

Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali



Sure: ALJINN 

Vers : 12

وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعۡجِزَ ٱللَّهَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَن نُّعۡجِزَهُۥ هَرَبٗا

Nasi tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allah ardhini, na wala hatutoweza kumponyoka Allah kwa kukimbia



Sure: ALJINN 

Vers : 13

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعۡنَا ٱلۡهُدَىٰٓ ءَامَنَّا بِهِۦۖ فَمَن يُؤۡمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا يَخَافُ بَخۡسٗا وَلَا رَهَقٗا

Nasi tulipo usikia uongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa



Sure: ALJINN 

Vers : 14

وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا

Na hakika sisi miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu wapo wakengeukaji; (wanao acha haki). Hivyo atakaye silimu, hao ndio waliofuata uongofu



Sure: ALJINN 

Vers : 15

وَأَمَّا ٱلۡقَٰسِطُونَ فَكَانُواْ لِجَهَنَّمَ حَطَبٗا

Na ama wanaoacha haki, hao watakuwa kuni za Moto wa Jahannamu



Sure: ALJINN 

Vers : 16

وَأَلَّوِ ٱسۡتَقَٰمُواْ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسۡقَيۡنَٰهُم مَّآءً غَدَقٗا

(Allah Anasema): Kwamba lau wangelinyooka na wakasimama sawasawa kwenye njia, bila shaka Tungeli wanywesha maji kwa wingi



Sure: ALJINN 

Vers : 17

لِّنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَمَن يُعۡرِضۡ عَن ذِكۡرِ رَبِّهِۦ يَسۡلُكۡهُ عَذَابٗا صَعَدٗا

Ili tuwatie katika majaribio kwayo. Na anayepuuza Ukumbusho wa Mola wake, Atamsukuma kwenye adhabu ngumu



Sure: ALJINN 

Vers : 18

وَأَنَّ ٱلۡمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدۡعُواْ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدٗا

Na hakika misikiti ni ya Allah, basi msimuabudu yeyote pamoja na Allah



Sure: ALJINN 

Vers : 19

وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبۡدُ ٱللَّهِ يَدۡعُوهُ كَادُواْ يَكُونُونَ عَلَيۡهِ لِبَدٗا

Na hakika Mja wa Allah Nabii Muhammad rehma na amani ziwe juu yake alipo simama kumuomba (na kumuabudu), wao walikaribia kumzonga.!



Sure: ALJINN 

Vers : 20

قُلۡ إِنَّمَآ أَدۡعُواْ رَبِّي وَلَآ أُشۡرِكُ بِهِۦٓ أَحَدٗا

Sema: Ewe Muhammad: Hakika mimi namuomba (na kumuabudu) Mola wangu na wala simshirikishi na yeyote



Sure: ALJINN 

Vers : 21

قُلۡ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا رَشَدٗا

Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni



Sure: ALJINN 

Vers : 22

قُلۡ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٞ وَلَنۡ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدًا

Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia



Sure: ALJINN 

Vers : 23

إِلَّا بَلَٰغٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَٰلَٰتِهِۦۚ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا

Isipokuwa nifikishe Ujumbe utokao kwa Allah, na ujumbe wake. Na wenye kumuasi Allah na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele



Sure: ALJINN 

Vers : 24

حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ أَضۡعَفُ نَاصِرٗا وَأَقَلُّ عَدَدٗا

Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi



Sure: ALJINN 

Vers : 25

قُلۡ إِنۡ أَدۡرِيٓ أَقَرِيبٞ مَّا تُوعَدُونَ أَمۡ يَجۡعَلُ لَهُۥ رَبِّيٓ أَمَدًا

Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu atayawekea muda mrefu



Sure: ALJINN 

Vers : 26

عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ فَلَا يُظۡهِرُ عَلَىٰ غَيۡبِهِۦٓ أَحَدًا

Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake



Sure: ALJINN 

Vers : 27

إِلَّا مَنِ ٱرۡتَضَىٰ مِن رَّسُولٖ فَإِنَّهُۥ يَسۡلُكُ مِنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ رَصَدٗا

Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake



Sure: ALJINN 

Vers : 28

لِّيَعۡلَمَ أَن قَدۡ أَبۡلَغُواْ رِسَٰلَٰتِ رَبِّهِمۡ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيۡهِمۡ وَأَحۡصَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ عَدَدَۢا

Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote waliyo nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu