Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 1

إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ قَالُواْ نَشۡهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُۥ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَكَٰذِبُونَ

Watakapokujia wanafiki wanasema: Tunashuhudia kwamba wewe bila ya shaka yoyote ni Mtume wa Allah. Na Allah Anajua kuwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Allah anashuhudia kuwa kwa hakika kabisa wanafiki ni waongo



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 2

ٱتَّخَذُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ جُنَّةٗ فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wamefanya viapo vyao ni ngao, hivyo wakazuia (watu wasiifuate) njia ya Allah. Hakika, ni uovu mno waliokuwa wakiufanya



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 3

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ

Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa (chapa) ya muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 4

۞وَإِذَا رَأَيۡتَهُمۡ تُعۡجِبُكَ أَجۡسَامُهُمۡۖ وَإِن يَقُولُواْ تَسۡمَعۡ لِقَوۡلِهِمۡۖ كَأَنَّهُمۡ خُشُبٞ مُّسَنَّدَةٞۖ يَحۡسَبُونَ كُلَّ صَيۡحَةٍ عَلَيۡهِمۡۚ هُمُ ٱلۡعَدُوُّ فَٱحۡذَرۡهُمۡۚ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۖ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ

Na ukiwaona miili yao inakupendeza kwa uzuri wao, na wakizungumza unavutika kuwasikiliza kwa utamu wa maneno. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa (hayana uhai wowote wa Imani). Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Allah awaangamizie mbali! Namna gani wanavyoghilibiwa (na kuiacha haki)?



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 5

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Allah akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 6

سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ أَسۡتَغۡفَرۡتَ لَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ لَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allah Haongoi watu mafasiki



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 7

هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُواْ عَلَىٰ مَنۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّواْۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَفۡقَهُونَ

Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Allah mpaka waondokelee mbali. Na ni za Allah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 8

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema: Tutakaporudi Madinah, mwenye hadhi zaidi atamfukuza humo aliye dhalili. Na hali utukufu ni wa Allah na wa Mtume Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 9

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Enyi mlio amini! Yasikusa-haulisheni mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Allah. Na wenye kufanya hayo ndio walio pata khasara



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 10

وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Ee Mola wangu! Naomba uniachilie angalau muda kidogo tu, ili nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?



Sure: ALMUNAAFIQUUN 

Vers : 11

وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَاۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Wala Allah hatoichelewesha nafsi yoyote ile (muda wake wa kufa) pale inapo fika ajali yake; na Allah anazo khabari za mnayo yatenda