وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ
Nina apa kwa nyota zinapozama
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ
Hakupotoka swahibu wenu na wala hakupotoka
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ
Na hasemi (neno lolote lile) kwa utashi wa nafsi (yake)
إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ
Hayakuwa hayo (anayaoyasema) isipokuwa tu ni Wahy unaofunuliwa
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ
Amemfundisha (Malaika Jibrili) Mwenye nguvu kubwa
ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ
Mwenye nguvu na hekima na akakaa katika umbile lake halisi
وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Naye yuko juu kabisa katika upeo wa macho
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
Kisha akakurubia na akashuka
فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ
Kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi
فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ
(Allah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy
مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ
Moyo (wake) haukukadhibisha yale aliyoyaona
أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?
وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ
Na hakika alimuona (Jibriyl) kwa mara nyingine
عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ
Karibu yake kuna Jannatu Al-Ma-waa
إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ
Ulipoufunika mkunazi huo hicho kilicho ufinika
مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Jicho lake halikukengeuka wala halikupindukia mipaka
لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ
Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Bwana wake kubwa kabisa
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّـٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ
Je, mmeona (masanamu) Laata na ‘Uzzaa?
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ
Na Manaata mwengine wa tatu?
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ
Je, nyinyi mna wana wa kiume Naye Ana wana wa kike?
تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ
Huo basi ni mgao wa dhulma!
إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ
Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali imekwishawajia kutoka kwa Bwana wao mwongozo
أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
Kwani kila Mtu anapata kila anayoyatamani?
فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ
Na Allah ndiye mmiliki wa Akhera na Dunia
۞وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ
Na kuna malaika wengi mbinguni hainufaishi chochote uombezi wao ila baada ya kupewa idhini na Allah kwa amtakaye na amridhie
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ
Hakika wale wasioamini Aakhirah bila shaka wanawaita Malaika kwa majina ya kike
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا
Na wala hawana ujuzi wowote ule wa hayo; hawafuati isipokuwa dhana, na hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki
فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Basi achana naye ambaye ameupa mgongo ukumbusho Wetu na wala hataki isipokuwa maisha ya dunia
ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Huo ndio upeo wao wa elimu. Hakika Bwana wako ni Mjuzi zaidi wa ambaye amepotoka njia Yake, Naye Mjuzi zaidi wa ambaye ameongoka