Sure: YUSUF 

Vers : 1

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Alif Laam Raa[1]. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha


1- - Allah ndiye ajuaye zaidi maana ya herufi mkato hizi.


Sure: YUSUF 

Vers : 2

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika, sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu ili mpate kuelewa



Sure: YUSUF 

Vers : 3

نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa (huu) Wahyi tuliokufunulia wa hii Qur’ani, na ingawa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua



Sure: YUSUF 

Vers : 4

إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ

(Kumbuka) Wakati Yusuf alipomwambia baba yake (Yakubu kwamba): Ewe Baba yangu, hakika mimi niliona (usingizini) nyota kumi na moja na jua na mwezi; nimeziona zikinisujudia



Sure: YUSUF 

Vers : 5

قَالَ يَٰبُنَيَّ لَا تَقۡصُصۡ رُءۡيَاكَ عَلَىٰٓ إِخۡوَتِكَ فَيَكِيدُواْ لَكَ كَيۡدًاۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

(Yakubu) Alisema: Ewe kijana wangu, usiwasimulie ndugu zako ndoto yako, wasije wakakufanyia hila (husuda). Hakika, shetani kwa mwanadamu ni adui wa wazi



Sure: YUSUF 

Vers : 6

وَكَذَٰلِكَ يَجۡتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعۡقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيۡكَ مِن قَبۡلُ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Na kama hivyo anakuteua Mola wako Mlezi na akakufundisha tafsiri za matukio (ndoto) na anatimiza neema zake kwako na kwa familia ya Yakubu, kama alivyozitimizia (neema hizo) kwa Baba zako wawili hapo kabla; Ibrahimu na Is-haka[1]. Hakika, Mola wako Mlezi ni Mjuzi, Mwenye hekima


1- - Hawa ni mababu wa Nabii Yusuf. Katika lugha ya Qur’ani babu anahisabika ni baba.


Sure: YUSUF 

Vers : 7

۞لَّقَدۡ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخۡوَتِهِۦٓ ءَايَٰتٞ لِّلسَّآئِلِينَ

Kwa yakini kabisa, katika (kisa cha) Yusuf na ndugu zake zipo ishara (nyingi) kwa wanaouliza



Sure: YUSUF 

Vers : 8

إِذۡ قَالُواْ لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰٓ أَبِينَا مِنَّا وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ

(Kumbukeni) Wakati (ndugu wa Yusuf) waliposema: Kwa hakika kabisa, Yusuf na nduguye (wa mama mmoja) wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, na ilihali sisi ni wengi. Hakika, Baba yetu yumo kwenye upotevu ulio wazi (anafanya kosa la wazi)



Sure: YUSUF 

Vers : 9

ٱقۡتُلُواْ يُوسُفَ أَوِ ٱطۡرَحُوهُ أَرۡضٗا يَخۡلُ لَكُمۡ وَجۡهُ أَبِيكُمۡ وَتَكُونُواْ مِنۢ بَعۡدِهِۦ قَوۡمٗا صَٰلِحِينَ

(Ndugu wa Yusuf walisema): Muueni Yusuf au mtupeni ardhi (ya mbali) ili uso (na upendo) wa Baba yenu utakuelekeeni nyinyi tena baada yake (baada ya kumuua Yusuf mtatubu dhambi hiyo na) mtakuwa watu wema



Sure: YUSUF 

Vers : 10

قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ لَا تَقۡتُلُواْ يُوسُفَ وَأَلۡقُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّ يَلۡتَقِطۡهُ بَعۡضُ ٱلسَّيَّارَةِ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ

Alisema msemaji kati yao: Msimuue Yusuf (lakini) mtupeni kwenye kina cha kisima (kirefu) ataokotwa na baadhi ya wasafiri kama nyinyi mna azma ya kufanya (jambo la kumtenganisha na baba yake)



Sure: YUSUF 

Vers : 11

قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأۡمَ۬نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَٰصِحُونَ

(Nduguze baada ya kuafikiana) Walisema: Ewe Baba yetu, una nini hata hutuamini kwa Yusuf na ilihali sisi, kwa hakika, ni wenye kumtakia mema?



Sure: YUSUF 

Vers : 12

أَرۡسِلۡهُ مَعَنَا غَدٗا يَرۡتَعۡ وَيَلۡعَبۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Mruhusu kesho (atoke) pamoja nasi (kwenda malishoni) atakula na kucheza kwa furaha, nakwa yakini kabisa, sisi tutamlinda



Sure: YUSUF 

Vers : 13

قَالَ إِنِّي لَيَحۡزُنُنِيٓ أَن تَذۡهَبُواْ بِهِۦ وَأَخَافُ أَن يَأۡكُلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَأَنتُمۡ عَنۡهُ غَٰفِلُونَ

(Yakubu) Alisema: Kwa hakika kabisa, inanihuzunisha nyinyi kwenda naye (na kuniacha peke yangu) na nachelea asije akaliwa na mbwa mwitu ilihali nyinyi mkiwa mmeghafilika



Sure: YUSUF 

Vers : 14

قَالُواْ لَئِنۡ أَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّآ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ

Walisema (kumwambia Baba yao): Iwapo ataliwa na mbwa mwitu na ilihali sisi ni wengi (kundi lenye nguvu), bila ya shaka sisi wakati huo tutakuwa hasarani (hatuna faida)



Sure: YUSUF 

Vers : 15

فَلَمَّا ذَهَبُواْ بِهِۦ وَأَجۡمَعُوٓاْ أَن يَجۡعَلُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمۡرِهِمۡ هَٰذَا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Basi walipokwenda naye na kukubaliana kumtumbukiza (kumtosa) katika kina cha kisima kirefu, na tulimfunulia Wahyi Yusuf (hapo kisimani kwamba): Hapana shaka yoyote utakuja kuwaambia (siku za usoni) kuhusu jambo lao hili, na wala wao hawatahisi (kama wewe ni Yusuf)



Sure: YUSUF 

Vers : 16

وَجَآءُوٓ أَبَاهُمۡ عِشَآءٗ يَبۡكُونَ

Walimjia Baba yao (wakati wa) usiku huku wakiangua kilio (cha uongo)



Sure: YUSUF 

Vers : 17

قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبۡنَا نَسۡتَبِقُ وَتَرَكۡنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤۡمِنٖ لَّنَا وَلَوۡ كُنَّا صَٰدِقِينَ

Walisema: Ewe Baba yetu, hakika sisi tulikwenda kushindana na tulimuacha Yusuf kwenye vitu vyetu, basi akaliwa na mbwa mwitu (lakini wewe hutatuamini na hata kama tunasema kweli



Sure: YUSUF 

Vers : 18

وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٖ كَذِبٖۚ قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٞۖ وَٱللَّهُ ٱلۡمُسۡتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ

Walikuja na kanzu yake huku ikiwa na damu ya uongo. (Yakubu alipobaini geresha yao) (Yakubu) Alisema: “Bali nafsi zenu zimekushawishini (kutenda) jambo (baya). Basi subira ni jambo zuri, na Allah ndiye wa kuombwa msaada kwa huu (uongo) mnaoueleza”



Sure: YUSUF 

Vers : 19

وَجَآءَتۡ سَيَّارَةٞ فَأَرۡسَلُواْ وَارِدَهُمۡ فَأَدۡلَىٰ دَلۡوَهُۥۖ قَالَ يَٰبُشۡرَىٰ هَٰذَا غُلَٰمٞۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَٰعَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Na uliwasili msafara, na ukamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake (ili kuchota maji). Alisema: Furaha iliyoje! Huyu hapa mvulana! Na walimficha akiwa (kama) bidhaa. Na Allah ni Mjuzi wa wanayoyatenda



Sure: YUSUF 

Vers : 20

وَشَرَوۡهُ بِثَمَنِۭ بَخۡسٖ دَرَٰهِمَ مَعۡدُودَةٖ وَكَانُواْ فِيهِ مِنَ ٱلزَّـٰهِدِينَ

Na (wale wasafiri) walimuuza (Yusuf) kwa thamani duni; pesa chache. Na hawakuwa na haja naye



Sure: YUSUF 

Vers : 21

وَقَالَ ٱلَّذِي ٱشۡتَرَىٰهُ مِن مِّصۡرَ لِٱمۡرَأَتِهِۦٓ أَكۡرِمِي مَثۡوَىٰهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗاۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلِنُعَلِّمَهُۥ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ وَٱللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِۦ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na alisema yule aliyemnunua huko Misri kumwambia mkewe: Muandalie (huyu kijana) makazi yake mazuri, (kwasababu) huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu. Na kama hivyo (tulivyo mnusuru Yusuf na mauaji) tulimpa (madaraka) katika nchi (ya Misri) na ili tumfundishe kutafasiri matukio (ndoto). Na Allah ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui



Sure: YUSUF 

Vers : 22

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُۥٓ ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na (Yusuf) alipofikia umri wa utu uzima tulimpa hukumu (Utume na utawala) na elimu. Na (malipo) kama haya tunawalipa wanaotenda mazuri (yanayo mpendeza Allah)



Sure: YUSUF 

Vers : 23

وَرَٰوَدَتۡهُ ٱلَّتِي هُوَ فِي بَيۡتِهَا عَن نَّفۡسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلۡأَبۡوَٰبَ وَقَالَتۡ هَيۡتَ لَكَۚ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ رَبِّيٓ أَحۡسَنَ مَثۡوَايَۖ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na yule (mke wa mfalme) ambaye yeye (Yusuf) alikuwa nyumbani kwake alimtongoza (Yusuf) bila ya ridhaa yake, na alifunga milango barabara na akamwambia: Njoo, niko tayari kwa ajili yako! (Yusuf) Alisema: “Audhubillahi[1]. Kwa hakika, huyu (mwenye nyumba) ni mlezi wangu, ameyafanya mazuri mno makazi yangu. Hakika ilivyo ni kwamba, madhalimu hawafaulu”


1- - Ninaomba kinga kwa Allah.


Sure: YUSUF 

Vers : 24

وَلَقَدۡ هَمَّتۡ بِهِۦۖ وَهَمَّ بِهَا لَوۡلَآ أَن رَّءَا بُرۡهَٰنَ رَبِّهِۦۚ كَذَٰلِكَ لِنَصۡرِفَ عَنۡهُ ٱلسُّوٓءَ وَٱلۡفَحۡشَآءَۚ إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُخۡلَصِينَ

Na kwa hakika kabisa (yule mke wa mfalme) alimkusudia (kutaka kufanya naye uchafu, na Yusuf naye) alikusudia (baada ya kuvutiwa na hisia za kibinadamu). Lau kama sio kwamba (Yusuf) aliona ishara za Mola wake Mlezi (angetumbukia katika kufanya machafu. Lakini Allah alimzindua na akakataa kufanya uchafu). Kama hivyo (tumefanya) ili tumuepushe (Yusuf) na uovu na uchafu. Hakika, yeye (Yusuf) alikuwa miongoni mwa waja wetu waliosafishwa



Sure: YUSUF 

Vers : 25

وَٱسۡتَبَقَا ٱلۡبَابَ وَقَدَّتۡ قَمِيصَهُۥ مِن دُبُرٖ وَأَلۡفَيَا سَيِّدَهَا لَدَا ٱلۡبَابِۚ قَالَتۡ مَا جَزَآءُ مَنۡ أَرَادَ بِأَهۡلِكَ سُوٓءًا إِلَّآ أَن يُسۡجَنَ أَوۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na wawili (hao) walikimbizana kuelekea mlangoni (baada ya Yusuf kukataa), na (mwanamke) akaikwida kanzu ya Yusuf kwa nyuma (kwa kumdhibiti asikimbie). Na (ghafla) wakamkuta bwana wake (mumewe) mlangoni. (Mwanamke) Alisema: Hakuna malipo ya anayetaka kumfanyia uovu mkeo isipokuwa tu kufungwa au kupewa adhabu inayoumiza



Sure: YUSUF 

Vers : 26

قَالَ هِيَ رَٰوَدَتۡنِي عَن نَّفۡسِيۚ وَشَهِدَ شَاهِدٞ مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن قُبُلٖ فَصَدَقَتۡ وَهُوَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

(Yusuf) Alisema (kwa kujitetea): Yeye ndiye aliyenitongoza bila ya ridhaa yangu. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake (Yusuf) imechanwa kwa mbele basi mwanamke amesema kweli, naye (Yusuf) ni miongoni mwa waongo



Sure: YUSUF 

Vers : 27

وَإِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٖ فَكَذَبَتۡ وَهُوَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Na ikiwa kanzu yake imechanwa (kwa) nyuma, basi mwanamke amesema uongo na yeye (Yusuf) ni miongoni mwa wakweli



Sure: YUSUF 

Vers : 28

فَلَمَّا رَءَا قَمِيصَهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٖ قَالَ إِنَّهُۥ مِن كَيۡدِكُنَّۖ إِنَّ كَيۡدَكُنَّ عَظِيمٞ

Basi (yule bwana) alipoona kanzu yake (Yusuf) imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika hivi ni katika vitimbi vyenu (wanawake). Kwa hakika, vitimbi vyenu ni vikubwa mno



Sure: YUSUF 

Vers : 29

يُوسُفُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَاۚ وَٱسۡتَغۡفِرِي لِذَنۢبِكِۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ ٱلۡخَاطِـِٔينَ

(Yule bwana alimwambia Yusuf kuwa: Ewe) Yusuf, lipuuze hili (na usiwasimulie watu). Na (wewe mwanamke): Omba msamaha kwa dhambi yako, (kwasababu) hakika wewe ni miongoni mwa waliofanya makosa



Sure: YUSUF 

Vers : 30

۞وَقَالَ نِسۡوَةٞ فِي ٱلۡمَدِينَةِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ تُرَٰوِدُ فَتَىٰهَا عَن نَّفۡسِهِۦۖ قَدۡ شَغَفَهَا حُبًّاۖ إِنَّا لَنَرَىٰهَا فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Na (kundi la) wanawake wa mjini walisema: (Hivi) Mke wa Mheshimiwa anamtongoza kijana wake bila ya ridhaa yake, hakika (Yusuf) amepasua moyo wake (mke wa mheshimiwa) kwa mapenzi?Hakika, sisi tunamuona (kwa kitendo hiki) kwa yakini kabisa yupo katika upotevu ulio dhahiri kabisa