الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Alif, laam, raa (hizi ni herufi za mkato na Allah ndiye anayejua maana yake). Hiki ni kitabu (ambacho) zimetengenezwa vyema Aya zake kisha zimefafanuliwa kutoka kwa aliye na Hekima, Mwenye habari nyingi
أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ
(Kwamba) Msiabudu chochote ispokuwa Allah tu. Hakika mimi ninatoka kwake (nikiwa) Muonyaji na Mwenye kutoa habari njema
وَأَنِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُمَتِّعۡكُم مَّتَٰعًا حَسَنًا إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى وَيُؤۡتِ كُلَّ ذِي فَضۡلٖ فَضۡلَهُۥۖ وَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ كَبِيرٍ
Na muombeni msamaha Mola wenu Mlezi kisha rejeeni kwake atawastarehesheni starehe nzuri mpaka muda uliotajwa, na atampa kila mwenye fadhila fadhila zake na kama watakengeuka kwa hakika mimi ninaogopea kwenu (kupata) adhabu ya Siku kubwa
إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Kwa Allah tu ndio marejeo yenu na Yeye kwa kila kitu ni Muweza
أَلَآ إِنَّهُمۡ يَثۡنُونَ صُدُورَهُمۡ لِيَسۡتَخۡفُواْ مِنۡهُۚ أَلَا حِينَ يَسۡتَغۡشُونَ ثِيَابَهُمۡ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Ehee!Kwa hakika wao wanaficha vifuani mwao (ukafiri,) ili wajifiche kwake. Ehee!Wakati wanajifunika nguo zao (wasionekane) kwamba Allah anajua yote wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha kwa hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani
۞وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ رِزۡقُهَا وَيَعۡلَمُ مُسۡتَقَرَّهَا وَمُسۡتَوۡدَعَهَاۚ كُلّٞ فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ
Na hakuna chochote kitem-beacho ardhini ispokuwa rizki yake ni kwa Allah pekee, na anayajua makazi yake (hapa duniani na baada ya kufa kwake) na sehemu atakapokufa. Hayo yote yapo katika kitabu kinacho bainisha
وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَكَانَ عَرۡشُهُۥ عَلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۗ وَلَئِن قُلۡتَ إِنَّكُم مَّبۡعُوثُونَ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡمَوۡتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na ni Yeye ambaye ameziumba mbingu na ardhi katika siku sita, na Arshi yake ilikuwa juu ya maji (kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi), ili awatahini (ajue) ni nani miongoni mwenu aliye mzuri sana wa matendo. Na endapo utawaambia: Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa, watasema wale waliokufuru: Hii Qur’ani sichochote ispokuwa ni uchawi tu ulio wazi
وَلَئِنۡ أَخَّرۡنَا عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٖ مَّعۡدُودَةٖ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحۡبِسُهُۥٓۗ أَلَا يَوۡمَ يَأۡتِيهِمۡ لَيۡسَ مَصۡرُوفًا عَنۡهُمۡ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na kwa hakika endapo tutawa-cheleweshea adhabu mpaka muda (maalumu) uliohesabiwa, kwa yakini watasema ni kipi kinachoifunga adhabu hiyo (kama ni kweli ipo)? Ehee siku itakapowajia haitawakosa wao na yatawazunguka yale waliyokuwa wanayafanyia mzaha
وَلَئِنۡ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ ثُمَّ نَزَعۡنَٰهَا مِنۡهُ إِنَّهُۥ لَيَـُٔوسٞ كَفُورٞ
Na kama mwanadamu tutam-uonjesha kutoka kwetu rehema yoyote kisha tukaiondoa kwake rehema hiyo, kwa hakika yeye hukata tamaa akakufuru
وَلَئِنۡ أَذَقۡنَٰهُ نَعۡمَآءَ بَعۡدَ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ ٱلسَّيِّـَٔاتُ عَنِّيٓۚ إِنَّهُۥ لَفَرِحٞ فَخُورٌ
Na iwapo tutamuonjesha neema nyingi baada ya madhara (matatizo) yaliyompata, kwa hakika atasema yameniondokea matatizo, kwa hakika yeye anakuwa mwenye furaha sana mwenye kujigamba mno
إِلَّا ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٞ كَبِيرٞ
Isipokuwa tu wale walio subiri na wakatenda mema, hao wanamsamaha (kutoka kwa Mola wao mlezi) na wanamalipo makubwa
فَلَعَلَّكَ تَارِكُۢ بَعۡضَ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَضَآئِقُۢ بِهِۦ صَدۡرُكَ أَن يَقُولُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ كَنزٌ أَوۡ جَآءَ مَعَهُۥ مَلَكٌۚ إِنَّمَآ أَنتَ نَذِيرٞۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٌ
Huenda wewe ni mwenye kuacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kinabana wanaposema kuwa: Kwanini asingeteremshiwa hazina au angekuja Malaika pamoja naye? Hakika sivingine wewe ni muhofishaji tu na Allah ni msimamizi wa kila kitu
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِعَشۡرِ سُوَرٖ مِّثۡلِهِۦ مُفۡتَرَيَٰتٖ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Au wanasema hii Qur’ani ameizua? Sema: Leteni Sura kumi zilizozushwa mfano wake na muiteni mtakayeweza (kumuita) badala ya Allah kama mkiwa wa kweli (katika madai yenu)
فَإِلَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلۡمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ
Na kama hawakukujibuni hilo basi juweni kwamba, sivinginevyo (Qur’ani imeteremshwa kwa elimu ya Allah na hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye tu je nyinyi mmesilimu?
مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيۡهِمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فِيهَا وَهُمۡ فِيهَا لَا يُبۡخَسُونَ
Wale wanaotaka (katika matendo yao wanayofanya wapate) maisha ya kidunia na mapambo yake (kama dhahabu, fedha, watoto nafasi, wanawake nk), tutawalipa (thawabu hizo) kikamilifu hapa duniani na hawatapunguziwa chochote
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَيۡسَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا ٱلنَّارُۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hao ndio wale ambao Akhera hawana chochote isipokuwa Moto tu, na yataharibika matendo yao yote na ni batili yote waliyokuwa wakiyatenda
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتۡلُوهُ شَاهِدٞ مِّنۡهُ وَمِن قَبۡلِهِۦ كِتَٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامٗا وَرَحۡمَةًۚ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ مِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ فَٱلنَّارُ مَوۡعِدُهُۥۚ فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّنۡهُۚ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ
Hivi yule aliye na hoja kutoka kwa Mola wake mlezi na akaifuata (hoja hiyo) shahidi kutoka kwake (Jibrili) na kabla yake palikuwepo kitabu (cha taurati kilichoteremshwa kwa Nabii) Musa juu yake amani, kikiwa ni kiongozi na rehema, hao wanaiamini Qur ani, na yeyote anaeikufuru miongoni mwa makundi, basi Moto ni mahali pake alipoahidiwa, basi usiwe katika shaka yoyote, hii Qur’ani ni haki kutoka kwa bwana wako, lakini watu wengi hawaamini
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ يُعۡرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمۡ وَيَقُولُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ أَلَا لَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ni nani aliye dhalimu zaidi (katika kuzua) kuliko yule aliyemzulia Allah uongo? Hao watahudhurishwa kwa Mola wao mlezi na mashahidi watasema: Hawa ndiyo wale waliyomzulia uongo Mola wao mlezi, ehee laana ya Allah iwe kwa Madhalimu
ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ
(Madhalimu) ambao wanawazuia watu (kuifuata) njia ya Allah na wanaitaka njia iende kombo (iwe sawa na matamanio yao) ilhali wao Akhera wanaikataa
أُوْلَـٰٓئِكَ لَمۡ يَكُونُواْ مُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَۘ يُضَٰعَفُ لَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ مَا كَانُواْ يَسۡتَطِيعُونَ ٱلسَّمۡعَ وَمَا كَانُواْ يُبۡصِرُونَ
Hao hawakuwa wenye kushin-dikana katika ardhi na hawakuwa na wakuwanusuru badala ya Allah, adhabu itazidishwa kwa watu hao, hawakuwa wanaweza kusikia (Qur’ani) na hawakuwa wanaona (miujiza na kunufaika nayo)
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Hao ndio ambao wamezitia hasara nafsi zao na yamewapotea yote waliyokuwa wanayazua
لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡأَخۡسَرُونَ
Ni hakika kwamba wao Akhera, ndiyo wenye hasara kubwa sana
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَأَخۡبَتُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakanyenyekea kwa Mola wao mlezi, hao ni watu wa Peponi wao humo wataishi milele
۞مَثَلُ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ كَٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡأَصَمِّ وَٱلۡبَصِيرِ وَٱلسَّمِيعِۚ هَلۡ يَسۡتَوِيَانِ مَثَلًاۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Mfano wa makundi mawili hayo ni kama kipofu na kiziwi na (kama) aliye na uoni sana na anayesikia mno hivi nikweli makundi mawili hayo yanalingana? Kwanini ham-kumbuki?
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Na kwa hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake (akawaambia watu wake kuwa) hakika mimi kwenu ni muonyaji ninaye bainisha
أَن لَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ أَلِيمٖ
(Kwamba) musimuabudu yeyote ispokuwa Allah kwa hakika mimi ninaogopea kwenu adhabu ya siku yenye kuumiza mno
فَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرٗا مِّثۡلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمۡ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ ٱلرَّأۡيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلِۭ بَلۡ نَظُنُّكُمۡ كَٰذِبِينَ
Wakasema waheshimiwa ambao wamekufuru katika watu wake: Wewe hatukuoni (chochote) ispokuwa tu ni mtu mfano wetu (sio Malaika) na hatuoni wafuasi wako ispokuwa tu ni wale ambao ni wanyonge wetu wenye mawazo duni, na hatuwaoni kuwa mnaubora wowote kwetu bali tuna hakika kuwa ni waongo
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتۡ عَلَيۡكُمۡ أَنُلۡزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمۡ لَهَا كَٰرِهُونَ
Akasema enyi jamaa zangu hivi mwaonaje nikiwa nina hoja kutoka kwa Mola wangu mlezi na amenipa rehema kutoka kwake na ikafichwa kwenu, hivi tuwalazimishe kukubali na ilhali nyinyi mnaichukia?
وَيَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مَالًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْۚ إِنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَلَٰكِنِّيٓ أَرَىٰكُمۡ قَوۡمٗا تَجۡهَلُونَ
Na enyi jamaa zangu siwaombi mali (malipo kama ujira wa kazi ya kuwafikishia daawa) hakuna wakunilipa ispokuwa Allah tu, nami si mwenye kuwafukuza wale walioamini (kwa unyonge wao), kwa hakika wao watakutana na Mola wao mlezi lakini mimi ninakuoneni ni watu wajinga
وَيَٰقَوۡمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمۡۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Na enyi jama zangu ninani atakaeninusuru kutokana na (adhabu ya) Allah iwapo nitawafukuza? Hivi hamuonyeki?