Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 211

وَمَا يَنۢبَغِي لَهُمۡ وَمَا يَسۡتَطِيعُونَ

Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 212

إِنَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّمۡعِ لَمَعۡزُولُونَ

Hakika hao wametengwa na kusikia



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 213

فَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُعَذَّبِينَ

Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Allah ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 214

وَأَنذِرۡ عَشِيرَتَكَ ٱلۡأَقۡرَبِينَ

Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 215

وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 216

فَإِنۡ عَصَوۡكَ فَقُلۡ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ

Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 217

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 218

ٱلَّذِي يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ

Ambaye anakuona unapo simama,



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 219

وَتَقَلُّبَكَ فِي ٱلسَّـٰجِدِينَ

Na mageuko yako kati ya wanao sujudu



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 220

إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 221

هَلۡ أُنَبِّئُكُمۡ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ

Je! Nikwambieni nani wana-washukia Mashet’ani?



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 222

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ

Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 223

يُلۡقُونَ ٱلسَّمۡعَ وَأَكۡثَرُهُمۡ كَٰذِبُونَ

Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 224

وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلۡغَاوُۥنَ

Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 225

أَلَمۡ تَرَ أَنَّهُمۡ فِي كُلِّ وَادٖ يَهِيمُونَ

Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 226

وَأَنَّهُمۡ يَقُولُونَ مَا لَا يَفۡعَلُونَ

Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?



Sure: ASH-SHUARAA 

Vers : 227

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَذَكَرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا وَٱنتَصَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَيَّ مُنقَلَبٖ يَنقَلِبُونَ

Isipokuwa wale walioamini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Allah kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka