Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 151

كَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِيكُمۡ رَسُولٗا مِّنكُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمۡ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Kama tulivyokuleteeni Mtume anayetokana nanyi anayekusomeeni Aya zetu na anayekutakaseni na anayekufundisheni kitabu na hekima, na anakufundisheni mliyokuwa hamyajui



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 152

فَٱذۡكُرُونِيٓ أَذۡكُرۡكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِي وَلَا تَكۡفُرُونِ

Basi nikumbukeni nami nitawakumbuka, na nishukuruni na msinikufuru



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 153

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Enyi mlioamini, ombeni msaada kwa uvumilivu (subra) na kuswali. Bila shaka, Allah yupo pamoja na wenye uvumilivu



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 154

وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتُۢۚ بَلۡ أَحۡيَآءٞ وَلَٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ

Na msiseme kuwa, waliouawa katika njia ya Allah ni wafu. Bali wapo hai, lakini hamtambui



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 155

وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَيۡءٖ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Na kwa yakini kabisa, tutakutieni katika mtihani mdogo wa hofu na njaa na upungufu wa mali na uhai na matunda. Na wape bishara wenye uvumilivu



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 156

ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٞ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika, sisi ni wa Allah, na kwake yeye tu tutarejea



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 157

أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ صَلَوَٰتٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَرَحۡمَةٞۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُهۡتَدُونَ

Hao watashushiwa msamaha na rehema kutoka kwa Mola wao na hao tu ndio wenye kuongoka



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 158

۞إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلۡمَرۡوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِۖ فَمَنۡ حَجَّ ٱلۡبَيۡتَ أَوِ ٱعۡتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَاۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَإِنَّ ٱللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ

Hakika, Swafaa na Mar’wa ni katika alama za[1] Allah. Basi anayehiji (katika) Nyumba (tukufu) au kufanya Umra, si kosa kwake kuizunguka milima miwili hiyo. Na anayefanya wema, kwa yakini, Allah ni Mwenye kushukuru, Mjuzi wa kila jambo


1- - Dini ya Allah


Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 159

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡتُمُونَ مَآ أَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلۡهُدَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا بَيَّنَّـٰهُ لِلنَّاسِ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أُوْلَـٰٓئِكَ يَلۡعَنُهُمُ ٱللَّهُ وَيَلۡعَنُهُمُ ٱللَّـٰعِنُونَ

Hakika, wale wanaoficha hoja za wazi na muongozo tuliouteremsha baada ya kuwa tumeubainisha kwa watu kitabuni, hao Allah anawalaani na pia wanalaaniwa na wenye kulaani



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 160

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَبَيَّنُواْ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَتُوبُ عَلَيۡهِمۡ وَأَنَا ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Isipokuwa waliotubu na wakare-kebisha na wakabainisha. Basi hao nitakubali tobayao, na mimi tu ndiye Mwingi wa kukubali toba, Mwingi wa kurehemu



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 161

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٌ أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ

Hakika, waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao wanastahiki laana ya Allah, na ya Malaika na (laana) ya watu wote



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 162

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Humo watakaa daima. Hawatapunguziwa adhabu na hawatapewa muda (wa kuomba radhi)



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 163

وَإِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ

Na Allah wenu ni Allah mmoja tu. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa yeye tu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 164

إِنَّ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱلۡفُلۡكِ ٱلَّتِي تَجۡرِي فِي ٱلۡبَحۡرِ بِمَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن مَّآءٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٖ وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ وَٱلسَّحَابِ ٱلۡمُسَخَّرِ بَيۡنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Hakika, katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kupishana kwa usiku na mchana, na (katika) merikebu zitembeazo baharini na kubeba vitu viwafaavyo watu, na (katika) maji (mvua) aliyoteremsha Allah kutoka mawinguni akahuisha ardhi baada ya kufa kwake na akasambaza (ardhini) humo kila aina ya wanyama, na (katika) mabadiliko ya Pepo na (katika) mawingu yanayoelea kati ya mbingu na ardhi, kwa hakika kabisa (katika yote hayo) kuna ishara nyingi kwa watu wanaozingatia



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 165

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادٗا يُحِبُّونَهُمۡ كَحُبِّ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَشَدُّ حُبّٗا لِّلَّهِۗ وَلَوۡ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِذۡ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ أَنَّ ٱلۡقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعَذَابِ

Na miongoni mwa watu kuna wanaofanya washirika badala ya (kumuamini) Allah (pekee); wanawapenda kama wampendavyo Allah. Na walioamini wanampenda zaidi Allah. Na laiti waliodhulumu wangejua watakapoiona adhabu kwamba, nguvu zote ni za Allah, na kwamba, Allah ni mkali wa kuadhibu[1]


1- - Wasingethubutu kumfanyia Allah washirika.


Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 166

إِذۡ تَبَرَّأَ ٱلَّذِينَ ٱتُّبِعُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَ وَتَقَطَّعَتۡ بِهِمُ ٱلۡأَسۡبَابُ

(Kumbuka) Waliofuatwa watakapowakataa waliowafuata, hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu, na yakakatika mahusiano (yao)



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 167

وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ لَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَتَبَرَّأَ مِنۡهُمۡ كَمَا تَبَرَّءُواْ مِنَّاۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡ حَسَرَٰتٍ عَلَيۡهِمۡۖ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ

Na watasema wale waliofuata: Laiti tungeweza kurudi (duniani) tukawakataa kama wanavyotukataa. Hivi ndivyo Allah atakavyowaonesha vitendo vyao kuwa majuto kwao, na hawatakuwa wenye kutoka motoni



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 168

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٌ

Enyi watu, kuleni vilivyomo katika ardhi vikiwa halali na vizuri. Na msifuate nyendo za shetani kwa sababu, bila ya shaka, yeye kwenu ni adui aliye wazi



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 169

إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ وَٱلۡفَحۡشَآءِ وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Yeye anakuamrisheni mambo mabaya na machafu tu na …kumsingizia Allah msiyoyajua



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 170

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ بَلۡ نَتَّبِعُ مَآ أَلۡفَيۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ

Na walipoambiwa: Fuateni aliyoteremsha Allah, walisema: Bali tunafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Hivi (wanawafuata tu) hata kama baba zao (hao) hawakuwa wakifahamu chochote wala hawakuongoka?



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 171

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ كَمَثَلِ ٱلَّذِي يَنۡعِقُ بِمَا لَا يَسۡمَعُ إِلَّا دُعَآءٗ وَنِدَآءٗۚ صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Na mfano wa waliokufuru ni kama mfano wa anayemwita asiyesikia ila (ni) sauti na kelele tu. Ni viziwi, mabubu, vipofu kwa sababu hiyo hawatumii akili[1]


1- - Wakayazingatia yale wanayo ambiwa.


Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 172

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِلَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ

Enyi mlioamini, kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, na mshukuruni Allah ikiwa mnamuabudu yeye tu



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 173

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيۡرِ ٱللَّهِۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Yeye tu amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichochinjwa kwa kutaja jina lisiliokuwa la Allah. Lakini, aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupitiliza kiasi, hana dhambi[1]. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu


1- - Kula katika hivyo vilivyo haramishwa.


Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 174

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡتُمُونَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَشۡتَرُونَ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَـٰٓئِكَ مَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ إِلَّا ٱلنَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Hakika, wale wanaoficha yaliyoteremshwa na Allah katika kitabu, na kufadhilisha kwayo thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto tu, wala Allah hatawasemeza Siku ya Kiyama wala hatawatakasa; na watapata adhabu iumizayo



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 175

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡعَذَابَ بِٱلۡمَغۡفِرَةِۚ فَمَآ أَصۡبَرَهُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ

Hao ndio walionunua upotevu badala ya uongofu, na adhabu badala ya msamaha. Ni wakushangaza sana uvumilivu wao wa kuuvumilia Moto!



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 176

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَفِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ

Hayo ni kwa sababu Allah ameteremsha kitabu kwa haki, na wale waliotafautiana katika kitabu wamo katika mpasuko ulio mbali



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 177

۞لَّيۡسَ ٱلۡبِرَّ أَن تُوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ قِبَلَ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلۡكِتَٰبِ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ وَءَاتَى ٱلۡمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ ذَوِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَٱلسَّآئِلِينَ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُوفُونَ بِعَهۡدِهِمۡ إِذَا عَٰهَدُواْۖ وَٱلصَّـٰبِرِينَ فِي ٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَحِينَ ٱلۡبَأۡسِۗ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُتَّقُونَ

Sio wema peke yake kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni (wa) wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Vitabu na Manabii, na wanatoa mali pamoja na kuwa wanaipenda wakawapa ndugu na mayatima na maskini na wasafiri na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha swala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na madhara na (katika) wakati wa vita. Hao ndio wa kweli na hao ndio wa mchao Allah



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 178

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِصَاصُ فِي ٱلۡقَتۡلَىۖ ٱلۡحُرُّ بِٱلۡحُرِّ وَٱلۡعَبۡدُ بِٱلۡعَبۡدِ وَٱلۡأُنثَىٰ بِٱلۡأُنثَىٰۚ فَمَنۡ عُفِيَ لَهُۥ مِنۡ أَخِيهِ شَيۡءٞ فَٱتِّبَاعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيۡهِ بِإِحۡسَٰنٖۗ ذَٰلِكَ تَخۡفِيفٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٞۗ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Enyi mlioamini, mmeandikiwa kulipa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Na aliyesamehewa jambo na ndugu yake (mtendewa jinai) basi fidia ifuatiliwe kwa wema na atekelezewe kwa uzuri. Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Na atakayekiuka baada ya hayo, basi yeye atapata adhabu iumizayo



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 179

وَلَكُمۡ فِي ٱلۡقِصَاصِ حَيَوٰةٞ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na mtakuwa na uhai (ulio bora) katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili muogope (msalimike)



Sure: AL-BAQARAH 

Vers : 180

كُتِبَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ إِن تَرَكَ خَيۡرًا ٱلۡوَصِيَّةُ لِلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ

Mmeandikiwa mmoja wenu kutoa wasia kwa wazazi na ndugu kwa namna nzuri anapofikwa na mauti kama akiacha mali, ikiwa ni haki kwa wa mchao Allah