أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na milima akaisimamisha,
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi itakapokuja hilo balaa kubwa kabisa
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya, (aliyoyakimbilia kuyafanyia juhudi)
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Na moto utakapodhihirishwa wazi kwa mwenye kuona
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Basi yule aliyepindukia mipaka na kuasi
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Na akapenda zaidi maisha ya dunia
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake, na akaikataza nafsi yake na na matamanio
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Wanakuuliza kuhusu Kiyama lini kufika kwake?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Una nini wewe hata ukitaje hicho kiyama?
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Kwa Mola wako ndio mwisho wake
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kukiogopa hicho kiyama
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Siku watakapokiona, watakuwa kana kwamba hawakubaki (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake