Sure: ANNAHLI 

Vers : 31

جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ لَهُمۡ فِيهَا مَا يَشَآءُونَۚ كَذَٰلِكَ يَجۡزِي ٱللَّهُ ٱلۡمُتَّقِينَ

Bustani za milele wataziingia zipitazo mbele yake mito watapata humo watakacho. Hivi ndivyo Allah anawalipa Wachamungu



Sure: ANNAHLI 

Vers : 32

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Wale ambao Malaika wame-wafisha wakiwa vizuri (Malaika watawaambia) Assalamu alaykum (amani iwe juu yenu!) Ingieni Peponi kwasababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda



Sure: ANNAHLI 

Vers : 33

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ أَمۡرُ رَبِّكَۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Hawangoji isipokuwa wawajie Malaika au iwafike amri ya Mola wako mlezi. Hivyo ndivyo walivyofanya wale waliokuwa kabla yao. Na Allah hakuwadhulumu, lakini wenyewe walikuwa wanazidhulumu nafsi zao



Sure: ANNAHLI 

Vers : 34

فَأَصَابَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُواْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Basi ukawafika uovu wa yale waliyoyafanya na ikawazunguka (adhabu) waliyokuwa wakiifanyia mzaha



Sure: ANNAHLI 

Vers : 35

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na watasema wale walio-shirikisha (Miungu mingine na Allah): Laiti kama Allah angali-penda, tusingeabudu chochote badala yake, sisi na Baba zetu, na tusingeharamisha chochote (ambacho Allah hakukiharamisha). (Hoja) kama hizi walizitoa wale waliokuwa kabla yao. Basi si kazi ya Mitume isipokuwa kufikisha (ujumbe) waziwazi[1]


1- - Katika Aya hii Allah anaeleza namna makafiri watakavyojenga hoja batili Siku ya Kiama ili wajiokoe na adhabu watadai kuwa hiyo ni qadhaa na qadari kwa maana walichokifanya hapa duniani ndivyo Allah alivyotaka wafanye, hawakuwa na hiari katika mambo. Hoja hii haipo kwa sababu Mitume walikuja na wakabainisha kila kitu wao wakakaidi.


Sure: ANNAHLI 

Vers : 36

وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّـٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Na bila shaka tulipeleka Mtume katika kila umma wakawaambia kwamba: Muabuduni Allah (peke yake) na epukeni (kuabudu) Twaghuti[1]. Basi miongoni mwao Allah amewaongoza (njia sahihi ya Uislamu), na miongoni mwao umewathibitikia upotevu. Basi tembeeni (nendeni) ardhini na muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wakadhibishaji


1- - Twaghuti ni kitu chochote kinachoabudiwa badala ya Allah kama sanamu, mawe shetani n.k.


Sure: ANNAHLI 

Vers : 37

إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ

Kama unafanya pupa juu ya kuongoka kwao, basi kwa hakika Allah hamuongozi yule anayeshikilia kupotea. Nao hawana yeyote wakuwanusuru



Sure: ANNAHLI 

Vers : 38

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na walimuapia Allah kwa kiapo chao cha nguvu kwamba Allah hatamfufua yeyote anayekufa. Ni kweli kabisa hiyo ni ahadi yake (atawafufua), lakini watu wengi hawaelewi



Sure: ANNAHLI 

Vers : 39

لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ

Ili kuwabainishia yale waliyohitilafiana, na ili wajue wale waliokufuru kwamba, wao walikuwa waongo



Sure: ANNAHLI 

Vers : 40

إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Hakika si vingine ni kauli yetu tu tunapotaka kitu tunakiambia kuwa, basi kinakuwa



Sure: ANNAHLI 

Vers : 41

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wale waliohama kwa ajili ya Allah baada ya kudhulumiwa, bila shaka tutawakalisha katika dunia kwa wema na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti wangekuwa wanajua!



Sure: ANNAHLI 

Vers : 42

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

(Hao ni) wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao mlezi



Sure: ANNAHLI 

Vers : 43

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Na hatukutuma kabla yako (ewe Muhammad) isipokuwa (Mitume) wanaume ambao tuliwapa wah-yi (ufunuo) basi (ikiwa enyi Washirikina hamuamini) waulizeni watunzaji wa vitabu vitakatifu (watakuelezeni) ikiwa ninyi hamjui



Sure: ANNAHLI 

Vers : 44

بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ

(Tuliwatuma) wakiwa na dalili za wazi. Na tumekuteremshia (ewe Muhammad) ukumbusho (Qur’ani) ili uwabainishie watu (kilichojificha katika maana na hukumu zake), na ili wapate kutafakari



Sure: ANNAHLI 

Vers : 45

أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخۡسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ يَأۡتِيَهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ

Hivi, wanajiona wako salama wale waliofanya vitimbi vibaya kwamba Allah hataweza kuwa-didimiza ardhini, au (wanaona kuwa) haitawafika adhabu ghafla bila ya kuhisi kuja kwake?



Sure: ANNAHLI 

Vers : 46

أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ فِي تَقَلُّبِهِمۡ فَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ

Au iwachukuwe wakiwa katika mihangaiko yao? Na hawatoweza wao kuponyoka



Sure: ANNAHLI 

Vers : 47

أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ عَلَىٰ تَخَوُّفٖ فَإِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٌ

Au awachukuwe (kwa kuwa-punguzia mali matunda na nafsi) au kwa adhabu yake? Hakika Mola wenu ni mlezi mpole mno, mwenye rehema



Sure: ANNAHLI 

Vers : 48

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ يَتَفَيَّؤُاْ ظِلَٰلُهُۥ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدٗا لِّلَّهِ وَهُمۡ دَٰخِرُونَ

Hivi, hawaoni vile vyote alivyo viumba Allah, (kama milima na miti) vivuli vyake vinageuka kulia na kushoto (kwa kufuata mwenendo wajua mchana na mwezi wakati wa usiku) vyote vinamsujudia Allah, huku vimedhalilika?



Sure: ANNAHLI 

Vers : 49

وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ

Na kwa Allah vinasujudu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini wanyama na Malaika, nao hawafanyi kiburi



Sure: ANNAHLI 

Vers : 50

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوۡقِهِمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ۩

Wanamuogopa Mola wao mlezi juu yao, na wanatenda yale wanayoamrishwa



Sure: ANNAHLI 

Vers : 51

۞وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓاْ إِلَٰهَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَإِيَّـٰيَ فَٱرۡهَبُونِ

Na amesema Allah: Kamwe msiwe na Miungu kuwa wawili, hakika sivingine Mungu ni mmoja tu: basi mimi tu niogopeni



Sure: ANNAHLI 

Vers : 52

وَلَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًاۚ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ

Na ni vyake tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini (kuumba umiliki na waja, na ni haki yake kufanyiwa ibada, utiifu na ikhlas) na dini ni yake daima. Basi hivi mnamuogopa mwingine badala ya Allah?



Sure: ANNAHLI 

Vers : 53

وَمَا بِكُم مِّن نِّعۡمَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيۡهِ تَجۡـَٔرُونَ

Na neema yeyote mliyonayo imetoka kwa Allah. Kisha inapowaguseni dhara, basi yeye tu mnamlilia



Sure: ANNAHLI 

Vers : 54

ثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنكُم بِرَبِّهِمۡ يُشۡرِكُونَ

Kisha anapo waondoleeni dhara hilo, mara kundi miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao mlezi;



Sure: ANNAHLI 

Vers : 55

لِيَكۡفُرُواْ بِمَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡۚ فَتَمَتَّعُواْ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Ili wavikatae tulivyowapa. Basi stareheni[1], mtakuja mtajua (matokeo ya ukafiri wenu)


1- - Kwa neema tulizo waneemesha nazo hapa duniani ikiwemo kuwaondolea majanga.


Sure: ANNAHLI 

Vers : 56

وَيَجۡعَلُونَ لِمَا لَا يَعۡلَمُونَ نَصِيبٗا مِّمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡۗ تَٱللَّهِ لَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَفۡتَرُونَ

Na (katika ubaya wao) wana-tenga fungu katika vile tuli-vyowaruzuku kuvipa vile visivyojua chochote (Waungu wao). Naapa kwa haki ya Allah, bila shaka mtaulizwa kuhusu yote mliyokuwa mkiyatunga



Sure: ANNAHLI 

Vers : 57

وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ ٱلۡبَنَٰتِ سُبۡحَٰنَهُۥ وَلَهُم مَّا يَشۡتَهُونَ

Na wanamfanyia Allah mabinti (kwa kusema Malaika ni mabinti wa Allah!) utakasifu ni wake!(Allah ametakasika na kauli yao hiyo) Ilhali wanajifanyia wanachotaka



Sure: ANNAHLI 

Vers : 58

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِٱلۡأُنثَىٰ ظَلَّ وَجۡهُهُۥ مُسۡوَدّٗا وَهُوَ كَظِيمٞ

Na pindi mmoja wao anapopewa habari ya (kuzaliwa mtoto) mwa-namke, uso wake hugeuka mweusi, nakujawa na huzuni mno



Sure: ANNAHLI 

Vers : 59

يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓۚ أَيُمۡسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمۡ يَدُسُّهُۥ فِي ٱلتُّرَابِۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ

Hujificha (asionekane) na watu kwasababu ya kujihisi vibaya kutokana na ile bishara aliyoiona kwake mbaya. (huku akijishauri kuhusu binti huyo) hivi, amchukue na avumilie fedheha au amfukie ardhini akiwa hai? Sikilizeni! Ni mabaya wanayoyahukumu



Sure: ANNAHLI 

Vers : 60

لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوۡءِۖ وَلِلَّهِ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Kwa wale wasioamini Akhera hawajui sifa ya ubaya, kushindwa uhitaji, ujinga wala ukafiri. Na Allah tu ndio mwenye sifa za juu (ukamilifu, kujitosha), nguvu, ufalme na hekima