Surata: ANNISAI 

O versículo : 151

أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ حَقّٗاۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Hao ndio makafiri kweli, na tumewaandalia makafiri adhabu yenye kukudhalilisha



Surata: ANNISAI 

O versículo : 152

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَلَمۡ يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ أُوْلَـٰٓئِكَ سَوۡفَ يُؤۡتِيهِمۡ أُجُورَهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na wale waliomuamini Allah na Mitume wake na hawakutofautisha baina ya (Mtume) yeyote miongoni mwao, Allah atawapa ujira wao. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehem



Surata: ANNISAI 

O versículo : 153

يَسۡـَٔلُكَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيۡهِمۡ كِتَٰبٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِۚ فَقَدۡ سَأَلُواْ مُوسَىٰٓ أَكۡبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓاْ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ بِظُلۡمِهِمۡۚ ثُمَّ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَعَفَوۡنَا عَن ذَٰلِكَۚ وَءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا

Watu wa Kitabu wanakutaka (kwa inadi) uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Kwa hakika walimtaka (Mtume) Mussa (kwa inadi pia awaonyeshe jambo) kubwa zaidi kuliko hilo na kusema: Tuonyeshe Allah (tumuone) wazi wazi. (Kwasababu hiyo) kimondo kiliwachukua (kiliwaangamiza) kwasababu ya udhalimu wao (wa ukinzani na kukufuru). Kisha walimfanya ndama kuwa (Mungu) baada ya kuwa hoja zilizowazi zimewafikia tukasamehe hayo.[1] Na tulimpa Mussa hoja inayofafanua


1- - Madhambi ya ukaidi wa kutoamini mpaka wamuone Allah duniani na madhambi ya kuabudu ndama.


Surata: ANNISAI 

O versículo : 154

وَرَفَعۡنَا فَوۡقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَٰقِهِمۡ وَقُلۡنَا لَهُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُلۡنَا لَهُمۡ لَا تَعۡدُواْ فِي ٱلسَّبۡتِ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا

Na tulinyanyua (mlima) Turi juu yao kwa makubaliano nao na kuwaambia: Ingieni lango (la mji wenu) mkiwa mmeinama. Na tuliwaambia: Msivunje mwiko (wa kuiheshimu) siku ya Jumamosi (Sabato). Na tulichukua kwao ahadi nzito



Surata: ANNISAI 

O versículo : 155

فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ وَكُفۡرِهِم بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَقَتۡلِهِمُ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَقَوۡلِهِمۡ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَلۡ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيۡهَا بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا

Basi kwasababu ya kuvunja kwao ahadi zao na kuzikufuru kwao Aya za Allah na kuua kwao Mitume pasina haki yoyote na kusema kwao: Mioyo yetu imefunikwa, wakati Allah ameipiga chapa kwa ukafiri wao, basi (kwasababu ya yote hayo) hawaamini ila kidogo sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 156

وَبِكُفۡرِهِمۡ وَقَوۡلِهِمۡ عَلَىٰ مَرۡيَمَ بُهۡتَٰنًا عَظِيمٗا

Na (pia hawaamini isipokuwa kidogo sana) kwasababu ya ukafiri wao na kumsingizia kwao Mariamu uzushi mkubwa sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 157

وَقَوۡلِهِمۡ إِنَّا قَتَلۡنَا ٱلۡمَسِيحَ عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ رَسُولَ ٱللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَٰكِن شُبِّهَ لَهُمۡۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُۚ مَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍ إِلَّا ٱتِّبَاعَ ٱلظَّنِّۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينَۢا

Na (kwa) kusema kwao: Hakika, sisi tumemuua Masihi Issa Mwana wa Mariamu Mtume wa Allah. Na hawakumuua na hawakumsulubu[1], na lakini walifananishiwa tu. Na hakika, waliotofautiana katika hilo, kwa yakini kabisa, wamo katika shaka nalo. Hawana elimu yoyote ya (kulijua) hilo, isipokuwa tu kufuata dhana, na, kwa yakini, hawakumuua


1- - Kumekuwepo na madai dhaifu ya udhaifu wa lugha ya Kiarabu katika Aya hii kwamba, imekuwaje kutangulizwe kuua kabla ya kusulubu wakati kinachotakiwa kutamkwa kwanza ni kusulubu halafu kuua? Ilivyo ni kwamba, Aya imejibu madai ya Wayahudi ya kuua kama mwanzo wa Aya unavyoeleza. Lengo la msingi la Wayahudi lilikuwa kumuua Isa na sio kumsulubu tu. Aya imejibu madai hayo ya msingi kwanza, na ndio maana pia mwisho wa Aya umerudia kukanusha madai hayo kwa msisitizo zaidi. Utaratibu huu uliotajwa na Qur’ani pia umetajwa katika Kumbukumbu la Torati 21:22 na Yoshua: 10:26. Pili ni kwamba kiunganishi cha “na” katika fasihi ya lugha ya Qur’ani ambayo ni Kiarabu hakilazimishi mfuatano. Unaposema: Amekuja Ali na Abdala hailazimishi kwamba aliyekuja mwanzo ni Ali. Neno “na” kwa mujibu wa fasihi ya lugha ya Kiarabu linawakilisha ujio wa Ali na Abdala bila ya kuainisha nani amekuja mwanzo.


Surata: ANNISAI 

O versículo : 158

بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيۡهِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا

Bali Allah alimpaisha kwake. Na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 159

وَإِن مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ إِلَّا لَيُؤۡمِنَنَّ بِهِۦ قَبۡلَ مَوۡتِهِۦۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ شَهِيدٗا

Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu isipokuwa kwa yakini kabisa watamuamini tu kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Kiama atakuwa shahidi kwao



Surata: ANNISAI 

O versículo : 160

فَبِظُلۡمٖ مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ طَيِّبَٰتٍ أُحِلَّتۡ لَهُمۡ وَبِصَدِّهِمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ كَثِيرٗا

Kwasababu ya dhuluma ya Wayahudi tumewaharamishia vizuri walivyohalalishiwa na kwasababu ya kuwazuia (watu) wengi wasiifuate njia ya Allah



Surata: ANNISAI 

O versículo : 161

وَأَخۡذِهِمُ ٱلرِّبَوٰاْ وَقَدۡ نُهُواْ عَنۡهُ وَأَكۡلِهِمۡ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ مِنۡهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Na (kwasababu ya) kuchukua kwao Riba na ilhali wamekatazwa, na (kwasababu ya) kula kwao mali za watu kwa batili. Na tumewaandalia makafiri miongoni mwao adhabu kali sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 162

لَّـٰكِنِ ٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ مِنۡهُمۡ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَۚ وَٱلۡمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَٱلۡمُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أُوْلَـٰٓئِكَ سَنُؤۡتِيهِمۡ أَجۡرًا عَظِيمًا

Lakini waliobobea katika elimu miongoni mwao, na waumini wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wenye kusimamisha Swala na wenye kutoa Zaka na wenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho. Hao tutawapa malipo makubwa sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 163

۞إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Hakika, sisi tumekufunulia (Wahyi) kama tulivyomfunulia (Wahyi) Nuhu na Manabii (wengine) baada yake. Na tumemfunulia (Wahyi) Ibrahimu na Ismail na Isihaka na Yakubu na kizazi (chake) na Issa na Ayubu na Yunus na Haruna na Sulaimani. Na tulimpa Daudi Zaburi



Surata: ANNISAI 

O versículo : 164

وَرُسُلٗا قَدۡ قَصَصۡنَٰهُمۡ عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُ وَرُسُلٗا لَّمۡ نَقۡصُصۡهُمۡ عَلَيۡكَۚ وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَكۡلِيمٗا

Na Mitume tuliokwisha kuku-simulia kabla, na Mitume (wengine) hatukukusimulia. Na Allah alizungumza na Mussa kwa maneno



Surata: ANNISAI 

O versículo : 165

رُّسُلٗا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى ٱللَّهِ حُجَّةُۢ بَعۡدَ ٱلرُّسُلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا

Mitume wanatoa bishara na wanaotoa maonyo ili watu wasiwe na hoja kwa Allah baada ya (kupele-kewa) Mitume. Na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana



Surata: ANNISAI 

O versículo : 166

لَّـٰكِنِ ٱللَّهُ يَشۡهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيۡكَۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلۡمِهِۦۖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَشۡهَدُونَۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا

Lakini Allah anashuhudia aliyokuteremshia. Ameyateremsha kwa ujuzi wake, na Malaika (pia) wanashuhudia. Na inatosha kwamba Allah ni Shahidi



Surata: ANNISAI 

O versículo : 167

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ قَدۡ ضَلُّواْ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا

Hakika, wale waliokufuru na wakaweka vikwazo ili njia ya Allah isifuatwe, hakika wamekwishapotea upotevu ulio mbali sana (na haki)



Surata: ANNISAI 

O versículo : 168

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَظَلَمُواْ لَمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ طَرِيقًا

Hakika, wale ambao wame-kufuru na wakadhulumu (nafsi zao kwa kufanya ushirikina), Allah hakuwa Mwenye kuwasamehe wala kuwaongoza njia (kama hawatatubu)



Surata: ANNISAI 

O versículo : 169

إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا

Isipokuwa (atawaongoza) njia ya Jahanamu wakae humo milele. Na hilo ni jambo jepesi sana kwa Allah



Surata: ANNISAI 

O versículo : 170

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Enyi watu, hakika amekujieni Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, iwe kheri kwenu. Na mkikufuru basi hakika ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allah ni Mjuzi sana, Mwenye hekima



Surata: ANNISAI 

O versículo : 171

يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ وَلَا تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلۡقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرۡيَمَ وَرُوحٞ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُواْ ثَلَٰثَةٌۚ ٱنتَهُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٞۘ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا

Enyi Watu wa Kitabu, msichupe mipaka katika dini yenu na msimsemee Allah isipokuwa haki tu. Hakika, ilivyo ni kwamba Masihi, Issa Mwana wa Mariamu ni Mtume wa Allah na neno lake alilompelekea Mariamu, na ni roho iliyotoka kwake. Basi muaminini Allah na Mitume wake, na msiseme: Miungu ni watatu. Acheni (kuamini hivyo) itakuwa kheri kwenu. Hakika, ilivyo ni kwamba, Allah ni Mungu mmoja tu, ametakasika (kwa) kutokuwa na mwana. Ni vyake yeye tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na imetosha kwamba, Allah ni Mwenye kutegemewa



Surata: ANNISAI 

O versículo : 172

لَّن يَسۡتَنكِفَ ٱلۡمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبۡدٗا لِّلَّهِ وَلَا ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ ٱلۡمُقَرَّبُونَۚ وَمَن يَسۡتَنكِفۡ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيَسۡتَكۡبِرۡ فَسَيَحۡشُرُهُمۡ إِلَيۡهِ جَمِيعٗا

Katu, Masihi hataona uchama (kinyaa) kuwa mja wa Allah wala Malaika waliokaribu (na Allah). Na yeyote anayeona kinyaa kumuabudu Allah na kufanya kiburi, basi Allah atawakusanya wote kwake (Siku ya Kiama na kuwahukumu)



Surata: ANNISAI 

O versículo : 173

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضۡلِهِۦۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡتَنكَفُواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ فَيُعَذِّبُهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Basi wale walioamini na kutenda mema (Allah) atawalipa ujira wao kamili na kuwaongozea fadhila zake. Na ama wale walioona kinyaa na kufanya kiburi, basi (Allah) atawaadhibu adhabu iumizayo sana, na hawatapata mlinzi wala wa kuwanusuru badala ya Allah



Surata: ANNISAI 

O versículo : 174

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُم بُرۡهَٰنٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ نُورٗا مُّبِينٗا

Enyi watu, hakika imekujieni hoja (Mtume Muhammad, Allah amfikishie rehema na amani) kutoka kwa Mola wenu, na tumekuteremshieni nuru (Qur’ani) yenye kufafanua



Surata: ANNISAI 

O versículo : 175

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱعۡتَصَمُواْ بِهِۦ فَسَيُدۡخِلُهُمۡ فِي رَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَفَضۡلٖ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَيۡهِ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Basi ambao wamemuamini Allah na wakashikamana naye basi atawaingiza katika rehema na fadhila zake na atawaongoza njia iliyonyooka kuelekea kwake (njia ambayo ni Uislamu)



Surata: ANNISAI 

O versículo : 176

يَسۡتَفۡتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِي ٱلۡكَلَٰلَةِۚ إِنِ ٱمۡرُؤٌاْ هَلَكَ لَيۡسَ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَهُۥٓ أُخۡتٞ فَلَهَا نِصۡفُ مَا تَرَكَۚ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهَا وَلَدٞۚ فَإِن كَانَتَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَۚ وَإِن كَانُوٓاْ إِخۡوَةٗ رِّجَالٗا وَنِسَآءٗ فَلِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۗ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ أَن تَضِلُّواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ

Wanakutaka Fat’wa. Sema: Allah anakupeni Fat’wa kuhusu Kalala.[1] Ikiwa mtu aliyekufa hakuacha mtoto na amemuacha dada, basi huyo dada anastahiki kupata nusu ya mali aliyoacha. Na yeye atamrithi dada yake kama (dada naye) hakuacha mtoto. (Dada) Wakiwa wawili watapata thuluthi mbili katika mali aliyoacha (marehemu kaka yao). Na (warithi) wakiwa ndugu; wanaume na wanawake basi mwanaume mmoja anastahiki kupata fungu lililo sawa na la wanawake wawili. Allah anakubainishieni nyinyi (sheria zake) ili msipotee. Na Allah ni Mjuzi wa kila kitu


1- - Kalala ni mtu aliyekufa akiwa hakuacha mzazi wala mtoto.