Surata: YUNUS 

O versículo : 91

ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ عَصَيۡتَ قَبۡلُ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Je, hivi sasa (ndio umeamini) na ilhali kwa hakika uliasi hapo kabla na ukawa miongoni mwa waharibifu?



Surata: YUNUS 

O versículo : 92

فَٱلۡيَوۡمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنۡ خَلۡفَكَ ءَايَةٗۚ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنۡ ءَايَٰتِنَا لَغَٰفِلُونَ

Basi leo tunauopoa mwili wako ili uwe ishara (na fundisho) kwa walioko nyuma yako (kwamba wewe sio Mungu). Na hakika kabisa, watu wengi ni wenye kughafilika na aya zetu



Surata: YUNUS 

O versículo : 93

وَلَقَدۡ بَوَّأۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدۡقٖ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ فَمَا ٱخۡتَلَفُواْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na, kwa hakika kabisa, tuliwaweka Wana wa Israili makazi ya ukweli (sahihi na mazuri), na tuliwaruzuku vilivyo vizuri. Basi hawakutofautiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika, Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wanatofautiana



Surata: YUNUS 

O versículo : 94

فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Basi kama una shaka katika yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma kitabu (Taurati) kabla yako. Kwa yakini kabisa, haki imekwisha kukufikia kutoka kwa Mola wako Mlezi. Kwa hiyo, katu usiwe miongoni mwa watiao shaka



Surata: YUNUS 

O versículo : 95

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na kamwe usiwe miongoni mwa wale wanaozipinga Aya za Allah, ikasababisha uwe miongoni mwa walio pata hasara



Surata: YUNUS 

O versículo : 96

إِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتۡ عَلَيۡهِمۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika, wale ambao neno la Mola wako Mlezi limethibiti kwao, kamwe hawaamini



Surata: YUNUS 

O versículo : 97

وَلَوۡ جَآءَتۡهُمۡ كُلُّ ءَايَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ

Na (hawaamini) hata ziwajie Aya zote (miujiza ya kila aina) mpaka waione adhabu iumizayo mno



Surata: YUNUS 

O versículo : 98

فَلَوۡلَا كَانَتۡ قَرۡيَةٌ ءَامَنَتۡ فَنَفَعَهَآ إِيمَٰنُهَآ إِلَّا قَوۡمَ يُونُسَ لَمَّآ ءَامَنُواْ كَشَفۡنَا عَنۡهُمۡ عَذَابَ ٱلۡخِزۡيِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٖ

Basi laiti ungepatikana mji ulioamini na imani yake ikaunufaisha, isipokuwa tu watu wa Yunus. Walipoamini, tuliwaondolea adhabu ya fedheha katika maisha ya duniani na tukawaneemesha kwa muda[1]


1- - Aya hii inaeleza kuwa, hakuna kutubu wakati inapofika adhabu, isipokuwa tu hilo lilitokea kwa watu wa Nabii Yunus tu (Allah amshushie amani). Allah aliwaondolea adhabu baada ya kutubu na kufuata yale ambayo Mtume wao Yunus (Allah amshushie amani) aliwaambia.


Surata: YUNUS 

O versículo : 99

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَأٓمَنَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ كُلُّهُمۡ جَمِيعًاۚ أَفَأَنتَ تُكۡرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ

Na lau kama Mola wako Mlezi angetaka, basi kwa hakika kabisa, wote waliomo duniani wangeamini. Hivi, wewe unawalazimisha watu ili wawe waumini?



Surata: YUNUS 

O versículo : 100

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تُؤۡمِنَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَجۡعَلُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ

Na haiwi kwa nafsi yoyote kuamini, isipokuwa tu kwa idhini ya Allah. Na (Allah) anaweka uchafu (wa uovu na upotevu) kwa wale wasiotumia akili (na kumtambua Allah na kumuamini)



Surata: YUNUS 

O versículo : 101

قُلِ ٱنظُرُواْ مَاذَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَا تُغۡنِي ٱلۡأٓيَٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ

Sema: Tazameni; kuna nini mbinguni na ardhini? Na Aya na maonyo hayawasaidii watu wasioamini



Surata: YUNUS 

O versículo : 102

فَهَلۡ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثۡلَ أَيَّامِ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِهِمۡۚ قُلۡ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Basi hivi hawangojei isipokuwa tu mfano wa masiku ya watu waliopita kabla yao? Sema: Basi ngojeeni, mimi pamoja na nyinyi ni miongoni mwa wenye kungojea



Surata: YUNUS 

O versículo : 103

ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيۡنَا نُنجِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Kisha tutawaokoa Mitume wetu na wale walioamini. Kama hivyo, ni haki kwetu kuwaokoa Waumini



Surata: YUNUS 

O versículo : 104

قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema: Enyi watu, ikiwa nyinyi mna shaka na (usahihi wa) dini yangu, basi mimi siabudu wale mnaowaabudu badala ya Allah. Na lakini ninamuabudu Allah ambaye anakufisheni, na nimeamrishwa kuwa miongoni mwa waumini



Surata: YUNUS 

O versículo : 105

وَأَنۡ أَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na (pia nimeamrishwa) kwamba: Elekeza uso wako katika dini[1] hali ya kumtakasa (Allah), na usiwe miongoni mwa washirikina


1- - Umetajwa uso hapa kwa sababu uso ndio unaofanya mwili wote ufuate. Maana ni kwamba, jikite na jielekeze katika dini kwa kufuata maelekezo ya Allah na Mtume wake kwa ukamilifu.


Surata: YUNUS 

O versículo : 106

وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na usiombe (usiabudu) chochote badala ya Allah ambacho hakikunufaishi na hakikudhuru. Basi kama ukifanya hivyo, hakika wewe wakati huo utakuwa miongoni mwa madhalimu (wanaozidhulumu nafsi zao)



Surata: YUNUS 

O versículo : 107

وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يُرِدۡكَ بِخَيۡرٖ فَلَا رَآدَّ لِفَضۡلِهِۦۚ يُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Na kama Allah atakugusisha madhara (yoyote), basi hakuna yeyote wa kuyaondoa isipokuwa yeye tu na akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha (kuzuia) fadhila zake. (Allah) Anamlenga (anampa fadhila zake) amtakaye katika waja wake, na yeye tu ndiye Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu



Surata: YUNUS 

O versículo : 108

قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۖ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِوَكِيلٖ

Sema: Enyi watu, hakika imekujieni haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi yeyote anayeongoka, anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi kwa hakika anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si msaidizi kwenu



Surata: YUNUS 

O versículo : 109

وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَٱصۡبِرۡ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Na fuata yale yanayofunuliwa kwako, na kuwa na subira hadi Allah ahukumu. Na yeye (Allah) ni Bora zaidi ya wanaohukumu