Surata: HUUD 

O versículo : 61

۞وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱسۡتَعۡمَرَكُمۡ فِيهَا فَٱسۡتَغۡفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٞ مُّجِيبٞ

Na kwa watu wa Thamudi (tulimtuma) ndugu yao Swaleh. (Swaleh) alisema: Enyi watu wangu, mwabuduni Allah; Hamna nyinyi Mungu mwingine zaidi yake. Yeye ndiye aliyeanza kukuumbeni (kwakumuumba Adamu) kutoka ardhini, na akawaimarisheni humo, basi muombeni msamaha Yeye, kisha rudini kwake. Hakika Mola wangu mlezi yupo karibu sana, mpokeaji (wa maombi ya waja)



Surata: HUUD 

O versículo : 62

قَالُواْ يَٰصَٰلِحُ قَدۡ كُنتَ فِينَا مَرۡجُوّٗا قَبۡلَ هَٰذَآۖ أَتَنۡهَىٰنَآ أَن نَّعۡبُدَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ

Wakasema: Ewe Swaleh! Hakika ulikuwa mtu unayetegemewa sana kwetu kabla ya haya, hivi unatukataza kuabudu walichokiabudu baba zetu? Na kwa hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia



Surata: HUUD 

O versículo : 63

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي مِنۡهُ رَحۡمَةٗ فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِنۡ عَصَيۡتُهُۥۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيۡرَ تَخۡسِيرٖ

(Swaleh) akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje kama ninayo dalili kutoka kwa Mola wangu mlezi? Na amenipa rehema kutoka kwake, basi ni nani atakayeninusuru kwa Allah endapo nitamuasi? Basi hamtanizidishia chochote isipokuwa kunitia hasara tu



Surata: HUUD 

O versículo : 64

وَيَٰقَوۡمِ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٞ قَرِيبٞ

Na enyi watu wangu, huyu ni ngamia wa Allah ni ishara kwenu, basi mwacheni ale katika ardhi ya Allah, na msimguse kwa ubaya isije kuwashikeni adhabu iliyo karibu mno



Surata: HUUD 

O versículo : 65

فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُواْ فِي دَارِكُمۡ ثَلَٰثَةَ أَيَّامٖۖ ذَٰلِكَ وَعۡدٌ غَيۡرُ مَكۡذُوبٖ

Basi walimchinja; Na (Swaleh) akasema, stareheni majumbani mwenu kwa siku tatu; hiyo ni ahadi isiyokadhibishwa



Surata: HUUD 

O versículo : 66

فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ

Basi ilipokuja amri yetu tulimuokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu na kutokana na fedheha ya siku hiyo. Hakika Mola wako mlezi ndiye mwenye nguvu zaidi mwenye ushindi



Surata: HUUD 

O versículo : 67

وَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na ukelele ukawaangamiza wale waliodhulumu, na wakapambazukiwa wakiwa maiti ndani ya majumba yao



Surata: HUUD 

O versículo : 68

كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ

Kana kwamba hawakuwepo humo. Elewa! Hakika Thamud walimkufuru Mola wao mlezi. Eleweni! Maangamizi yawafike watu wa Thamudi



Surata: HUUD 

O versículo : 69

وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ

Na hakika walikuja wajumbe wetu kwa Ibrahimu kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: salama! Haukupita muda akaleta ndama wa kuchoma



Surata: HUUD 

O versículo : 70

فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ

Na pindi alipoona mikono yao haimfikii (ndama-hawali) aliwatilia shaka, na woga ukamuingia. (Malaika) Wakamwambia: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa watu wa Lutwi’



Surata: HUUD 

O versículo : 71

وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ

Na mkewe alikuwa kasimama, na akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa mtoto) Is-haq, na baada ya Is-haq Yakubu



Surata: HUUD 

O versículo : 72

قَالَتۡ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ ءَأَلِدُ وَأَنَا۠ عَجُوزٞ وَهَٰذَا بَعۡلِي شَيۡخًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عَجِيبٞ

(Mke wa Ibrahimu) akasema: Ee, hivi nitazaa kweli ilhali mimi ni kikongwe! Na mume wangu huyu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu sana!



Surata: HUUD 

O versículo : 73

قَالُوٓاْ أَتَعۡجَبِينَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۖ رَحۡمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٞ مَّجِيدٞ

(Malaika) wakasema: hivi, unastaajabu amri ya Allah? Rehema ya Allah na baraka zake ziko kwenu, watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ni Mwenye kusifiwaMwenye kutukuzwa



Surata: HUUD 

O versículo : 74

فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ

Na pindi hofu ilipomuondoka Ibrahimu, na ikamjia ile bishara (ya kupata mtoto), alianza kujadiliana nasi kuhusu watu wa Lutwi’



Surata: HUUD 

O versículo : 75

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّـٰهٞ مُّنِيبٞ

Hakika Ibrahimu alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Allah



Surata: HUUD 

O versículo : 76

يَـٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ

(Malaika walimwambia): Ewe Ibrahimu! Hili liache! Kwa hakika kabisa amri ya Mola wako mlezi imeshafika, na hakika hao itawafika adhabu isiyo rudi nyuma



Surata: HUUD 

O versículo : 77

وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ

Na pindi wajumbe wetu walipo kuja kwa Lutwi’ alijihisi huzuni na akawaonea dhiki. Na akasema: Hii leo ni siku ngumu sana!



Surata: HUUD 

O versículo : 78

وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ

Watu wake wakamjia mbio mbio. Na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Lutwi) akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa hapa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Allah, na msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Hivi, miongoni mwenu hakuna hata mmoja aliye na akili?



Surata: HUUD 

O versículo : 79

قَالُواْ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنۡ حَقّٖ وَإِنَّكَ لَتَعۡلَمُ مَا نُرِيدُ

Wakasema: Bila shaka unajua hatuna haki juu ya binti zako, na hakika unajua tunayoyataka



Surata: HUUD 

O versículo : 80

قَالَ لَوۡ أَنَّ لِي بِكُمۡ قُوَّةً أَوۡ ءَاوِيٓ إِلَىٰ رُكۡنٖ شَدِيدٖ

(Lutwi) akasema: Laiti mimi ningekuwa na nguvu ya kuwazuia, au ningekuwa na kabila na jamaa wenye nguvu tungepambana nanyi!



Surata: HUUD 

O versículo : 81

قَالُواْ يَٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓاْ إِلَيۡكَۖ فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٌ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمۡۚ إِنَّ مَوۡعِدَهُمُ ٱلصُّبۡحُۚ أَلَيۡسَ ٱلصُّبۡحُ بِقَرِيبٖ

(Malaika) wakasema: Ewe Lutwi›! Sisi ni wajumbe wa Mola wako mlezi, hawatakufikia. Na ondoka pamoja na watu wako katika kipande cha usiku uliobaki. Na yeyote miongoni mwenu asigeuke kutazama nyuma, isipokuwa mkeo itamfika adhabu (itakayowafika wengine). Hakika miadi yao ni asubuhi. Hivi, asubuhi si karibu?



Surata: HUUD 

O versículo : 82

فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ

Basi ilipofika amri yetu tulikigeza (kijiji kile) juu chini, na tukawateremshia mvua ya mawe kutoka Motoni



Surata: HUUD 

O versículo : 83

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ

(Mawe) yaliyotiwa alama maalumu kwa Mola wako mlezi. Na (mawe) hayo hayawakosi madhalimu



Surata: HUUD 

O versículo : 84

۞وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ وَلَا تَنقُصُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَۖ إِنِّيٓ أَرَىٰكُم بِخَيۡرٖ وَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ مُّحِيطٖ

Na kwa watu wa Madyana (tulimpeleka) ndugu yao Shuaib. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Allah pekee, hamna nyinyi Allah mwingine asiye kuwa Yeye. Na msipunguze vipimo vya ujazo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mpo katika hali nzuri (kimaisha). Na mimi nahofia kwenu adhabu katika Siku itakayowazunguka (kwa sababu ya kuwapunja watu)



Surata: HUUD 

O versículo : 85

وَيَٰقَوۡمِ أَوۡفُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ

Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo vya ujazo na mizani kwa uadilifu na msiwapunje watu vitu vyao; Na msiende huku na kule ardhini mkafanya uharibifu



Surata: HUUD 

O versículo : 86

بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ

(Kile) anachowabakishieni Allah (katika faida baada ya kutekeleza vipimo) ni bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. Na mimi sio mlinzi wenu



Surata: HUUD 

O versículo : 87

قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأۡمُرُكَ أَن نَّتۡرُكَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوۡ أَن نَّفۡعَلَ فِيٓ أَمۡوَٰلِنَا مَا نَشَـٰٓؤُاْۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلۡحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ

Wakasema: Ewe Shuaibu! Hivi (hizi) swala zako ndizo zinakuamuru tuache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu au tuache kufanya tupendayo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mpole sana na muongofu



Surata: HUUD 

O versículo : 88

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ

Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje kama nitakuwa na dalili kutoka kwa Mola wangu mlezi, na ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Na sipendi niwe kinyume na nyinyi nikafanya yale ninayowakatazeni. Sitaki ispokuwa kutengeneza kiasi niwezavyo. Na hakuna taufiki ispokuwa kwa Allah tu. Kwake tu nimetegemea na kwake tu nimerejea



Surata: HUUD 

O versículo : 89

وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ

Na enyi watu wangu! Kuacha kwangu dini yenu kusipelekee muwe wakaidi ikawa sababu ya nyinyi kupatwa na (adhabu) mfano wa iliyowapata watu wa Nuhu au watu wa Huud au watu wa Swaleh Na watu wa Lutwi kwenu hawako mbali



Surata: HUUD 

O versículo : 90

وَٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٞ وَدُودٞ

Na ombeni msamaha kwa Mola wenu mlezi, kisha rejeeni kwake. Hakika Mola wangu mlezi ni Mwenye kurehemu mwenye upendo