Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 271

إِن تُبۡدُواْ ٱلصَّدَقَٰتِ فَنِعِمَّا هِيَۖ وَإِن تُخۡفُوهَا وَتُؤۡتُوهَا ٱلۡفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمۡۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Iwapo mtadhihirisha sadaka ni vizuri sana, na kama mtatoa kwa siri na kuwapa mafukara basi hilo ni bora zaidi kwenu na atakufutieni baadhi ya maovu yenu na Allah anayajua mno mnayoyatenda



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 272

۞لَّيۡسَ عَلَيۡكَ هُدَىٰهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَلِأَنفُسِكُمۡۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ ٱللَّهِۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يُوَفَّ إِلَيۡكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تُظۡلَمُونَ

Si jukumu lako kuwaongoa, lakini Allah humuongoa amtakaye. Na heri yoyote muitoayo, basi ni kwa (manufaa ya) nafsi zenu. Na msitoe ila kwa kutafuta wajihi (radhi) za Allah, na heri yoyote mtakayotoa mtarudishiwa kamili, nanyi hamtadhulumiwa



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 273

لِلۡفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحۡصِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ ضَرۡبٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ يَحۡسَبُهُمُ ٱلۡجَاهِلُ أَغۡنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعۡرِفُهُم بِسِيمَٰهُمۡ لَا يَسۡـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلۡحَافٗاۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ

(Heri na sadaka hizo) Wapewe mafakiri waliofungwa katika njia ya Allah wasioweza kusafiri katika ardhi (kwa kujitafutia riziki), asiyewajua huwadhania ni wakwasi kwa kujizuia kuomba. Utawatambua kwa alama zao, hawawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na heri yoyote mnayoitoa, basi kwa hakika Allah anaijua sana



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 274

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 275

ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِي يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Wale wanaokula riba, hawatai-nuka isipokuwa kama anavyoinuka ambaye amepagawa kwa kukumbwa na Shetani. Hayo ni kwa sababu walisema kuwa biashara ni kama riba, na Allah ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Basi ambaye amefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake na akaacha, basi yake ni yale yaliyokwishapita, na jambo lake lipo kwa Allah. Na watakaorejea, basi hao ndio watu wa Motoni, wao watakaa humo milele



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 276

يَمۡحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰاْ وَيُرۡبِي ٱلصَّدَقَٰتِۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ

Allah huiondolea baraka riba na huzibariki sadaka, na Allah hampendi kila kafiri mno mwingi wa dhambi



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 277

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika wale walioamini na kutenda vitendo vizuri na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, wanamalipo mema mbele ya Mola wao, na hawana hofu yoyote, na hawahuzuniki



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 278

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Enyi mlioamini, mcheni Allah, na acheni yaliyobakia katika riba ikiwa ninyi ni waumini



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 279

فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ فَأۡذَنُواْ بِحَرۡبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَإِن تُبۡتُمۡ فَلَكُمۡ رُءُوسُ أَمۡوَٰلِكُمۡ لَا تَظۡلِمُونَ وَلَا تُظۡلَمُونَ

Na msipofanya (hivyo) basi tangazeni vita na Allah na Mtume wake, na kama mkitubu, basi ni stahiki yenu rasilimali zenu, hamtadhulumu wala hamtadhulumiwa



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 280

وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٖ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٖۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na kama (mdeni) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka wakati wa uwezo. Na kulifanya sadaka (hilo deni) ni heri kwenu (kuliko kungoja mpaka mdaiwa kupata uwezo), ikiwa mnajua



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 281

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na iogopeni siku ambayo mtarejeshwa kwa Allah, kisha kila mtu atalipwa kikamilifu aliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 282

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيۡنٍ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى فَٱكۡتُبُوهُۚ وَلۡيَكۡتُب بَّيۡنَكُمۡ كَاتِبُۢ بِٱلۡعَدۡلِۚ وَلَا يَأۡبَ كَاتِبٌ أَن يَكۡتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ ٱللَّهُۚ فَلۡيَكۡتُبۡ وَلۡيُمۡلِلِ ٱلَّذِي عَلَيۡهِ ٱلۡحَقُّ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥ وَلَا يَبۡخَسۡ مِنۡهُ شَيۡـٔٗاۚ فَإِن كَانَ ٱلَّذِي عَلَيۡهِ ٱلۡحَقُّ سَفِيهًا أَوۡ ضَعِيفًا أَوۡ لَا يَسۡتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلۡيُمۡلِلۡ وَلِيُّهُۥ بِٱلۡعَدۡلِۚ وَٱسۡتَشۡهِدُواْ شَهِيدَيۡنِ مِن رِّجَالِكُمۡۖ فَإِن لَّمۡ يَكُونَا رَجُلَيۡنِ فَرَجُلٞ وَٱمۡرَأَتَانِ مِمَّن تَرۡضَوۡنَ مِنَ ٱلشُّهَدَآءِ أَن تَضِلَّ إِحۡدَىٰهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحۡدَىٰهُمَا ٱلۡأُخۡرَىٰۚ وَلَا يَأۡبَ ٱلشُّهَدَآءُ إِذَا مَا دُعُواْۚ وَلَا تَسۡـَٔمُوٓاْ أَن تَكۡتُبُوهُ صَغِيرًا أَوۡ كَبِيرًا إِلَىٰٓ أَجَلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ أَقۡسَطُ عِندَ ٱللَّهِ وَأَقۡوَمُ لِلشَّهَٰدَةِ وَأَدۡنَىٰٓ أَلَّا تَرۡتَابُوٓاْ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَٰرَةً حَاضِرَةٗ تُدِيرُونَهَا بَيۡنَكُمۡ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَلَّا تَكۡتُبُوهَاۗ وَأَشۡهِدُوٓاْ إِذَا تَبَايَعۡتُمۡۚ وَلَا يُضَآرَّ كَاتِبٞ وَلَا شَهِيدٞۚ وَإِن تَفۡعَلُواْ فَإِنَّهُۥ فُسُوقُۢ بِكُمۡۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱللَّهُۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Enyi mliyoamini, mnapoko-peshana mkopo wowote kwa muda maalum, basi uandikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu. Na mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama Allah alivyomfunza. Hivyo basi, aandike na ni juu ya mdaiwa kutoa maneno ya kuandikwa na amwogope Allah, Mola wake Mlezi, na asipunguze chochote ndani yake. Na kama yule anayedaiwa ni alie pumbaa mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi msimamizi wake aandikishe kwa uadilifu. Na shuhudisheni mashahidi wawili wanaume waaminifu sana miongoni mwenu. Na iwapo hakuna wanaume wawili, basi (apatikane) mwanaume mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia kuwa mashahidi, ili kama atasahau mmoja wa wanawake wawili, yule mwingine amkumbushe mwenzake. Na mashahidi wasikatae wanapoitwa. Na msikimwe kuliandika deni, likiwa dogo au kubwa, mpaka muda wake. Jambo hilo kwenu ni uadilifu zaidi mbele ya Allah, na sahihi zaidi kwa ushahidi, na pia inakurubisha mno kutokuwa na shaka, isipokuwa kama ni biashara mnayofanya kati yenu papo hapo, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na mnapouziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi, na kama mkifanya hivyo (kuwatia matatani), basi kwa hakika huo ni uovu mkubwa kwenu. Na mwogopeni Allah, na Allah ndiye ana kuelimisheni; na Allah ni Mjuzi mno wa kila kitu



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 283

۞وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ

Na kama mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, basi (mdai) apewe (kitu) kiwe rehani mikononi mwake. Na kama mtaaminiana, basi aliyeaminiwa atekeleze uaminifu wake, na amche Allah, Mola wake Mlezi. Na msifiche ushahidi. Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Allah ni mwenye kuyajua mno yote mnayoyatenda



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 284

لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na kama mkidhihirisha yaliyomo katika nyoyo zenu, au mkiyaficha, Allah atakuhojini kwayo; kwahiyo atamsamehe amtakaye, na atamuadhibu amtakaye. Na Allah ni Mwenye uweza mno wa kila kitu



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 285

ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Mtume ameamini yote yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi na Waumini (pia wameamini hivyo). Kila mmoja amemwamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake. (Waumini na Mtume wao husema), “Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake (wote tunawaamini). Na husema: “Tumesikia na tumetii tunakuomba msamaha ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako tu



Surata: AL-BAQARAH 

O versículo : 286

لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَعَلَيۡهَا مَا ٱكۡتَسَبَتۡۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذۡنَآ إِن نَّسِينَآ أَوۡ أَخۡطَأۡنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تَحۡمِلۡ عَلَيۡنَآ إِصۡرٗا كَمَا حَمَلۡتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلۡنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦۖ وَٱعۡفُ عَنَّا وَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَآۚ أَنتَ مَوۡلَىٰنَا فَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Allah haikalifishi nafsi yoyote ila (kwa) iliwezalo. Itafaidika na mema iliyoyachuma na itadhurika na mabaya iliyoyachuma. (Waumini) wanasema: “(Ewe) Mola wetu Mlezi, usitutie hatiani kama tukisahahu (kutenda yaliyo mema) au tukikosea (kwa kutenda mabaya). (Ewe) Mola wetu Mlezi, na usitubebeshe mazito kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. (Ewe) Mola wetu Mlezi, usitubebeshe tusiyoyaweza, na tusamehe na tughufirie na turehemu. Wewe ndiye Mola wetu. Basi tusaidie dhidi ya watu makafiri