Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 1

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ ٱلظُّلُمَٰتِ وَٱلنُّورَۖ ثُمَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ

Kila sifa njema anazistahiki Allah ambaye ameumba mbingu na ardhi, na ameweka giza na mwanga, halafu waliomkufuru Mola wao, wanalinganisha (wanam-linganisha Allah na vitu vingine wanavyoviabudu na kuona kuwa viko sawa na Allah)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 2

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٖ ثُمَّ قَضَىٰٓ أَجَلٗاۖ وَأَجَلٞ مُّسَمًّى عِندَهُۥۖ ثُمَّ أَنتُمۡ تَمۡتَرُونَ

Yeye ndiye aliyekuumbeni kutokana na udongo, kisha ameweka muda (wa kila kiumbe wa kuishi), na muda uliotajwa (wa kila kiumbe kuondoka duniani) upo kwake tu, kisha nyinyi mnatia shaka



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 3

وَهُوَ ٱللَّهُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَفِي ٱلۡأَرۡضِ يَعۡلَمُ سِرَّكُمۡ وَجَهۡرَكُمۡ وَيَعۡلَمُ مَا تَكۡسِبُونَ

Na yeye ndiye Allah (mwenye haki ya kuabudiwa) mbinguni na ardhini. Anajua mambo yenu ya siri na ya dhahiri na anayajua mnayoyachuma (mnayoyafanya)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 4

وَمَا تَأۡتِيهِم مِّنۡ ءَايَةٖ مِّنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِمۡ إِلَّا كَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ

Na hakuna Aya yoyote inayowafikia katika alama za (uwepo wa) Mola wao isipokuwa wamekuwa wenye kuzipuuza



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 5

فَقَدۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَسَوۡفَ يَأۡتِيهِمۡ أَنۢبَـٰٓؤُاْ مَا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Kwa hakika, wameikataa haki ilipowafikia. Basi ni punde tu zitawajia habari za yale waliyokuwa wanayabeza



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 6

أَلَمۡ يَرَوۡاْ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٖ مَّكَّنَّـٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَا لَمۡ نُمَكِّن لَّكُمۡ وَأَرۡسَلۡنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡهِم مِّدۡرَارٗا وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَنۡهَٰرَ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِينَ

Hivi hawakuona; ni karne ngapi tumeziangamiza kabla yao? Tuliwapa uwezo mkubwa ardhini ambao (nyinyi) hatujakupeni (uwezo kama huo), na tuliwapelekea mawingu yanayotiririsha mvua nyingi (za heri) na tulifanya mito ikipita chini yao. Tuliwaangamiza kwa (sababu ya) madhambi yao na tukaanzisha baada yao karne nyingine



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 7

وَلَوۡ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ كِتَٰبٗا فِي قِرۡطَاسٖ فَلَمَسُوهُ بِأَيۡدِيهِمۡ لَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na lau kama tungekuteremshia kitabu (kikiwa) katika (mfumo wa) karatasi na wakakigusa kwa mikono yao, hakika kabisa waliokufuru wangesema: Hayakuwa haya isipokuwa ni uchawi wa wazi



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 8

وَقَالُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ مَلَكٞۖ وَلَوۡ أَنزَلۡنَا مَلَكٗا لَّقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ

Na walisema: lau angeteremshiwa Malaika. Na lau tungeteremsha Malaika, kwa hakika kabisa, jambo lingehukumiwa, kisha wasingesubirishwa (wasingepewa muda wa kusubiri)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 9

وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ مَلَكٗا لَّجَعَلۡنَٰهُ رَجُلٗا وَلَلَبَسۡنَا عَلَيۡهِم مَّا يَلۡبِسُونَ

Na lau tungemfanya Mtume Malaika tungemfanya mwanaume na tungewavalisha (tungewachanganya) yale wanayoyavaa (wanayojichan-ganya)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 10

وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na kwa hakika kabisa, walibezwa Mitume waliokuwepo kabla yako, na kwa sababu hiyo, wale waliowabeza (Mitume) yaliwashukia yale waliyokuwa wakiyabeza (na kuangamizwa)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 11

قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ ٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Sema: Tembeeni ardhini kisha tazameni namna ulivyokuwa mwisho wa wenye kukadhibisha (wenye kupinga)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 12

قُل لِّمَن مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُل لِّلَّهِۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allah. Amejithibitishia rehema. Kwa yakini kabisa, atakukusanyeni Siku ya Kiama isiyokuwa na shaka. Waliozitia hasara nafsi zao, hawaamini



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 13

۞وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِي ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na ni milki yake (Allah) tu vyote vilivyotulia usiku na mchana, na yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi sana



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 14

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hivi nimfanye asiyekuwa Allah mwandani (Allah ambaye ni) Muumba wa mbingu na ardhi, na yeye ndiye analisha na halishwi? Sema: Hakika, mimi nimeamrishwa kuwa Muislamu wa kwanza (muumini wa kwanza wa haya ninayowaambia), na wewe kamwe usiwe katika washirikina



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 15

قُلۡ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Sema: Hakika, mimi naogopa adhabu ya Siku Kubwa ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 16

مَّن يُصۡرَفۡ عَنۡهُ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمَهُۥۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡمُبِينُ

Atakaye epushwa na adhabu Siku hiyo, hakika (Allah atakuwa) amemrehemu, na huko ndio kufaulu kuliko dhahiri kabisa



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 17

وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يَمۡسَسۡكَ بِخَيۡرٖ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na ikiwa Allah atakushikisha madhara yoyote, basi hakuna wa kuyatatua isipokuwa yeye tu. Na ikiwa atakushikisha kheri yoyote, basi yeye ni Muweza wa kila jambo



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 18

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Na yeye ni Mwenye nguvu juu ya waja wake, na yeye ni Mwenye hekima nyingi, Mwenye habari zote (za kila jambo)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 19

قُلۡ أَيُّ شَيۡءٍ أَكۡبَرُ شَهَٰدَةٗۖ قُلِ ٱللَّهُۖ شَهِيدُۢ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ لِأُنذِرَكُم بِهِۦ وَمَنۢ بَلَغَۚ أَئِنَّكُمۡ لَتَشۡهَدُونَ أَنَّ مَعَ ٱللَّهِ ءَالِهَةً أُخۡرَىٰۚ قُل لَّآ أَشۡهَدُۚ قُلۡ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ وَإِنَّنِي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ

Sema: Ni kitu gani kikubwa zaidi kwa ushahidi? Sema: Allah ni Shahidi sana baina yangu na baina yenu. Na nimeletewa Wahyi wa hii Qur’ani ili nikuonyeni kwayo na yeyote itakayomfikia. Je, hivi nyinyi, kwa hakika kabisa, mnashuhudia kwamba pamoja na Allah kuna Miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii (hilo). Sema: Hakika ni kwamba, yeye ni Mungu Mmoja tu na mimi simo kwenye yote mnayomshirikisha (nayo Allah)



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 20

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمُۘ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Ambao tuliwapa Kitabu wanamjua (Mtume Muhammad) kama wanavyowajua watoto wao. Ambao waliozitia hasara nafsi zao hawaamini



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 21

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia uongo Allah au aliyezipinga Aya zake? Hakika ni kuwa, madhalimu hawafaulu



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 22

وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُوٓاْ أَيۡنَ شُرَكَآؤُكُمُ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ

Na (kumbuka) siku tutakapowa-kusanya wote kisha tuwaambie wale washirikina (kwamba): Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwa ni washirika wa Allah)?



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 23

ثُمَّ لَمۡ تَكُن فِتۡنَتُهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ وَٱللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشۡرِكِينَ

Kisha haukuwa mtihani wao isipokuwa kwamba walisema tu: Ewe Mola wetu tunaapa; sisi hatukuwa Washirikina



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 24

ٱنظُرۡ كَيۡفَ كَذَبُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡۚ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Ona namna walivyozidanganya nafsi zao na yakawapotea yote waliyokuwa wanayazua



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 25

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُ إِلَيۡكَۖ وَجَعَلۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ أَكِنَّةً أَن يَفۡقَهُوهُ وَفِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٗاۚ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوكَ يُجَٰدِلُونَكَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na miongni mwao wapo wanaokusikiliza na tumeweka juu ya nyoyo zao vifuniko wasiyafahamu (hayo wanayoyasikia) na katika masikio yao (tumeweka) uziwi. Na wanapoona kila Aya (inayoteremka kusadikisha Utume wako) hawaiamini mpaka wanapokujia wanakufanyia mjadala wakisema wale waliokufuru kwamba: (Haya anayoyasema) sio chochote isipokuwa tu ni hadithi za kale



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 26

وَهُمۡ يَنۡهَوۡنَ عَنۡهُ وَيَنۡـَٔوۡنَ عَنۡهُۖ وَإِن يُهۡلِكُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Na wanakataza (watu kuiamini Qur’ani) na (wao wenyewe) wanajitenga nayo. Na hawaangamizi isipokuwa nafsi zao tu, na hawatambui



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 27

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُواْ يَٰلَيۡتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na lau ungeona wakati watakaposimamishwa motoni na kusema (kwa majuto): Eee! Laiti tungerudishwa (duniani) na tusizikanushe Aya za Mola wetu Mlezi na tuwe miongoni mwa Waumini



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 28

بَلۡ بَدَا لَهُم مَّا كَانُواْ يُخۡفُونَ مِن قَبۡلُۖ وَلَوۡ رُدُّواْ لَعَادُواْ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wanayaficha kabla ya hapo. Na lau kama wangerudishwa, kwa yakini kabisa wangerudia yale waliyokatazwa. Na kwa hakika kabisa wao ni waongo



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 29

وَقَالُوٓاْ إِنۡ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنۡيَا وَمَا نَحۡنُ بِمَبۡعُوثِينَ

Na walisema: Hayakuwa haya (maisha) isipokuwa tu ni maisha yetu ya duniani, na sisi si wenye kufufuliwa



Surata: AL-AN’AAM 

O versículo : 30

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ قَالَ أَلَيۡسَ هَٰذَا بِٱلۡحَقِّۚ قَالُواْ بَلَىٰ وَرَبِّنَاۚ قَالَ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Na lau kama utawaona wakati watakaposimamishwa kwa Mola wao atasema Allah na kuwaambia): Hivi hili (la kufufuliwa) sio kweli? Watasema: Tunaapa kwa Mola wetu (kwamba ni kweli). (Allah) Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayapinga