۞لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقۡرَبَهُم مَّوَدَّةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنۡهُمۡ قِسِّيسِينَ وَرُهۡبَانٗا وَأَنَّهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ
Hakika kabisa, utakuta watu walio na uadui mkubwa na Waislamu ni Wayahudi na washirikishaji (wanaomfanyia ushirika Allah). Na kwa hakika kabisa, utakuta (watu) walio karibu nao zaidi ni wale wanaosema: Sisi ni Wanaswara (Wakristo). Hayo ni kwasababu miongoni mwao wapo Makasisi na Watawa, na kwasababu wao hawafanyi kiburi (katika kuifuata haki)
وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanabubujika machozi kwasababu ya haki waliyoitambua. Wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi, tumeamini; basi tuandike (tuwe) pamoja na wanaoshuhudia (Uungu wako, upekee wako na kuabudiwa kwako)
وَمَا لَنَا لَا نُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡحَقِّ وَنَطۡمَعُ أَن يُدۡخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na kwanini tusimuamini Allah na haki iliyotujia (Qur’an) Na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema?
فَأَثَٰبَهُمُ ٱللَّهُ بِمَا قَالُواْ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Basi Allah, kwa yale waliyo yasema, amewalipa Pepo zipitazo mito mbele yake watadumu humo milele. Na hayo ndiyo malipo ya wafanyao mazuri
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Na wale waliokufuru na wakazi-kufuru Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحَرِّمُواْ طَيِّبَٰتِ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ
Enyi mlioamini, msiharimishe vizuri alivyokuhalalishieni Allah, na msikiuke mipaka. Hakika, Allah hawapendi wakiukao mipaka
وَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ
Na kuleni katika alivyoku-ruzukuni Allah vilivyo halali, vizuri. Na mcheni Allah ambaye Yeye tu mnamuamini
لَا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ ٱلۡأَيۡمَٰنَۖ فَكَفَّـٰرَتُهُۥٓ إِطۡعَامُ عَشَرَةِ مَسَٰكِينَ مِنۡ أَوۡسَطِ مَا تُطۡعِمُونَ أَهۡلِيكُمۡ أَوۡ كِسۡوَتُهُمۡ أَوۡ تَحۡرِيرُ رَقَبَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖۚ ذَٰلِكَ كَفَّـٰرَةُ أَيۡمَٰنِكُمۡ إِذَا حَلَفۡتُمۡۚ وَٱحۡفَظُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Allah hakuchukulieni hatua kwa viapo vyenu vya kipuuzi, lakini anakuchukulieni hatua kwa (viapo) mlivyovikusudia kweli kweli. Basi Kafara (adhabu) yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacholisha familia zenu au kuwavalisha (kuwapa nguo) au kumkomboa mtumwa. Asiyepata hayo, basi afunge siku tatu. Hiyo ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini (lindeni) viapo vyenu. Namna hivyo Allah anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Enyi mlioamini, ilivyo ni kwamba, ulevi na kamari na masanamu na Ramli ni uchafu utokanao na vitendo vya Shetani, basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu
إِنَّمَا يُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُوقِعَ بَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ فِي ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِ وَيَصُدَّكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَعَنِ ٱلصَّلَوٰةِۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّنتَهُونَ
Ilivyo ni kwamba, Shetani anataka kuweka uadui na chuki baina yenu kwasababu ya ulevi na kamari, na kukuzuieni kumkumbuka Allah na kuswali. Basi je, mmeacha?
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَٱحۡذَرُواْۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na mtiini Allah na mtiini Mtume, na jihadharini (na dhambi). Na mkikengeuka basi jueni ya kuwa jukumu la Mtume wetu ni kufikisha ujumbe wenye kufafanua
لَيۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ جُنَاحٞ فِيمَا طَعِمُوٓاْ إِذَا مَا ٱتَّقَواْ وَّءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ ثُمَّ ٱتَّقَواْ وَّءَامَنُواْ ثُمَّ ٱتَّقَواْ وَّأَحۡسَنُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakuna dhambi kwa walioamini na wakatenda mema katika walivyovila madamu wakimcha Allah na wakaamini na wakatenda mema, kisha wakamcha Allah na wakaamini kisha wakamcha Allah na wakafanya mazuri. Na Allah anawapenda wafanyao mazuri
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَيَبۡلُوَنَّكُمُ ٱللَّهُ بِشَيۡءٖ مِّنَ ٱلصَّيۡدِ تَنَالُهُۥٓ أَيۡدِيكُمۡ وَرِمَاحُكُمۡ لِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ مَن يَخَافُهُۥ بِٱلۡغَيۡبِۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Enyi mlioamini, Allah atawa-jaribuni kwa baadhi ya wanyamapori wafikiwao na mikono yenu na mikuki yenu, ili Allah amjue nani anayemuhofu kwa ghaibu. Basi atakayechupa mipaka baada ya hayo atapata adhabu iumizayo mno
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡتُلُواْ ٱلصَّيۡدَ وَأَنتُمۡ حُرُمٞۚ وَمَن قَتَلَهُۥ مِنكُم مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآءٞ مِّثۡلُ مَا قَتَلَ مِنَ ٱلنَّعَمِ يَحۡكُمُ بِهِۦ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ هَدۡيَۢا بَٰلِغَ ٱلۡكَعۡبَةِ أَوۡ كَفَّـٰرَةٞ طَعَامُ مَسَٰكِينَ أَوۡ عَدۡلُ ذَٰلِكَ صِيَامٗا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمۡرِهِۦۗ عَفَا ٱللَّهُ عَمَّا سَلَفَۚ وَمَنۡ عَادَ فَيَنتَقِمُ ٱللَّهُ مِنۡهُۚ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ
Enyi mlioamini, msiue wanya-mapori na hali mmeharimia (mmo ndani ya ibada ya Hija au Umra). Na yeyote miongoni mwenu atakayemuua mnyama huyo kwa makusudi, basi malipo (yake) ni (kuchinja) mnyama wa kufuga mfano wa aliyemuua. Watahukumu hayo waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama (huyo) apelekwe Al-Kaaba (Makkah ili achinjwe huko na nyama yake kugaiwa sadaka kwa maskini wa huko) au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini au badala ya hayo ni kufunga ili (aliyefanya kosa hilo la kuwinda) aonje ubaya wa jambo lake (baya alilolifanya). Allah amekwishafuta yaliyopita (lakini) atakayerudia (kufanya tena kosa hilo) Allah atamuadhibu. Na Allah ni Mwenye nguvu sana, Mwenye kutesa
أُحِلَّ لَكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَحۡرِ وَطَعَامُهُۥ مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِلسَّيَّارَةِۖ وَحُرِّمَ عَلَيۡكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَرِّ مَا دُمۡتُمۡ حُرُمٗاۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ
Mmehalalishiwa viwindwa vya baharini (uvuvi) na kuvila kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa viwindwa vya bara (nchi kavu) madhali mmehirimia (mmo ndani ya ibada ya Hija au Umra). Na mcheni Allah ambaye kwake mtakusanywa
۞جَعَلَ ٱللَّهُ ٱلۡكَعۡبَةَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ قِيَٰمٗا لِّلنَّاسِ وَٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَٱلۡهَدۡيَ وَٱلۡقَلَـٰٓئِدَۚ ذَٰلِكَ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ
Allah ameifanya Al-Kaaba, Nyumba Tukufu kuwa tegemeo la watu, na kadhalika (ameifanya) Miezi Mitukufu (tegemeo kwa kusitishwa vita) na wanyama wa hadiyi (dhabihu) waliovikwa koja. (Allah amefanya) Hayo ili mjue kwamba Allah anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini, na kwamba Allah ni Mjuzi wa kila kitu
ٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ وَأَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Jueni kwamba, Allah ni Mkali wa kuadhibu, na kwamba Allah ni Mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu
مَّا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا تَكۡتُمُونَ
Si juu ya Mtume isipokuwa kufikisha ujumbe tu. Na Allah anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha
قُل لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡخَبِيثُ وَٱلطَّيِّبُ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ كَثۡرَةُ ٱلۡخَبِيثِۚ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Sema: Haliwi sawa baya na jema na hata kama wingi wa baya utakuvutia. Basi mcheni Allah, enyi wenye akili, ili mpate kufanikiwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ
Enyi mlioamini, msiulize mambo (ambayo) mkidhihirishiwa yanakuchukizeni. Na mkiyauliza wakati Qur’ani inateremshwa mtadhihirishiwa. (Msirudie) Allah ameshayasamehe hayo (mliyokwishauliza). Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno
قَدۡ سَأَلَهَا قَوۡمٞ مِّن قَبۡلِكُمۡ ثُمَّ أَصۡبَحُواْ بِهَا كَٰفِرِينَ
Hakika, waliyauliza hayo watu (waliokuwepo) kabla yenu, kisha wakawa ni wenye kuyapinga
مَا جَعَلَ ٱللَّهُ مِنۢ بَحِيرَةٖ وَلَا سَآئِبَةٖ وَلَا وَصِيلَةٖ وَلَا حَامٖ وَلَٰكِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَأَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ
Allah hakuweka uharamu (wowote) katika Bahira[1] wala Saiba[2] wala Waswila[3] wala Hami.[4] Na lakini wale waliokufuru wanamzushia Allah uwongo, na wengi wao hawatumii akili
1- - Bahira ni jina la ngamia jike aliyetogwa masikio na kuachwa huru aende malishoni bila ya mchungaji.
Wapagani wa Kikuraishi na hasa kabila la Khuzaa walimtukuza Ngamia huyu na kumfanya maalumu kwa
ajili ya ibada za masanamu; habebeshwi kitu mgongoni kwake, ngozi yake haitiwi alama na maziwa
yake hunywewa na mgeni tu.
2- - Saiba ni ngamia aliyewekwa nadhiri kwa ajili ya masanamu pindi mtu anaposalimika na maradhi
au kupata hadhi fulani. Ngamia huyu pia aliachwa huru aende malishoni bila ya mchungaji na ilikuwa
marufuku kupandwa na yeyote, isipokuwa haikatazwi kumtumia katika kubeba majani ya malisho na utekaji maji.
3- - Waswila katika ngamia ni ngamia jike aliyeachwa huru. Na Waswila katika mbuzi au kondoo ni yule
aliyezaa majike kwa mfululizo.
4- - Hami ni fahali (dume) la ngamia lililozalisha zao nyingi na kuzeeka. Halipandwi kama chombo cha usafiri wala halibebeshwi mizigo na huachwa huru kwenda machungani bila ya mchungaji.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُواْ حَسۡبُنَا مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ
Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allah, na kwa Mtume, wanasema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, (wanafuata waliyoyakuta kwa baba zao) hata kama baba zao hao hawajui kitu na hawana muongozo?
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَيۡكُمۡ أَنفُسَكُمۡۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهۡتَدَيۡتُمۡۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Enyi mlioamini, zijalini nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotea ikiwa nyinyi mmeongoka. Kwa Allah tu ndio marejeo yenu nyote; basi atakuambieni yale yote mliyokuwa mnayatenda
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ شَهَٰدَةُ بَيۡنِكُمۡ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ حِينَ ٱلۡوَصِيَّةِ ٱثۡنَانِ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ أَوۡ ءَاخَرَانِ مِنۡ غَيۡرِكُمۡ إِنۡ أَنتُمۡ ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَأَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةُ ٱلۡمَوۡتِۚ تَحۡبِسُونَهُمَا مِنۢ بَعۡدِ ٱلصَّلَوٰةِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ لَا نَشۡتَرِي بِهِۦ ثَمَنٗا وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰ وَلَا نَكۡتُمُ شَهَٰدَةَ ٱللَّهِ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلۡأٓثِمِينَ
Enyi mlioamini, ushahidi wa baina yenu kinapomfikia mmoja wenu kifo wakati wa kuusia ni (mashahidi) wawili waadilifu miongoni mwenu au wawili wengine wasiokuwa katika nyinyi, mnapokuwa safarini na ukakusibuni msiba wa kifo. Mtawazuia wawili hao baada ya Swala. Waape kwa (jina la) Allah mkiwa na shaka (wakisema): Hatununui (hatupokei) thamani yoyote kwa haya (tunayoyatolea ushahidi) hata kama (tunaowatolea ushahidi dhidi yao) wakiwa ndugu wa nasaba, na hatufichi ushahidi wa Allah. Hakika, sisi tukifanya hivyo kwa yakini kabisa tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi
فَإِنۡ عُثِرَ عَلَىٰٓ أَنَّهُمَا ٱسۡتَحَقَّآ إِثۡمٗا فَـَٔاخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَحَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَوۡلَيَٰنِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ لَشَهَٰدَتُنَآ أَحَقُّ مِن شَهَٰدَتِهِمَا وَمَا ٱعۡتَدَيۡنَآ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ikigundulika kwamba, (mashahidi) wawili hao wametenda dhambi, basi (mashahidi) wawili wengine watasimama mahali pa wale wa mwanzo; hivyo wataapa kwa (jina la) Allah (kwamba): Hakika kabisa, ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wale wawili (wa kwanza) na hatujachupa mipaka; Hakika, wakati huo (tutakapoficha Ushahidi) sisi kwa yakini kabisa tutakuwa miongoni mwa madhalimu
ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِٱلشَّهَٰدَةِ عَلَىٰ وَجۡهِهَآ أَوۡ يَخَافُوٓاْ أَن تُرَدَّ أَيۡمَٰنُۢ بَعۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡمَعُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Hilo linaelekea karibu zaidi watoe ushahidi kwa usahihi wake au wahofie viapo kukataliwa baada ya viapo vyao. Na mcheni Allah na sikieni. Na hakika, Allah hawaongoi watu waovu
۞يَوۡمَ يَجۡمَعُ ٱللَّهُ ٱلرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَآ أُجِبۡتُمۡۖ قَالُواْ لَا عِلۡمَ لَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Siku Allah atakapowakusanya Mitume na kuwaambia: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui; hakika Wewe tu ndiye Mjuzi mno wa yote yaliyofichikana
إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱذۡكُرۡ نِعۡمَتِي عَلَيۡكَ وَعَلَىٰ وَٰلِدَتِكَ إِذۡ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِ تُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗاۖ وَإِذۡ عَلَّمۡتُكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَۖ وَإِذۡ تَخۡلُقُ مِنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ بِإِذۡنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِيۖ وَتُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ تُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ كَفَفۡتُ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ عَنكَ إِذۡ جِئۡتَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
(kumbuka) Pale Allah aliposema: Ewe Issa bin Mariamu, kumbuka neema yangu kwako na kwa mama yako, nilipokutia nguvu kwa Roho Mtakatifu (Jibrili), ukazungumza na watu katika utoto na ukiwa mtumzima. Na (kumbuka) nilivyokufundisha kitabu na hekima na Taurati na Injili, na wakati unaunda kutokana na udongo mfano wa ndege kwa idhini yangu, kisha unapuliza katika mfano huo na wakawa ndege kwa idhini yangu, na (kumbuka) ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini yangu, na (kumbuka) wakati unawafufua wafu kwa idhini yangu. Na (kumbuka) nilipowazuia Wana wa Israili wasikudhuru ulipowaendea na hoja zilizo wazi, wakasema waliokufuru miongoni mwao (kwamba): Haya (aliyoyaleta Issa) si lolote isipokuwa tu ni uchawi mtupu!
وَإِذۡ أَوۡحَيۡتُ إِلَى ٱلۡحَوَارِيِّـۧنَ أَنۡ ءَامِنُواْ بِي وَبِرَسُولِي قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَٱشۡهَدۡ بِأَنَّنَا مُسۡلِمُونَ
Na (kumbuka) nilipowafunulia Hawariyyina (wanafunzi wa karibu wa Nabii Issa) kwamba: Niaminini Mimi na Mtume wangu. Walisema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu