وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ
Na nini hicho kilichomo katika mkono wako wa kulia, ewe Mussa?
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ
Akasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine
قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ
(Allah) Akasema: Basi iangushe ewe Mussa
فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ
Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio
قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ
Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza
وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ
Na ukumbatie mkono wako kwenye ubavu wako. Utatoka mweupe pasipo kuwa na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyengine
لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى
Ili tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka
قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي
(Mussa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي
Na uifanye kazi yangu (kuwa) nyepesi,
وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي
Wapate kufahamu maneno yangu
وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي
Na nipe waziri katika watu wangu,
هَٰرُونَ أَخِي
Harun, ndugu yangu
ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي
Kwake yeye niongeze nguvu zangu
وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي
Na umshirikishe katika kazi yangu
كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا
Ili tukutakase sana
وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا
Na tukukumbuke sana
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا
Hakika Wewe unatuona
قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ
Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Mussa!
وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ
Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine
إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ
Pale tulipo mfunulia mama yako yaliyo funuliwa,
أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوّٞ لِّي وَعَدُوّٞ لَّهُۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةٗ مِّنِّي وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِيٓ
Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayotoka kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu
إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّـٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ
Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madiyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Mussa!
وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِي
Na nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu
ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَٰتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكۡرِي
Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka
ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka
فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa
قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ
Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri
قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِي مَعَكُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ
Akasema: Msiogope! Hakika Mimi nipo pamoja nanyi. Nasikia na ninaona