يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينًا
Enyi mlioamini, msiwafanye makafiri marafiki wa ndani badala ya Waumini (wenzenu). Je, mnataka Allah awe na hoja iliyo wazi kwenu (kwamba nyinyi ni waovu na kustahiki adhabu kwa kuwapenda makafiri badala ya Waislamu wenzenu)?
إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا
Hakika, wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa la Moto, na hutampata yeyote wa kuwanusuru
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Isipokuwa wale waliotubu (unafiki wao) na wakatengeneza (wakarekebisha na kusahihisha itikadi na misimamo yao mibovu) na wakashikamana na (sheri za) Allah na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Allah. Basi hao watakuwa pamoja na waumini. Na Allah atawapa waumini ujira mkubwa sana
مَّا يَفۡعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمۡ إِن شَكَرۡتُمۡ وَءَامَنتُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمٗا
Allah hatakuadhibuni iwapo mtashukuru na kuamini, na Allah ndiye Mwenye kupokea shukurani na ndiye Mjuzi sana