وَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٌ أَنۡ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَجَٰهِدُواْ مَعَ رَسُولِهِ ٱسۡتَـٔۡذَنَكَ أُوْلُواْ ٱلطَّوۡلِ مِنۡهُمۡ وَقَالُواْ ذَرۡنَا نَكُن مَّعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ
Na inapoteremshwa Sura (inayowaamrisha) kwamba: Muaminini Allah na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye uwezo (wa mali na nguvu) miongoni mwao wanakuomba ruhusa na kusema: Tuache tuwe pamoja na wanaokaa nyuma
رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ
Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma (wenye nyudhuru), na nyoyo zao zikapigwa chapa kwa hivyo hawafahamu
لَٰكِنِ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ جَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ وَأُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡخَيۡرَٰتُۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Lakini Mtume na wale walioamini pamoja naye walipigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na hao ndio watakaopata heri nyingi na hao ndio hasa wenye kufaulu
أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Allah amewaandalia Pepo zipitazo mito mbele yake wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa hasa
وَجَآءَ ٱلۡمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ لِيُؤۡذَنَ لَهُمۡ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na walikuja wenye kujitia udhuru katika Mabedui ili wapewe ruhusa (ya kutokwenda vitani), na walikaa wale (wanafiki) waliomwambia uwongo Allah na Mtume wake. Itawafika (wale) waliokufuru katika wao (na kusema uongo) adhabu iumizayo sana
لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakuna dhambi kwa wanyonge na wagonjwa na wasiokuwa na cha kutoa, iwapo wanamsafia nia Allah na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye Rehemu
وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوۡكَ لِتَحۡمِلَهُمۡ قُلۡتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحۡمِلُكُمۡ عَلَيۡهِ تَوَلَّواْ وَّأَعۡيُنُهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُواْ مَا يُنفِقُونَ
Na wala (hawana dhambi) wale (Answari) ambao walipokujia ili uwachukue (uwawezeshe na uwape vipando vya kwendea jihadi) ulisema: Sina kipando cha kukuchukueni (cha kukupeni) waliondoka na ilhali macho yao yanatiririka machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa