السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 202

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّمَّا كَسَبُواْۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hao wanalo fungu katika waliyoyachuma. Na Allah ni Mwepesi wa kuhesabu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 203

۞وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ فِيٓ أَيَّامٖ مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Na mtajeni Allah katika siku chache. Atakayefanya haraka[1] ndani ya siku mbili, basi hakuna dhambi yoyote kwake. Na atakayechelewa hakuna dhambi kwake; kwa mwenye kumcha Allah. Na mcheni Allah najueni kuwa bila ya shaka nyinyi mtakusanywa kwake tu


1- - Kuondoka Mina


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 204

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao zinakuvutia kauli zao katika maisha ya dunia, na wanamshuhudisha Allah juu ya yaliyo moyoni mwake hali yeye ni mpingaji mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 205

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ

Na anapoondoka (kwako) anahangaika huku na kule ardhini ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na vizazi. Na Allah hapendi ufisadi



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 206

وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Na wanapoambiwa; Muogopeni Allah hupandwa na mori wa kufanya uovu. Basi kitakachowatosha ni Jahanamu na ni makazi mabaya mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 207

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡرِي نَفۡسَهُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao huuza nafsi zao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah na Allah ni Mpole sana kwa waja



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 208

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِي ٱلسِّلۡمِ كَآفَّةٗ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Enyi mlioamini, ingieni kwenye Uislamu wote (wazima wazima), na msifuate nyayo za shetani, hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 209

فَإِن زَلَلۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡكُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Na kama mtateleza[1] baada ya kukujieni hoja za wazi, basi jueni kwamba, Allah ni mwenye nguvu nyingi mwingi wa hekima


1- - Kwa kuacha baadhi ya sheria na hukumu


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 210

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِي ظُلَلٖ مِّنَ ٱلۡغَمَامِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Hakuna wanachongojea isipokuwa kuwajia Allah na Malaika kwenye vivuli vya mawingu na jambo lishakatiwa shauri. Na kwa Allah pekee ndipo yanaporudishwa mambo



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 211

سَلۡ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ كَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّنۡ ءَايَةِۭ بَيِّنَةٖۗ وَمَن يُبَدِّلۡ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Waulize Wana wa Israili: Ni Aya ngapi zilizo wazi tumewapa? Na yeyote atakayebadili neema za Allah baada ya kumfikia, kwa hakika Allah ni Mkali wa kuadhibu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 212

زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَيَسۡخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ

Makafiri wamepambiwa maisha ya dunia, na wanawadharau walioamini. Na Wacha Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiama. Na Allah anamruzuku amtakaye bila ya hesabu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 213

كَانَ ٱلنَّاسُ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَبَعَثَ ٱللَّهُ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَ ٱلنَّاسِ فِيمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَمَا ٱخۡتَلَفَ فِيهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ أُوتُوهُ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۖ فَهَدَى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ ٱلۡحَقِّ بِإِذۡنِهِۦۗ وَٱللَّهُ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٍ

Watu walikuwa umma mmoja. Allah akatuma Mitume wakitoa habari njema na wakitoa maonyo na aliteremsha vitabu pamoja nao kwa haki ili ahukumu kati ya watu katika yale ambayo wametofatiana. Na hawakutofautiana katika hayo isipokuwa wale tu waliopewa vitabu hivyo, baada ya kuwafikia hoja za waziwazi kwa sababu tu ya uovu walionao. Basi Allah akawaongoza wale ambao wameamini kwenye haki kwa idhini yake na Allah anamuongoza amtakaye kwenye njia iliyo nyooka



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 214

أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۖ مَّسَّتۡهُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ

Je, mmedhani kuwa mtaingia peponi ilhali haujakufikeni mfano wa ambao wamepita kabla yenu? Yaliwapata misukosuko na madhara na walitetemeshwa hadi akasema Mtume na walioamini pamoja naye kwamba: Ni lini itafika nusura ya Allah? Eleweni kwamba, hakika nusura ya Allah iko karibu mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 215

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلۡ مَآ أَنفَقۡتُم مِّنۡ خَيۡرٖ فَلِلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

Wanakuuliza: Watoe nini? Sema: Chochote cha heri mtakachotoa basi wapeni wazazi na ndugu na Mayatima na masikini na Msafiri na heri yoyote muifanyayo kwa hakika Allah anaijua mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 216

كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ شَرّٞ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Imefaradhishiwa kwenu kupigana vita na ilihali ni jambo msilolipenda. Na huenda mkachukia kitu na ilhali ni heri kwenu. Na huenda mkapenda kitu na ilhali ni shari kwenu. Na Allah anajua na ilhali nyinyi hamjui



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 217

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ قِتَالٖ فِيهِۖ قُلۡ قِتَالٞ فِيهِ كَبِيرٞۚ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَكُفۡرُۢ بِهِۦ وَٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ وَإِخۡرَاجُ أَهۡلِهِۦ مِنۡهُ أَكۡبَرُ عِندَ ٱللَّهِۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَكۡبَرُ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمۡ عَن دِينِكُمۡ إِنِ ٱسۡتَطَٰعُواْۚ وَمَن يَرۡتَدِدۡ مِنكُمۡ عَن دِينِهِۦ فَيَمُتۡ وَهُوَ كَافِرٞ فَأُوْلَـٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Wanakuuliza kuhusu kupigana ndani ya mwezi mtukufu. Sema: Kupigana vita humo ni dhambi kubwa. Na kuzuia (watu) katika njia ya Allah na kumkufuru Allah na kuzuia (watu kutumia) Msikiti Mtukufu na kuwatoa humo watu wake ni dhambi kubwa zaidi mbele ya Allah na fitina ni dhambi kubwa mno kuliko kuua. Na hawataacha kukupigeni mpaka wakurudisheni muiache dini yenu kama wataweza. Na yeyote atakaye rudi nyuma akaiacha dini yake miongoni mwenu na akafa hali akiwa kafiri, basi hao amali zao zitakuwa zimebatilika duniani na akhera, na hao ndio watu wa Motoni; watakaa humo milele



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 218

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أُوْلَـٰٓئِكَ يَرۡجُونَ رَحۡمَتَ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika, walioamini na waliohama na wakapigana katika njia ya Allah hao wanataraji rehema za Allah, na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 219

۞يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِۖ قُلۡ فِيهِمَآ إِثۡمٞ كَبِيرٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَإِثۡمُهُمَآ أَكۡبَرُ مِن نَّفۡعِهِمَاۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلِ ٱلۡعَفۡوَۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo kuna dhambi kubwa mno na manufaa kwa watu. Na dhambi za viwili hivyo ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza: Watoe nini? Sema: (Toeni) Kilichozidi mahitaji. Kama hivi Allah anakubainishieni Aya zake ili mpate kutafakari



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 220

فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡيَتَٰمَىٰۖ قُلۡ إِصۡلَاحٞ لَّهُمۡ خَيۡرٞۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ ٱلۡمُفۡسِدَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعۡنَتَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

(Ili mtafakari) duniani na akhera. Na wanakuuliza kuhusu Mayatima. Sema: Kuwatengenezea vizuri mambo yao ni jambo la heri, na mkijichanganya nao basi hao ni ndugu zenu. Na Allah anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Allah lau angetaka (kukupatisheni tabu) angekupatisheni tabu. Kwa hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 221

وَلَا تَنكِحُواْ ٱلۡمُشۡرِكَٰتِ حَتَّىٰ يُؤۡمِنَّۚ وَلَأَمَةٞ مُّؤۡمِنَةٌ خَيۡرٞ مِّن مُّشۡرِكَةٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَتۡكُمۡۗ وَلَا تُنكِحُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤۡمِنُواْۚ وَلَعَبۡدٞ مُّؤۡمِنٌ خَيۡرٞ مِّن مُّشۡرِكٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكُمۡۗ أُوْلَـٰٓئِكَ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلنَّارِۖ وَٱللَّهُ يَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلۡجَنَّةِ وَٱلۡمَغۡفِرَةِ بِإِذۡنِهِۦۖ وَيُبَيِّنُ ءَايَٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ

Na msiwaoe wanawake washi-rikina mpaka waamini. Na kwa hakika kabisa, kijakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina, hata kama atakupendezeni. Na msiwaozeshe wanaume washirikina (makafiri) mpaka waamini. Na kwa hakika kabisa, mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina hata kama atakupendezeni. Hao (Washirikina) wanahubiri kwenda motoni, na Allah anahubiri kwenda peponi na kwenye msamaha kwa idhini yake, na anazibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 222

وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡمَحِيضِۖ قُلۡ هُوَ أَذٗى فَٱعۡتَزِلُواْ ٱلنِّسَآءَ فِي ٱلۡمَحِيضِ وَلَا تَقۡرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطۡهُرۡنَۖ فَإِذَا تَطَهَّرۡنَ فَأۡتُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَكُمُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلتَّوَّـٰبِينَ وَيُحِبُّ ٱلۡمُتَطَهِّرِينَ

Na wanakuuliza kuhusu Hedhi. Sema: Huo ni uchafu. Basi waepukeni wanawake (wake zenu) katika kipindi cha Hedhi, na msiwasogelee (msifanye nao jimai) mpaka watoharike. Na watakapojitoharisha, basi waendeeni kwa kupitia alipokuamrisheni Allah. Hakika, Allah anawapenda wenye kujitoharisha na anawapenda wenye kutubu sana



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 223

نِسَآؤُكُمۡ حَرۡثٞ لَّكُمۡ فَأۡتُواْ حَرۡثَكُمۡ أَنَّىٰ شِئۡتُمۡۖ وَقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُم مُّلَٰقُوهُۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Wake zenu ni mashamba yenu. Basi yaendeeni mashamba yenu namna mtakavyo. Na jifanyieni utangulizi. Na muogopeni Allah na jueni kuwa mtakutana naye. Na wape bishara wenye kuamini



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 224

وَلَا تَجۡعَلُواْ ٱللَّهَ عُرۡضَةٗ لِّأَيۡمَٰنِكُمۡ أَن تَبَرُّواْ وَتَتَّقُواْ وَتُصۡلِحُواْ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Msimfanye Allah kinga ya viapo vyenu mkaacha kufanya wema na kumcha (Allah) na kufanya suluhu kati ya watu. Na Allah ni Mwingi wa kusikia, Mjuzi mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 225

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتۡ قُلُوبُكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Allah hatakuchukulieni hatua kwa viapo vyenu vya kipuuzi. Lakini atakuchukulieni hatua kwa yale yaliyo nuiwa na nyoyo zenu. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 226

لِّلَّذِينَ يُؤۡلُونَ مِن نِّسَآئِهِمۡ تَرَبُّصُ أَرۡبَعَةِ أَشۡهُرٖۖ فَإِن فَآءُو فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kwa wanaoapa kujitenga na wake zao, basi wangoje miezi minne. Na endapo watarejea (kwa kutengua viapo vyao) basi kwa hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 227

وَإِنۡ عَزَمُواْ ٱلطَّلَٰقَ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na kama wakiazimia kutoa Talaka, basi Allah ni Mwingi wa kusikia, Mjuzi mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 228

وَٱلۡمُطَلَّقَٰتُ يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَٰثَةَ قُرُوٓءٖۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكۡتُمۡنَ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِيٓ أَرۡحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤۡمِنَّ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنۡ أَرَادُوٓاْ إِصۡلَٰحٗاۚ وَلَهُنَّ مِثۡلُ ٱلَّذِي عَلَيۡهِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيۡهِنَّ دَرَجَةٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Na wanawake walioachwa wangoje Kurui tatu. Na haifai kwao kuficha alichoumba Allah kwenye mifuko yao ya uzazi ikiwa kweli wanamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Na Waume wao wana haki zaidi ya kuwarejea katika muda huo kama wanakusudia suluhu. Na wanawake wanazo haki kwa waume wao kama walivyo na wajibu juu yao kwa wema. Na wanaume wana daraja zaidi kwa wake zao. Na Allah ni Mwenye nguvu nyingi, Mwenye hekima sana



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 229

ٱلطَّلَٰقُ مَرَّتَانِۖ فَإِمۡسَاكُۢ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ تَسۡرِيحُۢ بِإِحۡسَٰنٖۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَأۡخُذُواْ مِمَّآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ شَيۡـًٔا إِلَّآ أَن يَخَافَآ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۖ فَإِنۡ خِفۡتُمۡ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَا فِيمَا ٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَعۡتَدُوهَاۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Talaka ni mara mbili[1]. Basi (baada ya kumrejea) akae naye kwa wema au kumuacha kwa uzuri (aendelee kumaliza Eda yake). Na si halali kwenu kuchukua chochote katika vile mlivyowapa (wake zenu) isipokuwa kama wote wawili wataogopa kukiuka sharia za Allah. Basi kama mtaogopa kuwa hawatatekeleza sharia za Allah, hakuna ubaya kwa wawili (mke kurejesha mahari na mume kupokea) katika kile mwanamke alichojikombolea. Hiyo ni mipaka ya Allah, basi msiikiuke. Na watakaoikiuka mipaka ya Allah basi hao ni madhalimu hasa


1- - Ambazo mume ana haki ya kumrejea mkewe


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 230

فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُۥ مِنۢ بَعۡدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوۡجًا غَيۡرَهُۥۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۗ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na kama (mume) akimpa (mkewe) Talaka (ya tatu) basi si halali kwake (kumrejea au kumuoa upya) baada ya hapo mpaka afunge ndoa na mume mwingine. Na kama akimuacha (huyo mume wa pili) basi si vibaya kurejeana (kwa kufunga ndoa upya) kama wataona wanaweza kusimamisha mipaka ya Allah. Na hiyo ni mipaka ya Allah anayoibainisha kwa watu wanaojua



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 231

وَإِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖۚ وَلَا تُمۡسِكُوهُنَّ ضِرَارٗا لِّتَعۡتَدُواْۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ هُزُوٗاۚ وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمَآ أَنزَلَ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡحِكۡمَةِ يَعِظُكُم بِهِۦۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Na mtakapowaacha wake na wakakaribia kumaliza muda wa Eda zao, basi ishini nao kwa wema (kwa kuwarejea) au muwaachie (wamalize Eda zao na wawe huru) kwa wema. Na msibaki nao kwa lengo la kuwadhuru ili kuwafanyia uonevu. Na yeyote atakaye fanya hivyo basi kwa hakika atakuwa amejidhulumu mwenyewe. Na msizifanyie mzaha Aya za Allah. Na kumbukeni neema za Allah kwenu, na kitabu na hekima alizokuteremshieni. Allah anakuonyeni kwa hayo, na mcheni Allah na jueni kwamba, Allah ni Mjuzi mno wa kila kitu