فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ
Basi ilipokuja amri yetu tulimuokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu na kutokana na fedheha ya siku hiyo. Hakika Mola wako mlezi ndiye mwenye nguvu zaidi mwenye ushindi
وَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Na ukelele ukawaangamiza wale waliodhulumu, na wakapambazukiwa wakiwa maiti ndani ya majumba yao
كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ
Kana kwamba hawakuwepo humo. Elewa! Hakika Thamud walimkufuru Mola wao mlezi. Eleweni! Maangamizi yawafike watu wa Thamudi
وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ
Na hakika walikuja wajumbe wetu kwa Ibrahimu kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: salama! Haukupita muda akaleta ndama wa kuchoma
فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ
Na pindi alipoona mikono yao haimfikii (ndama-hawali) aliwatilia shaka, na woga ukamuingia. (Malaika) Wakamwambia: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa watu wa Lutwi’
وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ
Na mkewe alikuwa kasimama, na akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa mtoto) Is-haq, na baada ya Is-haq Yakubu
قَالَتۡ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ ءَأَلِدُ وَأَنَا۠ عَجُوزٞ وَهَٰذَا بَعۡلِي شَيۡخًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عَجِيبٞ
(Mke wa Ibrahimu) akasema: Ee, hivi nitazaa kweli ilhali mimi ni kikongwe! Na mume wangu huyu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu sana!
قَالُوٓاْ أَتَعۡجَبِينَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۖ رَحۡمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٞ مَّجِيدٞ
(Malaika) wakasema: hivi, unastaajabu amri ya Allah? Rehema ya Allah na baraka zake ziko kwenu, watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ni Mwenye kusifiwaMwenye kutukuzwa
فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ
Na pindi hofu ilipomuondoka Ibrahimu, na ikamjia ile bishara (ya kupata mtoto), alianza kujadiliana nasi kuhusu watu wa Lutwi’
إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّـٰهٞ مُّنِيبٞ
Hakika Ibrahimu alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Allah
يَـٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ
(Malaika walimwambia): Ewe Ibrahimu! Hili liache! Kwa hakika kabisa amri ya Mola wako mlezi imeshafika, na hakika hao itawafika adhabu isiyo rudi nyuma
وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ
Na pindi wajumbe wetu walipo kuja kwa Lutwi’ alijihisi huzuni na akawaonea dhiki. Na akasema: Hii leo ni siku ngumu sana!
وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ
Watu wake wakamjia mbio mbio. Na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Lutwi) akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa hapa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Allah, na msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Hivi, miongoni mwenu hakuna hata mmoja aliye na akili?
قَالُواْ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنۡ حَقّٖ وَإِنَّكَ لَتَعۡلَمُ مَا نُرِيدُ
Wakasema: Bila shaka unajua hatuna haki juu ya binti zako, na hakika unajua tunayoyataka
قَالَ لَوۡ أَنَّ لِي بِكُمۡ قُوَّةً أَوۡ ءَاوِيٓ إِلَىٰ رُكۡنٖ شَدِيدٖ
(Lutwi) akasema: Laiti mimi ningekuwa na nguvu ya kuwazuia, au ningekuwa na kabila na jamaa wenye nguvu tungepambana nanyi!
قَالُواْ يَٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓاْ إِلَيۡكَۖ فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٌ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمۡۚ إِنَّ مَوۡعِدَهُمُ ٱلصُّبۡحُۚ أَلَيۡسَ ٱلصُّبۡحُ بِقَرِيبٖ
(Malaika) wakasema: Ewe Lutwi›! Sisi ni wajumbe wa Mola wako mlezi, hawatakufikia. Na ondoka pamoja na watu wako katika kipande cha usiku uliobaki. Na yeyote miongoni mwenu asigeuke kutazama nyuma, isipokuwa mkeo itamfika adhabu (itakayowafika wengine). Hakika miadi yao ni asubuhi. Hivi, asubuhi si karibu?
فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ
Basi ilipofika amri yetu tulikigeza (kijiji kile) juu chini, na tukawateremshia mvua ya mawe kutoka Motoni
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ
(Mawe) yaliyotiwa alama maalumu kwa Mola wako mlezi. Na (mawe) hayo hayawakosi madhalimu
۞وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ وَلَا تَنقُصُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَۖ إِنِّيٓ أَرَىٰكُم بِخَيۡرٖ وَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ مُّحِيطٖ
Na kwa watu wa Madyana (tulimpeleka) ndugu yao Shuaib. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Allah pekee, hamna nyinyi Allah mwingine asiye kuwa Yeye. Na msipunguze vipimo vya ujazo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mpo katika hali nzuri (kimaisha). Na mimi nahofia kwenu adhabu katika Siku itakayowazunguka (kwa sababu ya kuwapunja watu)
وَيَٰقَوۡمِ أَوۡفُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo vya ujazo na mizani kwa uadilifu na msiwapunje watu vitu vyao; Na msiende huku na kule ardhini mkafanya uharibifu
بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ
(Kile) anachowabakishieni Allah (katika faida baada ya kutekeleza vipimo) ni bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. Na mimi sio mlinzi wenu
قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأۡمُرُكَ أَن نَّتۡرُكَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوۡ أَن نَّفۡعَلَ فِيٓ أَمۡوَٰلِنَا مَا نَشَـٰٓؤُاْۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلۡحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ
Wakasema: Ewe Shuaibu! Hivi (hizi) swala zako ndizo zinakuamuru tuache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu au tuache kufanya tupendayo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mpole sana na muongofu
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje kama nitakuwa na dalili kutoka kwa Mola wangu mlezi, na ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Na sipendi niwe kinyume na nyinyi nikafanya yale ninayowakatazeni. Sitaki ispokuwa kutengeneza kiasi niwezavyo. Na hakuna taufiki ispokuwa kwa Allah tu. Kwake tu nimetegemea na kwake tu nimerejea
وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ
Na enyi watu wangu! Kuacha kwangu dini yenu kusipelekee muwe wakaidi ikawa sababu ya nyinyi kupatwa na (adhabu) mfano wa iliyowapata watu wa Nuhu au watu wa Huud au watu wa Swaleh Na watu wa Lutwi kwenu hawako mbali
وَٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٞ وَدُودٞ
Na ombeni msamaha kwa Mola wenu mlezi, kisha rejeeni kwake. Hakika Mola wangu mlezi ni Mwenye kurehemu mwenye upendo
قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفٗاۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٖ
Wakasema: Ewe Shuaibu! Hatufahamu saana hayo uyasemayo. Na wewe kwetu tunakuona mtu dhaifu tu. Lau kama sio kuwepo jamaa zako, tunge (kuuwa kwa) kukupiga mawe, na wewe kwetu si mtu mwenye heshima yoyote
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ
Akasema: Enyi watu wangu! Hivi kundi langu ndio lina nguvu zaidi kwenu kuliko Allah? Na mmemuweka (Allah) nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu mlezi ni mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda
وَيَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَمَنۡ هُوَ كَٰذِبٞۖ وَٱرۡتَقِبُوٓاْ إِنِّي مَعَكُمۡ رَقِيبٞ
Na enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakaye mfika adhabu ya kumfedhehesha, na nani aliye mwongo. Na ngojeni, mimi pia ninangoja pamoja nanyi
وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Na ilipo fika amri yetu, tulimuokoa Shuaibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na uliwachukuwa wale waliyodhulumu ukelele, basi wakapambazukiwa wakiwa wamekufa kifudifudi! Majumbani mwao
كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ
Kana kwamba hawakuishi humo. Elewa mangamizi yawe kwa watu wa Madyana, kama walivyo angamia watu wa Thamud!