قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٌۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَنِي بِهِمۡ جَمِيعًاۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
(Yakub) Alisema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo. Basi subira ni jambo jema! Asaa Allah akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye (Allah) ndiye Mjuzi sana, Mwenye hekima
وَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَـٰٓأَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَٱبۡيَضَّتۡ عَيۡنَاهُ مِنَ ٱلۡحُزۡنِ فَهُوَ كَظِيمٞ
Na (Yakubu) akajitenga nao na kusema: Ah! Maskini Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni. Kwasababu hiyo yeye ni mwenye kuugulia maumivu
قَالُواْ تَٱللَّهِ تَفۡتَؤُاْ تَذۡكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوۡ تَكُونَ مِنَ ٱلۡهَٰلِكِينَ
Walisema: Wallahi, (hivi) huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walioangamia?
قَالَ إِنَّمَآ أَشۡكُواْ بَثِّي وَحُزۡنِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
(Yakub) Alisema: Hakika mimi ninamshitakia Allah sikitiko langu na huzuni yangu na ninajua kwa Allah msiyoyajua
يَٰبَنِيَّ ٱذۡهَبُواْ فَتَحَسَّسُواْ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَاْيۡـَٔسُواْ مِن رَّوۡحِ ٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ لَا يَاْيۡـَٔسُ مِن رَّوۡحِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Enyi wanangu, nendeni (Misri) mkamtafute Yusuf na ndugu yake, wala msiikatie tamaa faraja ya Allah. Hakika, hawaikatii tamaa faraja ya Allah isipokuwa watu makafiri tu.[1]
1- - Aya hapa inamhimiza Muislamu kufanya juhudi katika jambo lenye manufaa na hatakiwi kukata tamaa.
فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَيۡهِ قَالُواْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهۡلَنَا ٱلضُّرُّ وَجِئۡنَا بِبِضَٰعَةٖ مُّزۡجَىٰةٖ فَأَوۡفِ لَنَا ٱلۡكَيۡلَ وَتَصَدَّقۡ عَلَيۡنَآۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَجۡزِي ٱلۡمُتَصَدِّقِينَ
Basi (watoto wa Yakub) wa-lipoingia kwake (kwa Yusuf) walisema: Ewe Mheshimiwa, yametupata sisi na familia zetu madhara (ukame) na tumeleta bidhaa duni. Basi tupimie kipimo na tupe sadaka. Hakika, Allah huwalipa watoao sadaka
قَالَ هَلۡ عَلِمۡتُم مَّا فَعَلۡتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذۡ أَنتُمۡ جَٰهِلُونَ
(Yusuf) Alisema: Je, mnaya-kumbuka mliyomfanyia Yusuf na nduguye wakati nyinyi ni wajinga?
قَالُوٓاْ أَءِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُۖ قَالَ أَنَا۠ يُوسُفُ وَهَٰذَآ أَخِيۖ قَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَآۖ إِنَّهُۥ مَن يَتَّقِ وَيَصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Walisema: Kwani wewe kwa hakika kabisa ndiye Yusuf? Alisema (naam): Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Allah ametuneemesha. Ilivyo ni kwamba, yeyote amchae Allah na akawa na subira, basi Allah hapotezi ujira wa wafanyao mazuri
قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ ءَاثَرَكَ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَإِن كُنَّا لَخَٰطِـِٔينَ
Walisema: Tunaapa kwa Allah (kwamba), hakika Allah amekufadhilisha wewe (amekufanya wewe bora) kuliko sisi, na hakika kabisa sisi tulikuwa wakosefu
قَالَ لَا تَثۡرِيبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَۖ يَغۡفِرُ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّـٰحِمِينَ
(Yusuf) Alisema: Leo hakuna lawama juu yenu. Allah atakusameheni, naye ni Mwenye huruma kuliko wenye huruma wote
ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Nendeni na kanzu yangu hii na mkaitupie usoni kwa Baba yangu, (akiipata harufu yangu tu atapona na) ataona na nileteeni familia yenu yote
وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ
Na msafara ulipoondoka tu (Misri), Baba yao alisema (kuwaambia aliokuwa nao): Hakika, mimi kwa yakini kabisa nanusa harufu ya Yusuf, lau kama hamtaniona mpuuzi
قَالُواْ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَٰلِكَ ٱلۡقَدِيمِ
Walisema: Tunaapa kwa Allah, hakika wewe bado kabisa ungali katika upotevu wako wa kale (wa kumpenda Yusuf)
فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلۡبَشِيرُ أَلۡقَىٰهُ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ فَٱرۡتَدَّ بَصِيرٗاۖ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Basi alipofika mbashiri na akaitupa kanzu usoni kwake na kwasababu hiyo, akarejea kuona, alisema: Je, sikukuambieni kuwa mimi ninajua kwa Allah msiyoyajua?
قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا ٱسۡتَغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَآ إِنَّا كُنَّا خَٰطِـِٔينَ
Walisema: Ewe Baba yetu, tuombee (kwa Allah) msamaha kwa dhambi zetu. Kwa hakika sisi tulikuwa wakosaji
قَالَ سَوۡفَ أَسۡتَغۡفِرُ لَكُمۡ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Alisema: Nitakuombeeni msa-maha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika, Yeye (Allah) ndiye tu Msamehevu, Mwenye kurehemu
فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَبَوَيۡهِ وَقَالَ ٱدۡخُلُواْ مِصۡرَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ
Basi walipoingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na alisema: Ingieni Misri, Inshaa-Allah, mkiwa katika amani
وَرَفَعَ أَبَوَيۡهِ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ وَخَرُّواْ لَهُۥ سُجَّدٗاۖ وَقَالَ يَـٰٓأَبَتِ هَٰذَا تَأۡوِيلُ رُءۡيَٰيَ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَعَلَهَا رَبِّي حَقّٗاۖ وَقَدۡ أَحۡسَنَ بِيٓ إِذۡ أَخۡرَجَنِي مِنَ ٱلسِّجۡنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلۡبَدۡوِ مِنۢ بَعۡدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيۡطَٰنُ بَيۡنِي وَبَيۡنَ إِخۡوَتِيٓۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٞ لِّمَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi, na wote wakaporomoka kumsujudia.[1] Na (Yusuf) alisema: Ewe Baba yangu, hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu pale zamani. Na Allah ameijaalia (ndoto hiyo) kuwa ya kweli. Na (Allah) amenifanyia mazuri mno kwasababu alinitoa gerezani na amekuleteni kutoka jangwani baada ya shetani kuchochea uhasama baina yangu na baina ya ndugu zangu. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Muungwana kwa ayatakayo. Kwa hakika, Yeye (Allah) ndiye Mjuzi, Mwenye hekima
1- - Huu ulikuwa utaratibu wa wakati huo wa kusalimia viongozi kwa kusujudu.
۞رَبِّ قَدۡ ءَاتَيۡتَنِي مِنَ ٱلۡمُلۡكِ وَعَلَّمۡتَنِي مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَنتَ وَلِيِّۦ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ تَوَفَّنِي مُسۡلِمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّـٰلِحِينَ
(Kisha Yusuf akaomba akasema): Ewe Mola wangu Mlezi, kwa hakika umenipa sehemu ya ufalme na umenifundisha sehemu ya tafsiri ya matukio (ndoto). (Ewe) Muumba wa mbingu na ardhi, Wewe ndiye Mlinzi wangu duniani na Akhera. Nifishe nikiwa Muislamu na nikutanishe na wenye kutenda mema
ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۖ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ أَجۡمَعُوٓاْ أَمۡرَهُمۡ وَهُمۡ يَمۡكُرُونَ
Hizo (habari zilizotajwa kuhusu Yusuf) ni sehemu ya habari za Ghaibu tulizokufunulia (ewe Muhammad) na hukuwa pamoja nao wakati (ndugu wa Yusuf) walipo azimia kwa pamoja shauri lao (la kumdhuru Yusuf) na ilhali wao wanafanya hila
وَمَآ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ وَلَوۡ حَرَصۡتَ بِمُؤۡمِنِينَ
Na watu wengi sana si wenye kuamini nahataukijitahidi
وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Na (wewe) huwaombi ujira wowote juu ya hilo (la kuifikisha hii Qur’ani). Haikuwa hiyo (Qur’ani) isipokuwa tu ni ukumbusho kwa walimwengu wote
وَكَأَيِّن مِّنۡ ءَايَةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يَمُرُّونَ عَلَيۡهَا وَهُمۡ عَنۡهَا مُعۡرِضُونَ
Na (kuna) ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, na hali ya kuwa wanazipuuza?
وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ
Na wengi wao hawamuamini Allah isipokuwa tu wakiwa washirikina
أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Je, hivi wamejiaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Allah ya kuwagubika au hakitawafikia Kiyama kwa ghafla na hali hawatambui?
قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Hii ndiyo njia yangu; ninalingania (ninahubiri) kwa Allah kwa kujua, mimi na wanaonifuata. Na Allah ametakasika na mimi siomiongoni mwa washirikina
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hivi hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Na hakika, nyumba ya Akhera ni bora kwa wanaomcha Allah. Basi hamtumii akili?
حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
(Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) Mpaka Mitume (hao) walipokata tamaa (ya watu wao kutoamini) na wakadhani kuwa wamekadhibishwa (wamepingwa), hapo ikawajia nusura yetu natukawaokoa tuwatakao. Na adhabu yetu kali hairudishwi (haizuiliki) kwa watu waovu
لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Kwa hakika kabisa, katika simulizi zao (hao Mitume) kuna mazingatio kwa wenye akili. Haikuwa (hii Qur’an ni) maneno yanayozushwa lakini ni usadikisho (uthibitisho) wa (maandiko matakatifu) yaliyokuwepo kabla yake (Taurati na Injili) na ni ufafanuzi wa kila kitu na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini
الٓمٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِۗ وَٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ
Alif Laam Miim Raa[1]. Hizo ni Aya za Kitabu. Na (hii Qur’an ni wahyi) ambayo umeteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni haki lakini watu wengi hawaamini
1- - Allah pekee ndiye anayejua maana ya herufi hizi mkato.