لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ
Nyinyi mna dini yenu, nami nina dini yangu
إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ
Itakapokuja nusra ya Allah na ushindi (ukombozi wa mji wa Makka)
وَرَأَيۡتَ ٱلنَّاسَ يَدۡخُلُونَ فِي دِينِ ٱللَّهِ أَفۡوَاجٗا
Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Allah kwa makundi
فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُۚ إِنَّهُۥ كَانَ تَوَّابَۢا
Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na muombe msamaha. Hakika, Yeye (Allah) amekuwa Mwenye kukubali sana toba. Sura imetoa utabiri wa kifo cha Mtume rehma na amani ziwe juu yake
تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abulahab na yeye (kwa maana hiyo) ameangamia
مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Haitamfaa mali yake na (vitendo) alivyovichuma (alivyovifanya)
سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ
Atauingia moto wenye muwako
وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ
(Ataingia Motoni yeye) Na mkewe, mchukuzi mkubwa wa kuni
فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ
Shingoni mwake iko kamba ya kusokotwa
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ
Sema: Yeye Allah ni wa pekee
ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ
Allah ndiye tu Mkusudiwa (katika kuabudiwa, kutegemewa na kutatua shida za watu)
لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ
Hakuzaa[1] na hakuzaliwa.[2]
1- - Kwa maana hiyo hana mtoto.
2- - Kwa maana hiyo hana baba wala mama.
---------------
------------------------------------------------------------
---------------
------------------------------------------------------------
وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ كُفُوًا أَحَدُۢ
Na hakuna yeyote anaye fanana naye
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ
Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko
مِن شَرِّ مَا خَلَقَ
(Najikinga) Dhidi ya shari ya alivyoviumba
وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ
Na (najikinga) dhidi ya shari ya giza la usiku liingiapo
وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ
Na (najikinga) dhidi ya shari ya (wanawake) wanaopulizia mafundoni
وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ
Na (najikinga) dhidi ya shari ya hasidi anapo husudu
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu
مَلِكِ ٱلنَّاسِ
Mfalme wa watu
إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ
Muabudiwa wa haki wa watu (Mwenye haki ya kuabudiwa na watu)
مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ
(Najilinda dhidi ya shari ya (shetani) mwenye kutia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma
ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ
Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu
مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ
(Shetani) Anayetokana na majini na watu