يَوۡمَ نَحۡشُرُ ٱلۡمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ وَفۡدٗا
Siku tutakayo wakusanya wacha Mungu kuwapeleka kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni wageni wake
وَنَسُوقُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرۡدٗا
Na tukawachunga waovu kuwapeleka Jahannamu hali ya kuwa wana kiu
لَّا يَمۡلِكُونَ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَنِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا
Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale walio chukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema
وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَلَدٗا
Na wao ati husema kuwa (Allah) Mwingi wa Rehema amejifanyia mtoto!
لَّقَدۡ جِئۡتُمۡ شَيۡـًٔا إِدّٗا
Hakika mmeleta jambo kubwa mno!
تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِنۡهُ وَتَنشَقُّ ٱلۡأَرۡضُ وَتَخِرُّ ٱلۡجِبَالُ هَدًّا
Mbingu zinakaribia kupasuka pasuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande
أَن دَعَوۡاْ لِلرَّحۡمَٰنِ وَلَدٗا
Kwa kudai kwao kuwa (Allah) Mwingi wa Rehema ana mtoto
وَمَا يَنۢبَغِي لِلرَّحۡمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
Na haitakiwi kwa (Allah) Mwingi wa Rehema kuwa na mtoto.[1]
1- - Aya hizi tano 88, 89, 90, 91 na 92 zinakataa kwa ukali itikadi kwamba Mungu ana mtoto. Muislamu hatakiwi kabisa kuikumbatia itikadi hii au kuishabikia. Ni itikadi mbaya mno kiasi kwamba mbingu, ardhi na milima haziivumilii kuisikia.
إِن كُلُّ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ إِلَّآ ءَاتِي ٱلرَّحۡمَٰنِ عَبۡدٗا
Hapana yeyote aliyomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake
لَّقَدۡ أَحۡصَىٰهُمۡ وَعَدَّهُمۡ عَدّٗا
Yeye hakika amewadhibiti na amewahesabu sawa sawa
وَكُلُّهُمۡ ءَاتِيهِ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَرۡدًا
Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ سَيَجۡعَلُ لَهُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وُدّٗا
Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi
فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ ٱلۡمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِۦ قَوۡمٗا لُّدّٗا
Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur’ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wacha Mungu, na uwaonye kwayo watu wabishi
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هَلۡ تُحِسُّ مِنۡهُم مِّنۡ أَحَدٍ أَوۡ تَسۡمَعُ لَهُمۡ رِكۡزَۢا
Na kaumu ngapi tuziangamiza kabla yao. Je! Unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mchakato wao