إِنَّمَا مَثَلُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَآءٍ أَنزَلۡنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخۡتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلۡأَرۡضِ مِمَّا يَأۡكُلُ ٱلنَّاسُ وَٱلۡأَنۡعَٰمُ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذَتِ ٱلۡأَرۡضُ زُخۡرُفَهَا وَٱزَّيَّنَتۡ وَظَنَّ أَهۡلُهَآ أَنَّهُمۡ قَٰدِرُونَ عَلَيۡهَآ أَتَىٰهَآ أَمۡرُنَا لَيۡلًا أَوۡ نَهَارٗا فَجَعَلۡنَٰهَا حَصِيدٗا كَأَن لَّمۡ تَغۡنَ بِٱلۡأَمۡسِۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ
Hakika ilivyo ni kwamba, mfano wa maisha ya duniani ni kama maji (mvua) tuliyo yateremsha kutoka mawinguni yakachanganyika na mimea ya ardhini, ikiwa ni pamoja na mimea inayoliwa na watu na mifugo mpaka ardhi ilipokamilisha urembo wake na ikapendeza (kwa kustawi vizuri) na watu wake (wamiliki wake) wakadhani kwamba wameyaweza (mazao hayo kufanikiwa kuyafikisha hatua ya kuvuna), likawajia jambo letu usiku au mchana basi tukaifanya imevunwa (na kufyekwa) kana kwamba haikuwepo jana. Hivi ndivyo tunavyo zifafanua Aya (zetu) kwa watu wanaofikiri
وَٱللَّهُ يَدۡعُوٓاْ إِلَىٰ دَارِ ٱلسَّلَٰمِ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na Allah anaita (watu) kwenye nyumba ya amani na anamuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka