وَقَالُواْ كُونُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰ تَهۡتَدُواْۗ قُلۡ بَلۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِـۧمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Na wamesema: Kuweni Wayahudi au Wanaswara mtaon-goka. Sema: Bali (tunafuata) dini ya Ibrahimu aliyeacha dini zote potevu na kufuata Uislamu, na hakuwa miongoni mwa washirikina
قُولُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِيَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ
Semeni: Tumemuamini Allah na tulichoteremshiwa na alichoteremshiwa Ibrahimu na Ismaili na Isihaka na Yakubu na watoto wa Yakubu na alichopewa Musa na Isa, na walichopewa Manabii kutoka kwa Mola wao. Hatumbagui yeyote kati yao, na sisi ni wenye kujisalimsha kwake
فَإِنۡ ءَامَنُواْ بِمِثۡلِ مَآ ءَامَنتُم بِهِۦ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا هُمۡ فِي شِقَاقٖۖ فَسَيَكۡفِيكَهُمُ ٱللَّهُۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Endapo wataamini kama mlivyoamini, basi watakuwa wameongoka. Na endapo watakataa, basi elewa kuwa si vingine bali hao wako katika upinzani tu. Na Allah atakusalimisha nao. Na yeye ni Msikivu, Mwenye kujua sana
صِبۡغَةَ ٱللَّهِ وَمَنۡ أَحۡسَنُ مِنَ ٱللَّهِ صِبۡغَةٗۖ وَنَحۡنُ لَهُۥ عَٰبِدُونَ
(Dini ya Uislamu) Ni pambo la Allah (analotaka Waislamu wajipambe nalo). Na ni nani mzuri zaidi wa kupamba kuliko Allah? Na sisi tunamuabudu yeye tu
قُلۡ أَتُحَآجُّونَنَا فِي ٱللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمۡ وَلَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُخۡلِصُونَ
Sema: Hivi mnajadiliana na sisi kuhusu Allah ilhali yeye ndiye Mola wetu na ndiye Mola wenu na sisi tuna matendo yetu na nyinyi mnamatendo yenu na sisi tunamkusudia na kumuelekea yeye tu kwa matendo yetu?
أَمۡ تَقُولُونَ إِنَّ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطَ كَانُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ قُلۡ ءَأَنتُمۡ أَعۡلَمُ أَمِ ٱللَّهُۗ وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَٰدَةً عِندَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Au mnasema kuwa, Ibrahimu na Ismaili na Isihaka na Yakubu na watoto wake walikuwa Wayahudi au Wanaswara? Sema: Hivi nyinyi ndio wajuzi zaidi au Allah? Na ni nani aliyedhalimu mno kuliko yule aliyeuficha ushahidi alionao kutoka kwa Allah? Na Allah si mwenye kughafilika na yote mnayoyafanya
تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Huo ni umma umeshapita. Utapata ulichokichuma na nyinyi mtapata mlichokichuma. Na hamtaulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyafanya