يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ
Ewe uliye jifunika
قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا
Simama usiku kucha (kuswali) isipokuwa kidogo tu
نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا
Nusu yake au ipunguze kidogo
أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا
Au izidishe, na soma Qurani vizuri (kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zake)
إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا
Hakika Sisi hivi punde tutakute-remshia neno zito (Qur’ani).[1]
1- - Qur’ani imetajwa hapa kwamba ni kauli nzito kwa sababu imekusanya amri, makatazo, mafunzo, sheria majukumu mazito ambayo Muislamu anatakiwa awe imara ili aweze kuyatekeleza.
إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا
Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.[1]
1- - Hakika ibada zinazo fanywa usiku zinaganda zaidi katika moyo wa mtu, na zinabainika zaidi ulimini, na zinasibu vyema zaidi, kuliko visomo vya ibada za mchana.
إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا
Kwani hakika mchana una shughuli nyingi
وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا
Na litaje Jina la Mola wako, na jitolee Kwake kikamilifu
رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا
Mola wa Mashariki na Magharibi, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi mfanye kuwa ni Mdhamini wako (na Mtegemewa wako)
وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا
Na subiri juu ya yale wayasemayo, na uwaepuke muepuko wa wema
وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا
Na Niache Mimi na wanaoka-dhibisha, walioneemeka na wape muhula kidogo
إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا
Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unaowaka kwa ukali kabisa!
وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا
Na chakula kinachokwama kooni (hakimezeki) na adhabu inayoumiza sana
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا
Siku ambayo ardhi itatikisika na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا
Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni
فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا
Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso
فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا
Basi vipi mtaweza kujikinga, kama mkikufuru Siku itakayowafanya watoto kuwa wenye kutoka mvi?
ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا
Hapo ndipo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa
إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Kwa hakika huu ni ukumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kuelekea kwa Mola wake
۞إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ
Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Allah ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamuwezi kuweka hesabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qurani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila za Allah, na wengine wanapigana katika Njia ya Allah. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Allah mkopo ulio mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Allah, nayo imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Allah. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu