طه
Twaahaa!
مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ
Hatukukuteremshia Qur’an ili upate mashaka
إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ
Bali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea
تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى
(Hii Qur’ani ni) uteremsho kutoka kwa Allah Ambaye Ameum-ba ardhi na mbingu zilizo juu
ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ
Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliyestawi juu ya Kiti cha Enzi
لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَمَا تَحۡتَ ٱلثَّرَىٰ
Ni vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na viliomo baina yao, na viliomo chini ya ardhi
وَإِن تَجۡهَرۡ بِٱلۡقَوۡلِ فَإِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخۡفَى
Na ukinyanyua sauti kwa kusema... basi hakika Yeye anajua siri na kilichofichikana zaidi kuliko siri
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ
Allah! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa
وَهَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Na je! Imekufikia habari ya Mussa?
إِذۡ رَءَا نَارٗا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدٗى
Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka (katika) huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto
فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ يَٰمُوسَىٰٓ
Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Mussa!
إِنِّيٓ أَنَا۠ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوٗى
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la Tuwa
وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ
Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa
إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ
Hakika Mimi ndiye Allah. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi
إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ
Hakika Saa (Kiyama) kitakuja bila ya shaka. Nimekaribia kukificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyo yafanya
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡهَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرۡدَىٰ
Kwa hivyo asikukengeushe nacho (Kiyama) yule ambaye hakiamini na akafuata matamanio yake ukaja kuangamia
وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ
Na nini hicho kilichomo katika mkono wako wa kulia, ewe Mussa?
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ
Akasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine
قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ
(Allah) Akasema: Basi iangushe ewe Mussa
فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ
Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio
قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ
Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza
وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ
Na ukumbatie mkono wako kwenye ubavu wako. Utatoka mweupe pasipo kuwa na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyengine
لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى
Ili tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka
قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي
(Mussa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي
Na uifanye kazi yangu (kuwa) nyepesi,
وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي
Wapate kufahamu maneno yangu
وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي
Na nipe waziri katika watu wangu,
هَٰرُونَ أَخِي
Harun, ndugu yangu