السورة: AL-IMRAN 

الآية : 181

لَّقَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ فَقِيرٞ وَنَحۡنُ أَغۡنِيَآءُۘ سَنَكۡتُبُ مَا قَالُواْ وَقَتۡلَهُمُ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَنَقُولُ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika Allah amesikia kauli ya wale waliosema: Hakika Allah ni fukara na sisi ndio matajiri, tutakisajili walichokisema, na kuwaua kwao manabii bila ya haki, na siku ya Kiama tutawaambia: onjeni adhabu ya Moto wenye kuunguza



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 182

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيكُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيۡسَ بِظَلَّامٖ لِّلۡعَبِيدِ

Hayo ni kutokana na ambayo imetanguliza mikono yenu na hakika Allah si mwenye kuwadhulumu waja



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 183

ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ عَهِدَ إِلَيۡنَآ أَلَّا نُؤۡمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأۡتِيَنَا بِقُرۡبَانٖ تَأۡكُلُهُ ٱلنَّارُۗ قُلۡ قَدۡ جَآءَكُمۡ رُسُلٞ مِّن قَبۡلِي بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَبِٱلَّذِي قُلۡتُمۡ فَلِمَ قَتَلۡتُمُوهُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Ambao wamesema hakika Allah ametuusia yakuwa tusimuamini Mtume yeyote hadi atuletee sadaka ambayo Moto utakula sadaka hiyo, basi sema wamewajieni Mitume kabla yangu wakiwa na ubainifu na ambalo mmelisema kwa nini mliwaua hao kama ni wa kweli



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 184

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدۡ كُذِّبَ رُسُلٞ مِّن قَبۡلِكَ جَآءُو بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُنِيرِ

Na kama watakukadhibisha basi hakika wamekadhibishwa Mitume kabla yako wamekuja na ubainifu na vitabu na kitabu chenye nuru



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 185

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوۡنَ أُجُورَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ فَمَن زُحۡزِحَ عَنِ ٱلنَّارِ وَأُدۡخِلَ ٱلۡجَنَّةَ فَقَدۡ فَازَۗ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ

Kila nafsi itaonja kifo, si vingine malipo yenu mtapewa yakiwa kamili siku ya kiyama, atakaye epushwa na kuwekwa mbali na Moto na akaingizwa Peponi basi huyo amefanikiwa, na haikua maisha ya dunia ila ni starehe zenye kudanganya



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 186

۞لَتُبۡلَوُنَّ فِيٓ أَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ وَلَتَسۡمَعُنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُوٓاْ أَذٗى كَثِيرٗاۚ وَإِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنۡ عَزۡمِ ٱلۡأُمُورِ

Na apa ya kuwa mtapewa mitihani katika mali zenu na nafsi zenu, na mtazisikia kero nyingi kutoka kwa waliopewa vitabu kabla yenu na kutoka kwa wale waliofanya ushirikina, na ikiwa mtavumilia na mkamcha Allah, basi hayo ndiyo mambo ya kuazimia



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 187

وَإِذۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ لَتُبَيِّنُنَّهُۥ لِلنَّاسِ وَلَا تَكۡتُمُونَهُۥ فَنَبَذُوهُ وَرَآءَ ظُهُورِهِمۡ وَٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلٗاۖ فَبِئۡسَ مَا يَشۡتَرُونَ

Na kumbuka pale Allah alipochukua ahadi nzito, kwa ambao wamepewa kitabu kuwa lazima mtakibainisha kwa watu na hamtakificha, wakaitupa ahadi hiyo nyuma ya migongo yao, wakiuza ahadi kwa thamani ndogo, basi biashara mbaya ni hiyo waliyoifanya



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 188

لَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أَتَواْ وَّيُحِبُّونَ أَن يُحۡمَدُواْ بِمَا لَمۡ يَفۡعَلُواْ فَلَا تَحۡسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٖ مِّنَ ٱلۡعَذَابِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Usidhanie ambao wanafurahi kwa walichokifanya, na wanapenda wasifiwe kwa wasichokifanya msifikirie kuwa wamefaulu kuepuka adhabu wao wana adhabu iumizayo



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 189

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Na ufalme wa Mbingu na Ardhi ni wa Allah, na Allah ni muweza wa kila kitu



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 190

إِنَّ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Hakika katika kuumba Mbingu na Ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana ni dalili tosha kwa wenye akili



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 191

ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَٰذَا بَٰطِلٗا سُبۡحَٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

(Wenye akili) ambao wanamtaja Mola wao wakiwa wamesimama na wamekaa na wamelalia mbavu zao, na huku wakitafakari katika umbo la Mbingu na Ardhi wa kisema: Ewe Mola wetu haukuliumba umbo hili bila ya hekima, umetakasika na basi tuepushe na adhabu ya Moto



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 192

رَبَّنَآ إِنَّكَ مَن تُدۡخِلِ ٱلنَّارَ فَقَدۡ أَخۡزَيۡتَهُۥۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ

Ewe Mola wetu hakika unaemuingiza Motoni basi umemdhalilisha na madhalimu hawana mtetezi



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 193

رَّبَّنَآ إِنَّنَا سَمِعۡنَا مُنَادِيٗا يُنَادِي لِلۡإِيمَٰنِ أَنۡ ءَامِنُواْ بِرَبِّكُمۡ فَـَٔامَنَّاۚ رَبَّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرۡ عَنَّا سَيِّـَٔاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ ٱلۡأَبۡرَارِ

Ewe Mola wetu hakika sisi tumemsikia mtoa wito akitoa wito wa imani: Muaminini Mola wenu hapo hapo tukaamini, ewe Mola tusamehe makosa yetu na utufutie maovu yetu na utuweke pamoja na waja wako wema



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 194

رَبَّنَا وَءَاتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخۡزِنَا يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ إِنَّكَ لَا تُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ

Ewe Mola wetu na utupe ulichotuahidi kupitia Mitume wako na usitudhalilishe siku ya Kiyama hakika wewe huendi kinyume na ahadi



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 195

فَٱسۡتَجَابَ لَهُمۡ رَبُّهُمۡ أَنِّي لَآ أُضِيعُ عَمَلَ عَٰمِلٖ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰۖ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۖ فَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ وَأُخۡرِجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَأُوذُواْ فِي سَبِيلِي وَقَٰتَلُواْ وَقُتِلُواْ لَأُكَفِّرَنَّ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ ثَوَابٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلثَّوَابِ

Mola wao akawajibu: Mimi sipotezi tendo la mtendaji yeyote miongoni mwenu awe mwanaume au mwanamke nyinyi kwa nyinyi, basi wale waliohama na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa na kukerwa katika njia yangu, na wakapigana na wakauliwa naapa nitawafutia makosa yao na naapa nitawaingiza katika Pepo inayotiririka chini yake mito ikiwa malipo kutoka kwa Allah, na kwa Allah ndiko kuliko na malipo mazuri



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 196

لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ

Yasikuhadae mabadiliko ya maisha ya makafiri katika miji



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 197

مَتَٰعٞ قَلِيلٞ ثُمَّ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Hiyo starehe ya muda mchache lakini makazi yao ya kudumu ni Moto wa Jahannamu, na ni mafikio mabaya



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 198

لَٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ رَبَّهُمۡ لَهُمۡ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا نُزُلٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۗ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّلۡأَبۡرَارِ

Lakini wale wamchao Mola wao, wana Pepo zenye kutiririka chini yake mito na watabaki humo, ni makaribisho kutoka kwa Allah, na kilicho kwa Allah ni bora mno kwa wafanyao mema



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 199

وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Na kwa hakika katika Watu wa kitabu wapo wanaomuamini Allah hasa na kilichoteremshwa kwenu na kilichoteremshwa kwao, huku wakinyenyekea kwa Allah. Hawauzi Aya za Allah kwa thamani ndogo (ya dunia). Hao malipo yao yako kwa Mola wao mlezi, hakika Allah ni mwepesi mno wa kuhesabu



السورة: AL-IMRAN 

الآية : 200

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱصۡبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi ambao mmeamini vumilieni na yote yanayowapata, na yavumilieni matatizo ya maadui mnayokumbana nayo, na lindeni mipaka ya nchi dhidi ya maadui, na mcheni Allah ili mfaulu