فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Basi likawachukua tetemeko (la ardhi) wakawa wameangamia majumbani mwao huku wamepiga magoti
ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَاۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَانُواْ هُمُ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Ambao wamemkadhibisha (wamempinga) Shuaibu (waliangamia na kutoweka majumbani mwao) kama vile hawakuwemo kabisa humo. Ambao walimkadhibisha Shuaibu walikuwa hasa ndio wenye hasara
فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡۖ فَكَيۡفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ
Basi (Shuaibu) aliachana nao (aliwapuuza) na kuwaambia: Enyi watu wangu, kwa hakika kabisa, nimewafikishieni ujumbe wa Mola wangu na nimekupeni nasaha. Basi inakuwaje niwasikitikie watu makafiri?
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ
Na hatukumpeleka Mtume yeyote katika mji wowote isipokuwa kwamba tuliwashikisha adabu watu wake kwa mateso na shida ili wapate kunyenyekea
ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Kisha tulibadilisha sehemu ya baya tukaweka zuri mpaka wakaneemeka (na neema zilipowazidi) na wakasema: Ziliwapata baba zetu shida na raha, kwa sababu hiyo, tuliwashika (tuliwaadhibu) ghafla na ilhali hawatambui
وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡقُرَىٰٓ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَفَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَرَكَٰتٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذۡنَٰهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Na lau kama watu wa miji wangeamini na kumcha Allah tungewafungulia baraka nyingi kutoka mbinguni na ardhini na lakini wamekadhibisha kwa sababu hiyo tumewashikisha adabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wanayachuma (wanayafanya)
أَفَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا بَيَٰتٗا وَهُمۡ نَآئِمُونَ
Hivi watu wa miji wamejia-minisha kwamba haitawajia adhabu yetu usiku na ilhali wamelala?
أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ
Au watu wa miji wamejiaminisha kwamba haitawajia adhabu yetu mchana na ilhali wanacheza?
أَفَأَمِنُواْ مَكۡرَ ٱللَّهِۚ فَلَا يَأۡمَنُ مَكۡرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Hivi wamejiaminisha vitimbi vya Allah? Basi hawajiaminishi vitimbi vya Allah isipokuwa tu watu wenye hasara
أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ
Hivi haijawa muongozo kwa wale wanaoirithi ardhi baada ya watu wake (walioangamizwa) kwamba lau tungetaka tungewapa msiba (mitihani na matatizo) kwa sababu ya madhambi yao, na tungepiga lakiri katika nyoyo zao wakawa hawasikii?
تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hiyo ni miji tunakusimulia miongoni mwa habari zake. Na kwa hakika kabisa, Mitume wao waliwajia na hoja za wazi wazi. Basi hawakuyaamini yale waliyoyakadhibisha hapo kabla. Kama hivyo Allah anazipiga lakini nyoyo za makafiri
وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ
Na hatukupata kwa wengi wao (utekelezaji wa) ahadi yoyote na hakika kabisa, tumekuta wengi wao ni waovu
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Kisha tulimtuma Musa kwa Aya zetu baada yao, aende kwa Firauni na kundi lake la mamwinyi, basi wakazidhulumu (wakazipinga) Aya hizo. Basi ona namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu
وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na Musa akasema: Ewe Firauni, hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ
Ni haki kwangu kutomsemea Allah ila lile la haki tu. Hakika, nimekujieni na hoja za wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi (zinazothibitisha ukweli wangu). Basi waachie Wana wa Israili (wawe huru) wawe pamoja na mimi (kwenda kwenye mji wa baba zao)
قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
(Firauni) Akasema: Kama umekuja na hoja basi ilete kama wewe ni miongoni mwa wasemao kweli
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Basi (Musa) akaitupa chini fimbo yake na ghafla ikawa nyoka wa dhahiri
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ
Na akautoa kwa nguvu mkono wake (kutoka katika nguo yake) na ghafla ukawa mweupe kwa wanaotazama
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Mamwinyi katika watu wa Firauni wakasema: Hakika, huyu ni mchawi mjuzi sana
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
Anataka kukutoeni katika ardhi (nchi) yenu (kwa uchawi wake). Basi mnaniamuru (mnanishauri nifanye) nini?
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema: Mpe muda yeye (Musa) na ndugu yake na tuma katika miji yote (watu) watakaofanya kazi ya kukusanya (wachawi)
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
Wakuletee kila mchawi mahiri sana
وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Na wachawi walikuja kwa Firauni wakasema: Hivi sisi tutalipwa endapo tutashinda?
قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
(Firauni) Akasema: Ndio, na kwa hakika kabisa, nyinyi mtakuwa miongoni mwa watu wangu wa karibu sana
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
(Wachawi) Wakasema: Ewe Musa, ama tupa (toa wewe uchawi wako) au sisi tuwe wa mwanzo kutupa (kutoa)
قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ
(Musa) Akasema: Tupeni (Toeni). (Wachawi) Walipotupa (walipotoa uchawi wao) waliyaroga macho ya watu na waliwatisha na walikuja na uchawi mkubwa sana!
۞وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ
Na tulimfunulia Musa Wahyi kwamba: Tupa fimbo yako, na ghafla ikawa inameza vyote wanavyovizusha
فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Basi haki ikathibiti na vikabatilika vyote walivyokuwa wanafanya
فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ
Basi (wachawi) hapo wakashindwa na wakabadilika wakawa wanyonge!
وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ
Na wachawi wakaporomoka chini kumsujudia (Allah)