فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?
مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ
Mna nini hata hamsemi?
فَرَاغَ عَلَيۡهِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia
فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ
Basi wakamjia upesi upesi
قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ
Akasema: Hivyomnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe?
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ
Na hali Allah ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!
قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنٗا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!
فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدٗا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa
رَبِّ هَبۡ لِي مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa wema
فَبَشَّرۡنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمٖ
Basi tukambashiria mtoto aliye mpole
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعۡيَ قَالَ يَٰبُنَيَّ إِنِّيٓ أَرَىٰ فِي ٱلۡمَنَامِ أَنِّيٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفۡعَلۡ مَا تُؤۡمَرُۖ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri
فَلَمَّآ أَسۡلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلۡجَبِينِ
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji (kifudifudi ili amchinje)
وَنَٰدَيۡنَٰهُ أَن يَـٰٓإِبۡرَٰهِيمُ
Tulimwita: Ewe Ibrahim!
قَدۡ صَدَّقۡتَ ٱلرُّءۡيَآۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡبَلَـٰٓؤُاْ ٱلۡمُبِينُ
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri
وَفَدَيۡنَٰهُ بِذِبۡحٍ عَظِيمٖ
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu (mnyama wa kuchinja) mtukufu
وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye
سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ
Iwe salama kwa Ibrahim!
كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema
إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini
وَبَشَّرۡنَٰهُ بِإِسۡحَٰقَ نَبِيّٗا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema
وَبَٰرَكۡنَا عَلَيۡهِ وَعَلَىٰٓ إِسۡحَٰقَۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحۡسِنٞ وَظَالِمٞ لِّنَفۡسِهِۦ مُبِينٞ
Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa vizazi vyao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi
وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Mussa na Harun
وَنَجَّيۡنَٰهُمَا وَقَوۡمَهُمَا مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa
وَنَصَرۡنَٰهُمۡ فَكَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda
وَءَاتَيۡنَٰهُمَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلۡمُسۡتَبِينَ
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha
وَهَدَيۡنَٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka
وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِمَا فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye
سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Iwe salama kwa Mussa na Harun!